Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Mashemeji, Mawifi na watu baki hawana hiyo nafasi kwa mke wangu, kwanza mawifi zake wakifika anakuwa amepona na kazi Labda zile ambazo nataka azifanye yéyé mwenyewe kwaajili yangu.

Lakini pia niwekee sawa kidogo huwezi kuwaingiza kaka zangu jikoni au kazi nyingine za ndani na kwanza hawawezi kumaliza hâta Siku moja kwangu.

Hapa home nipo na dogo langu la mwisho tangu likiwa form one mpaka Sasa form six linatumwa kila kazi hâta kupika and so on na kila kitu kipo normal tu tunaishi kwa amani kabisa.

Unajua mimi sipo hapa kumgandamiza mwanamke, kuna vitu vingine tu vya kutumia akili za kuzaliwa kujua kwamba hili ni jukumu langu au laah, hili naweza kwamwambia mume wangu au laah, hili naonewa au laah........lakini swala la kumtuma mmeo kikombe mbele za wageni ili wewe uendelee kuchati aiseeeeeh..!!
 
Hiki ndicho ninachokisisistiza humu ndani, mwanaume afanye kazi kwa matakwa yake na sio kwasababu katumwa na mkewe.
Na mwanaume mwenye akili hawezi acha mwenzie anapambana na kazi zote pekeyake akiwa hoi amechoka,yeye amekaa tu.

Hivi wenzetu mnawezaje aisee!!
Binafsi nikitegea kazi huwa najisikia vibaya sana.
 
Oh safi sana


Sasa mbona la kuchukua kikombe uliwatesa wenzio?[emoji16][emoji38]
 
Oh safi sana


Sasa mbona la kuchukua kikombe uliwatesa wenzio?[emoji16][emoji38]
Hivi nifike kwa mwanaume mwenzangu for the first time hapohapo nijue vikombe vilipo kisha nikachukue nitafute maji yalipo nijimiminie ilihali mwenyeji umekaa pembeni yangu busy una chati? Hiyo ni nyumba au geto?

Nikichokifanya ni kuomba maji jamaa kamuangalia wife wake, wife nae kamtuma aaahahaha aiseeeh😄
 
❤️❤️❤️🥰
 
Sasa si ulikiona kikombe?
Wewe kwanini unafika kwa watu na kuanza kuwasumbua?[emoji846]
 
Wasukuma wana hizi tabia.
Kuna huyo dada yangu mmoja ameolewa na msukuma aisee nadhani siku ya mwisho atatunukiwa taji ya ushindi yule dada.

Hataki mtoto wa kiume aguse jikoni na ana wa kiume tu.
Ndiyo baadaye mitoto itaanza kuishi kama milemavu.
Mtoto wangu wa kiume miaka 7 anajiandalia breakfast yake mwenyewe kila siku kabla hajaenda shule + kujiandaa mwenyewe mie ni kumpasia tuu nguo
 
Sasa hawa wanaolialia humu sidhani kama package hii ya mumeo wanayo.

Hawana.
 
Kwanza najichimbia zangu room sitaki shida mimi.

Kazi zako ziniumize kichwa,na washkaji zako waje nisumbuke! Hapana kwa kweli.
Ni bora ukajichimbie huko chumbani kuliko uwepo hapo karibu alafu unitume 😄.

Na kwa hiyo mentality aliyekuoa akija home na rafiki zake, utawakimbia uende chumbani ili mmeo ndo aandae chakula na kila kitu.

Aiseeh ni halali vilio vitawale humu MMU😁
 
Ukitaka kuja na wageni useme mapema,
Siyo unakurupuka tu na kunijazia nyomi la watu nianze kuteseka na kuvuruga ratiba zangu.

Ninaweza nipike ndiyo lakini nipo mzito mno kujichanganya na watu...anti social na introvert wa aina yake...kwa hiyo huwa naangalia.
Kusocialize kwangu ni mtihani.

Wewe ukija bila taarifa basi itakuwa kwako.
 
Hukumpenda kweli toka moyoni ulimpendea hela na connection baada ya kuingia ndoani ukajua kuwa ndoa ni zaidi ya hela, ikiwemo bond and chemistry hapo ndio ukachaganyikiwa.

Pole na move on with life maana inferiority ilikuwa inakusumbua
Yeye bila shaka ndo alichaguliwa sio yeye aliyechagua, hivi kumpiga kote ngumi yeye bado yupo tu, bila shaka yeye ndo kachaguliwa na kupendwa
 
Utasifia kwenye hamna? Sidhani kama kuna boya atakeshindwa kutoa complement kwa mwanamke anaejitambua.

Hao wanawake wakufanyiwa hayo yote hawamo humu.
 
Utasifia kwenye hamna? Sidhani kama kuna boya atakeshindwa kutoa complement kwa mwanamke anaejitambua.

Hao wanawake wakufanyiwa hayo yote hawamo humu.
Hata nyie wanaume wa package hizo za mumewa huyo dada hampo humu
 
Need I say more? Acha nitulie as long as ninae anaenielewa inatosha, nyinyi pia mtapata hao mtakaokuwa mnawatuma ili mpate muda wa kuchati humu jf.

Take an example (mfano), hapo ulipokaa saivi ni saa saba, kisha mmeo aje anadai ana njaa alafu umwambie akapike mwenyewe ili wewe uendelee kukaa hapo ujibizane na mimi kwenye simu😄. Really? Hayo ndo mapenzi mnayotaka? Mtawapata tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…