NGOMEKONGWE2021 - Tupo wengi, kiongozi. Mie pia watoto 4 kama wewe. Miaka 12 ya ndoa. Mama wa nyumbani. Tatizo hawezi kujifunza kitu. Kila siku ni shida tupu ndani ya nyumba. Mfano, hawezi kutoa magamba ya samaki yakaisha yote kabla ya kumpika samaki. Chakula anavyonunua kwenye supermarket, ndivyo navyokipika! Anaweza kupika nyama ya kuku na kinyeo chake ama bado kuna kiasi fulani ya vinyoya!! Hata nikimweleza vipi, akili yake haishiki!! Hataki niwafundishe watoto. Nikiwakosoa watoto kwa namna ya kuwafundisha, anakuja juu. Watoto wananiona mimi shetani na yeye malaika. Amejenga chuki kati yangu na watoto ambao bado ni wadogo tu. Sijawahi kumpiga ama kuchepuka lakini nilikwisha mwambia kuwa tungekuwa tunaoa mara ya 2, nisingemuoa tena. Sina hamu tena hata ya kulala naye.