Yaani unampiga mkeo kisa hajapika au hajafua! Hivi sijui kwanini mnafananisha mwanamke anayetafuta pesa na anayeshinda nyumbani, mkae mkijua hawa ni wanawake wa aina mbili tofauti yaani hawatakaa wawe sawa, kama ambavyo mwanaume tajiri na mwanaume masikini hawako sawa kwenye hii dunia!
Mwanamke anayekusaidia wewe kutafuta pesa usitegemee ataweza kutimiza majukumu yake kikamilifu kama anavyofanya mama wa nyumbani, ninyi wenyewe si ndiyo mmetaka haya mambo ya kusaidiana maisha, kwa kukimbia majukumu yenu! Basi kama vipi oeni wanawake wasiosoma muwahudumie tu!