Tujaribu kuvaa uhusika wa wanawake tutaona ugumu wanaopata.
Au wanaume tujifunze kuwasaidia kazi wake zetu tunaweza angalau kuona ugumu wa kazi hizo.
Mimi nakumbuka wakati wife analea mtoto wetu mchanga hatukuwa na binti wa kazi nilikuwa naamka saa kumi kasoro nakosha vyombo,nafua nguo,nadeki,nasafisha jiko,napika chai,natia maji chooni ya kutumia then saa mbili nakoga naenda kwenye ishu zangu,yeye wife anabaki anapambana na mtoto.
Tulikiiishi kipindi hiko bila binti wa kazi,lakini hizo kazi zote ningemuachia mzigo ungezidi kuwa mzito.