Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

Miaka 15 ungeamua kuwa selemala ungekuwa fundi mzuri sana. Ajabu ulichagua kwenda kujaza Majibu na maswali hauna.

Kimbembe maswali yanakuja majibu hayafit.
Maswali Yale Yale ila yanataka majibu tofauti.

Chagua jibu lililo sahihi zaid hiki ndio kilikuwa kisanduku kuwa lazima wore tufanane.
#warthog
 
For sure, now I can relate
Just imagine,tukiacha elimu ya msingi ambayo ndo muhimu unapoteza miaka minne plus miwili kuhitimu kidato cha sita. Ikiwa ni binti tayari ushavunja ungo na vyombo vingine vya jikoni,ikiwa ni mvulana ushaota nywele hadi maeneo yasiyofikika kirahisi...unaacha kuzaa kuongeza wapiga kura,serikali inarubuni wazazi wauze mifugo ili upelekwe day care in the name of University,miaka mitatu ,minne ama mitano kwa kozi baadhi,hafalu unalipia martenity gown 50k kwa jina la joho ili upewe karatasi inayoitwa shahada. Unarudi nyumbani kusikilizia mchongo na umri ushakupiga kisogo...daah tutafika uzeeni tukiwa tumechoka sana! Na tukifa tunakutana na moto wa milele ukichochewa na nyampara Ben Netanyahu!
 
Elimu uliyoisoma bado ina umuhimu kwako na itaendeles kuwa ya muhimu na hukupoteza muda darasani. Ukitaka kuamini hayo angalia haya uliyoandika yadhiirisha hukupoteza muda shuleni
 
Mleta mada uko sawa kwa upande wako,ila nlitaka niseme tushukuru Mungu kwa kila jambo ingawa hatupati kazi au hatujiajiri kwa tuliyoyasomea ila kupitia Elimu tunakutana na watu mbalimbali kwa urahisi ambapo tunajifunza mengi kuanzia tabia za makabila,Fedha,nidhamu n.k
 
Ni kweli mkuu tatizo huo muda ni mwingi sana kujifunza ivo vitu kupitia mwamvuli wa elimu, it's not worth it.

Elimu ya mtaa inafundishwa mtaani na ya shule ni mofimu tu na Archimedes principle kwa sana, that's all
 

Ukweli ni kuwa Elimu ni muhimu sana
Ukiangalia vizuri utajua kuwa, hata unachokifanya sasa hivi ni kwa sababu ya Elimu hata kama hutumii ulichokisoma chuoni moja kwa moja;
Kwa Bongo wanaofanya walichokisoma sio wengi sana japo ukweli upo palepale kuwa wengi wamesoma na kupata maarifa ya kufanya vitu vingine

1. Kusoma kunakupa maarifa ya kufikiri nje ya boxi
2. Kuna kukutanisha na watu wenye tabia tofauti tofauti (mbaya na nzuri) hivyo hukuandaa kwani hizo tabio za ajabu ajabu ndizo utakutana nazo mtaani
3. Kuna kupa mwanga (exposure) ya kufanya maamuzi kwa usahihi zaidi
4. Wengi wamepata connection za kuwasaidia kupitia marafiki waliowapata shuleni/chuoni - fursa
5. Mwenye Elimu (anayejitambua) anauwezo wa kufanya kazi kwa usahihi zaidi hata kama hajaisomea
 
Nakubaliana nawewe kwa 25%, unachojaribu kuongea ni kama myth ambayo haiapply kwa kila mtu aliepita shule
 
tunakoelekea wazazi kabla ya kupeleka tu watoto shule tutakuwa tunakaa chini na kufanya upembuzi mrefu sana.

hasa baada ya kijana kuhitimu 4 au 6
Katika vitu vya kipuuzi ni elimu ya kidato cha 5&6
Inatakiwa kufutwa haraka kwakuwa ni kupotezea watu muda wa kujijenga kimaisha
Mtu akimaliza kidato cha nne akafanye anachopenda mfano; ufundi, upishi, massage, udereva, uhasibu, biashara, nk
Tuache kupotezeana muda na pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…