Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

ANGALIZO: Huu uzi hauwahusu wale ambao bado wapo kwenye industry ya Elimu bali ni kwa wale waliokwishatoka nje ya Game tu ⚠️

Ughonile..

kuna muda nikiwa idle nakumbuka muda niliopoteza shule kusoma hususani kuanzia A-Level na University naishiwa nguvu, nikitazama vyeti vyangu, nikiangalia picha nilizopiga maeneo tofauti tofauti enzi nasoma sometimes najutia sana.

Kutoboa kupitia Elimu ya Bongo ni ngumu sana either kwa kuajiriwa au kujiajiri kupitia iyo elimu uliyoisotea miaka yote iyo takriban zaidi ya miaka 15 ni kizungumkuti.

Hata ikitokea umeajiriwa na hiyo elimu yako kutoboa bado ni ngumu unless uwe mtu wa kupiga danadana huko kazini kwako or else uridhike tu na huo mshahara unaokuwezesha kumudu kujenga na kununua kiusafiri chako ingawa still usipoingia Bank/microfinance kukopa pia bado ni mtiani.
nikiangaliaga ivi vyeti vinanifikirisha sana ukizingatia nilivipata kwa tabu sana. Mtaani kwetu na familia kwa ujumla waliwekeza sana kwangu na walikua na matumaini makubwa sana namimi pengine ningekuja kuwa mtu mkubwa sana hapa nchini kutokana na juhudi nilizokuanazo katika kusoma.

Good thing ni kwamba baada tu ya kugraduate chuo niliweza kufikiria nje ya box na mpaka hapa nilipo namshukuru Mungu, sipati picha ningeuface vipi mtaa na jamaa zangu pindi ambapo ningekua naenda kuwatembelea ilhali sieleweki kisa ajira hamna! Inafikirisha sana

Saivi nikienda kijijini nishajiwekea utaratibu nahakikisha niko full equipped (tai ndefu, ndinga japo ya kuazima na vibunda vya kutosha) sifanyi kwa sifa bali nafanya ili wajivunie kijana waliekuwa wamewekeza kwake hajawaangusha na kutowakatisha tamaa ya kusoma wadogo zangu mtaani.

All in all all is well

Vipi wenzangu na mie hali ikoje
Nipo hapa mkuu.
Sema haukupotea kwa 100% maana hqta akili ya kuishi inayonipa maisha imetokana na experience ya chuo.
 
Just imagine,tukiacha elimu ya msingi ambayo ndo muhimu unapoteza miaka minne plus miwili kuhitimu kidato cha sita. Ikiwa ni binti tayari ushavunja ungo na vyombo vingine vya jikoni,ikiwa ni mvulana ushaota nywele hadi maeneo yasiyofikika kirahisi...unaacha kuzaa kuongeza wapiga kura,serikali inarubuni wazazi wauze mifugo ili upelekwe day care in the name of University,miaka mitatu ,minne ama mitano kwa kozi baadhi,hafalu unalipia martenity gown 50k kwa jina la joho ili upewe karatasi inayoitwa shahada. Unarudi nyumbani kusikilizia mchongo na umri ushakupiga kisogo...daah tutafika uzeeni tukiwa tumechoka sana! Na tukifa tunakutana na moto wa milele ukichochewa na nyampara Ben Netanyahu!
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Katika vitu vya kipuuzi ni elimu ya kidato cha 5&6
Inatakiwa kufutwa haraka kwakuwa ni kupotezea watu muda wa kujijenga kimaisha
Mtu akimaliza kidato cha nne akafanye anachopenda mfano; ufundi, upishi, massage, udereva, uhasibu, biashara, nk
Tuache kupotezeana muda na pesa.
Taifa haliwezi kuwa na viongozi wajinga kama wewe
 
My friend, kuna darasa la saba kibao wako more financially stable kuliko maprofesa wengi hapa nchini so sijui unaongelea maarifa yapi.

Binafsi nafanya mitikasi yangu kariakoo, %kubwa ya wapemba, wakinga na wachaga ambao wanamiliki biashara kubwa hapa Kariakoo walikimbia shule.

What's the point of regarding yourself as educated person with different honors while you got nothing in the Bank man?

Which knowledge are you talking about specifically?
Unaonekana una stress za maisha pole utavuka
 
Ngoja nimtafute Elon Musk tajiri wa kwanza Duniani kumiliki utajiri wa USD 248B nimuulize kama elimu imemusaidia au haijamsaidia.
Musk moved to the United States in 1992 to study business and physics at the University of Pennsylvania. He earned an undergraduate degree in economics before continuing on to earn a second bachelor's degree in physics. Musk went to Stanford University in California to earn a Ph.D. in energy physics after leaving Penn
 
Huu ufafanuzi ndio umenisaidia zaidi hoja yangu kuwa lengo la shule sio kupata fedha au ajira.
Elimu ni uwekezaji kama ilivyo shares, stocks na bonds.

Ni kitu ambacho wazazi wetu waliwekezewa na babu na bibi zetu wakafanikiwa vizuri kubadilisha mazingira ya maisha kule vijijini.

Imani hio wamekuwa nayo na wakathubutu kuwekeza kwetu wakitarajia the same results. Hakuna uwekezaji usio na faida mkuu ina maana mtu akitoboa akaingia BOT kama mweka hazina mkuu tu lazma hela ingetembelea familia yake tu. Afisa mkuu wa manunuzi wa serikalini hawezi kusikitika juu ya elimu aliyonayo sababu imempa maisha.

In contrary, kama hujafanikiwa kupata channel yeyote ya namna hio baada ya masomo hapo ndipo uwekezaji unakuwa wa hasara.
 
Elimu ni uwekezaji kama ilivyo shares, stocks na bonds.

Ni kitu ambacho wazazi wetu waliwekezewa na babu na bibi zetu wakafanikiwa vizuri kubadilisha mazingira ya maisha kule vijijini.

Imani hio wamekuwa nayo na wakathubutu kuwekeza kwetu wakitarajia the same results. Hakuna uwekezaji usio na faida mkuu ina maana mtu akitoboa akaingia BOT kama mweka hazina mkuu tu lazma hela ingetembelea familia yake tu. Afisa mkuu wa manunuzi wa serikalini hawezi kusikitika juu ya elimu aliyonayo sababu imempa maisha.

In contrary, kama hujafanikiwa kupata channel yeyote ya namna hio baada ya masomo hapo ndipo uwekezaji unakuwa wa hasara.
Kipindi tuko shule wazee wa back bencha tulikuwa tunajazana ujinga eti ambao hatuko vizuri kwenye masomo ndio tunakuja kuwa matajiri aisee huku kitaa tukikutana tunacheka tuu😁
 
Back
Top Bottom