Mkuu sijui umeamua kufikiria vipi... Lakini bila elimu hii hii unayoiona hapa duniani tungeishi kijima hali Ingekua duni vibaya mno mfano, unaona wanavyoishi wahadzabe nje na kuwinda hawajui kitu chochote.
Ukitaka ujue umuhimu wa kitu chochote kile uwe hauna icho kitu arafu kinahitajika kwa wakati huo.
Yaani huoni umuhimu wa elimu ni kwasababu unayo tayari sasa jaribu kuvaa viatu vya mwamba mmoja alieishia lasaba kijijini huko. Just imagine hata ku search Habari mtandaoni ingekua kipengele, tufanye unajua ku Google haya sasa utaelewa vipi zile tutorial za YouTube na maskills mengi ya maana mtandaoni, yanatumia lugha za kigeni kizungu.
Ila kama tunasoma kuajiliwa basi tatizo sio elimu bali tatizo ni nafasi na fursa za ajira.
Yaani katika hili elimu haina nogwa hakuna cha kusema mtaala wa elimu ya bongo unatuandaa kuajiriwa na wala sio kujiajiri ni namna ya kumkwepa hali halisi iliyopo kuwa fursa za ajira ni chache wahitaji wengi... Yaaaani!
a). Sector nyingi Tanzania zinazalisha nafasi chache za ajira. Pia
b). Fursa zipo kem kem ila Mazingira(miundombinu, mitaji, sera tafiti, sapoti serikalini) Ni changamoto.