Wale tuliopoteza muda shule kusoma tukutane hapa

🤣🤣🤣
 
Mkuu sijui umeamua kufikiria vipi... Lakini bila elimu hii hii unayoiona hapa duniani tungeishi kijima hali Ingekua duni vibaya mno mfano, unaona wanavyoishi wahadzabe nje na kuwinda hawajui kitu chochote.

Ukitaka ujue umuhimu wa kitu chochote kile uwe hauna icho kitu arafu kinahitajika kwa wakati huo.

Yaani huoni umuhimu wa elimu ni kwasababu unayo tayari sasa jaribu kuvaa viatu vya mwamba mmoja alieishia lasaba kijijini huko. Just imagine hata ku search Habari mtandaoni ingekua kipengele, tufanye unajua ku Google haya sasa utaelewa vipi zile tutorial za YouTube na maskills mengi ya maana mtandaoni, yanatumia lugha za kigeni kizungu.

Ila kama tunasoma kuajiliwa basi tatizo sio elimu bali tatizo ni nafasi na fursa za ajira.

Yaani katika hili elimu haina nogwa hakuna cha kusema mtaala wa elimu ya bongo unatuandaa kuajiriwa na wala sio kujiajiri ni namna ya kumkwepa hali halisi iliyopo kuwa fursa za ajira ni chache wahitaji wengi... Yaaaani!

a). Sector nyingi Tanzania zinazalisha nafasi chache za ajira. Pia

b). Fursa zipo kem kem ila Mazingira(miundombinu, mitaji, sera tafiti, sapoti serikalini) Ni changamoto.
 
Mimi nakumbuka niliacha shule kipindi nipo Kidato Cha pili nilikuwa nafanya Biashara ya samaki kupeleka vijijini kwenye minada niliweza kupandisha mtaji Wangu sijui nini. Kilinipeleka tena shule Daah najuta sana
 
Watu wanafikiri elimu aliyoanzisha mkoloni Tanzania ya kuchanganua sentensi kwa njia ya matawi na kukariri theories za akina Newton ni sawa na Elimu inayotumiwa kuinnovate vitu mfano viwandani, too late to be discussing this
 
Hapo ndo kiwango chako cha kufikiri kilipoishia au namna gani mkuu? No way
 
Tatizo la wasomi wengi Tanzania 🇹🇿 wameifanya elimu kama sehemu ya kuwafanikisha kiuchumi na maendeleo ya mali na ndio maana pesa zao zimejaa dhuluma, wizi, utapeli na kila aina ya uchafu na wasomi wengi wenye pesa hawana utu, adabu, hofu ya Mungu na maadili, elimu ina mjenga mtu kubadili mawazo na kupanda assets kama: Attitude, knowledge na skills.

Msomi mwenye upungufu wa vitu tajwa anahitaji ajira na akiwa na pesa ana maringo na ukatili kiutendaji na lugha kiuwasilishaji.
 
Personal point of view
 
Mfumo wa elimu unaongeza umaskini. Na unatoa matajiri wachache ili waweze kuwasumbua wale wengi kuwa wafanyakazi wa bei rahisi. Huu nfumo upingwe sana na maskin sababu hao ndo unawasumbua na hata kupata kazi hawapati
Ndio maana unatoa watu ambao tunahangaika na ajira. Hatugundui chochote wala hatuwezi kutawala mazingira.
 
Una uwasilishaji mbovu sana wa lugha na uandishi mwepesi usiyo na kina cha uerevu.

Unaweza ukawa na point nzuri ila namna ya uandishi kilugha na mpangilio wa maneno kiubaguzi ikaharibu maana ya kusudio lako lililo jema.
 
Ni sawa lakini hio ni asilimia ndogo sana na maisha ya ajira yakishaisha wanakuwa na maisha magumu sana mkuu ni Bora ukajiajir na maisha ya kawaida ndio mazuri kwa sababu maisha halisi yapo mtaani sio kwenye ofisi unapulizwa na AC hayo maisha hayafai tunayaona mtaani huku
 
Hapo ndo kiwango chako cha kufikiri kilipoishia au namna gani mkuu? No way
Mkuu elimu unaona kama haina maana ni kwasababu umeipata tayari.

Umuhimu wa kitu huwa unaonekana ukiwa huna hicho kitu.

Ukija katika national level elimu umuhimu wake uko pale pale ila kinaonekana haina umuhimu ni kwasababu elimu imekua sana au wasomi wamekua wengi kuliko uhitaji /uhitajikaji wao katika mfumo.

Demand & supply "bidhaa ikiwa adimu ndio inapanda thamani ikiwa tele inashuka thamani. Labda tutokee hapa nadhani ulikua unamaanisha hivi na sio kwamba elimu haina umuhimu kabisa.

Mahitaji na upatikanaji.:
We unafikiri kwanini mafuta Fuel ina thamani kubwa kushinda maji. Na wakati maji ndio muhimu mara million kwa kiumbe yeyote kushinda hayo mafuta.

Kuna watu hawana hiyo level ya elimu na wanatamani sana wangekua nayo, wengine wanajilaumu sana maana walipata fursa lakini waliichezea Leo wanajuta.
 
Iyo form 6 itoe, pure wastage of time
Nimesoma f6 nikiwa mtu mzima na watoto nikiwa nao( nilirudia f4 ili nipate angalau D ya physics niweze kusoma diploma ya kozi flani ambapo matokeo yakaja nina maksi nzuri, nikasema acha nijaribu advance PCB hahaha! Natatumia mfano mdogo ili uone umuhimu wa advance hata kwenye mambo mdogo tu!
Cell (plant/animal) niliyoisoma o-level haikuwa Sawa na niliyoisoma advance, ila je hiyo cell inanisaidia nini sasa hivi? Hapa ndipo ninapotaka kukupa ujumbe wa kwanini advance ni muhimu sana tena Sana twende pamoja.

Napenda kusoma vitabu na uzee wangu huu, majuzi kuna kitabu nimekutana nacho kinaelezea kuhusu "mitochondria" sehemu ya cell ambamo ndimo kwenye "miujiza" ya kinga ya magonjwa sugu kama kansa, kuzuia kuzeeka mapema, nk,
Uelewa wangu wa cell katika topic ya "cytology" umenifanya nielewe kitabu hiki vizuri Sana, nataka kuwa mtaalam wa tiba asili na kutibu kansa! Lol!
 
Una uwasilishaji mbovu sana wa lugha na uandishi mwepesi usiyo na kina cha uerevu.

Unaweza ukawa na point nzuri ila namna ya uandishi kilugha na mpangilio wa maneno kiubaguzi ikaharibu maana ya kusudio lako lililo jema.
Okay
 
siku ukiacha kulalamika na kuanza kufanya kazi utakuwa umepiga hatua kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…