Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS

Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS

Wala hatuhitaji kuwajua - huo muda tunatoa wapi na inasaidia nini?? Wao wapambane na majukumu yao, na sisi tupambane na ya kwetu - mwisho wa siku kila mtu anataka kupeleka chochote mezani kwa watoto wake
Halafu ni ushamba tu,kusujudia kazi ya mtu mwingine ambayo haikusaidii wewe na familia yako, nchi inaliwa na wao wapo busy kweli kushona Kaunda suti, na kutufuata vijiweni kutusikiliza et nani tunampiga spana ndio kazi wanazozifanya
 
Wewe ndiye umepatia, hao informer ndio hujinadi mtaani kuwa usalama wa taifa.
Atuambie kwanza je DSO na RSO Hawa ni wafanyakazi TISS au ma agent na kama ni wafanyakazi wa TISS mbona wanafahamika lakin pia na wale walio chini yao ni ma agent au wafanyakazi wa TISS mbona tuna wajua? Halafu pia huyo jamaaa inaonekana anaujua vizuri mfumo wa TISS anijuze tu mishahara Yao maana tusije tukapoteza muda kujadili watu ambao mishahara na marupurupu hayalingani hata na afisa matapato wa TRA
 
acha uongo.na wale wanaotembea na samia?
Hao ni walinzi tu na siyo majasusi.

Hao walinzi kazi yao kuu ni kumkinga Rais asidhurike na shambulizi lolote lile, ikiwezekana hata kutumia miili yao kama ngao ya kumkinga Rais.

Hao walinzi, hata kama wapo chini ya idara moja na majasusi, majukumu yao ni tofauti kabisa.

Walinzi ni walinzi tu na kazi yao ni kumlinda Rais, makazi yake, viongozi wengine wa serikali.

Kwa mfano, endapo inatokea Rais anashambuliwa kwa silaha, hao walinzi walio karibu na Rais kazi yao si kujibu hayo mashambulizi.

Kazi yao hapo ni kumkinga Rais na kumwondoa kwenye hilo eneo lenye hatari.

Wataojibu mashambulizi ni wale wanaobebaga zile bunduki kubwa/ ndefu.
 
Hao ni walinzi tu na siyo majasusi.

Hao walinzi kazi yao kuu ni kumkinga Rais asidhurike na shambulizi lolote lile, ikiwezekana hata kutumia miili yao kama ngao ya kumkinga Rais.

Hao walinzi, hata kama wapo chini ya idara moja na majasusi, majukumu yao ni tofauti kabisa.

Walinzi ni walinzi tu na kazi yao ni kumlinda Rais, makazi yake, viongozi wengine wa serikali.

Kwa mfano, endapo inatokea Rais anashambuliwa kwa silaha, hao walinzi walio karibu na Rais kazi yao si kujibu hayo mashambulizi.

Kazi yao hapo ni kumkinga Rais na kumwondoa kwenye hilo eneo lenye hatari.

Wataojibu mashambulizi ni wale wanaobebaga zile bunduki kubwa/ ndefu.
kwa hao walinzi ni wagambo?
 
Wale wa Enzi za Mwalim ndiyo usingewajua kirahisi.
Hata hivyo kama wewe ni raia mwema usihangaike kuwajua au kutowajua!
Na nahisi hata JD zao zimebadilika wale wa enzi za mwalimu walikuwa very committed na nchi Yao Hawa wa saizi wanataka tuwe tuna sifu na kuabudu tu ukienda kinyume wanakushughulikia🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo hata mtu asiekua mtumishi TISS anaweza kupewa majukumu ya RSO?
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Hivi ajira zao Huwa wanatangaza lini?.Maana nikiangalia kwenye mtandao Huwa siwaoni
 
Ukindoa Mkurugenzi wa TISS, ambaye anajulikana, ni kosa la jinai kumuanika mtumishi wa TISS.
Kwani nimekula kiapo cha kutomwanika?,
yeye ilikuwaje mpaka mimi nikamfahamu
Huoni kwamba yeye ndiyo mzembe hapo na hafai katika hiyo nafasi tena?
 
Katika mji Mmoja mkoa Fulani Kuna chizi alitokea...na akawa anapenda kukaa karibu na kikundi Fulani kilichojitenga bila watu hao kujijua(kutokana na hisia zangu alikua anawachunguza Hawa jamaa)..lakini chizi huyu Kuna siku alipigana na chizi mwingine na akamkalisha..lakini upiganaji wake aliotumia ni ule wa kuonyesha Yuko well trained na watu wakaona yule chizi kiboko na wakawa hawamchezei,,siku Moja usiku chizi huyu alinikuta nafanya mazoezi ..nikamuomba acheze kata nimuone..akacheza vizuri tu ..ila kuongea ikawa kama anaongelea kifuani..nikamuomba koneksheni..alipotea hapohapo...from that day onward huyu chizi hakuwahi kuonekana Tena.. ....je wajuvi wa mambo je chizi huyu ndio hao Tiss au alikua chizi tu..??
 
Katika mji Mmoja mkoa Fulani Kuna chizi alitokea...na akawa anapenda kukaa karibu na kikundi Fulani kilichojitenga bila watu hao kujijua(kutokana na hisia zangu alikua anawachunguza Hawa jamaa)..lakini chizi huyu Kuna siku alipigana na chizi mwingine na akamkalisha..lakini upiganaji wake aliotumia ni ule wa kuonyesha Yuko well trained na watu wakaona yule chizi kiboko na wakawa hawamchezei,,siku Moja usiku chizi huyu alinikuta nafanya mazoezi ..nikamuomba acheze kata nimuone..akacheza vizuri tu ..ila kuongea ikawa kama anaongelea kifuani..nikamuomba koneksheni..alipotea hapohapo...from that day onward huyu chizi hakuwahi kuonekana Tena.. ....je wajuvi wa mambo he chizi huyu ndio hao Tiss au alikua chizi tu..??
Huyo atakuwa Chizi Maarifa!!
 
Hawana nidhamu ya kazi.

Uncle wangu alikuwa Mkurugenzi wao kwa miaka na miaka nimekua najua "Uncle anafanya kazi Ikulu" sikujua anafanya kazi gani.

Mpaka nimekuwa mkubwa mambo yamewekwa wazi kwa kuwa declassified ndiyo nikajua.
Hawa wazee walikuwa na nidhamu lakini idara pia ilikuwa very thorough kwenye recruitment. Nina mzee wangu mmoja (RIP), hakuna siku amewahi kukiri kuwa idarani, ila maisha yake, kazi zake, marafiki, tabia zake, and the kind of stories unapiga nae, unaona kabisa huyu mzee alikuwa ndani ndani kabisa.

The discpline you see in him, these people were born to be intel officer
 
Tafuta maana ya double agent,spy and informer unachanganya wali na makande.
Hapa umemaliza kila kitu, wengi wanachanganya sana hivi vitu. Wapiga kelele wengi huku mtaani ni informers na wapo kwenye sekta nyingi nyingi na tunaishi nao sana.
 
Kwani nimekula kiapo cha kutomwanika?,
yeye ilikuwaje mpaka mimi nikamfahamu
Huoni kwamba yeye ndiyo mzembe hapo na hafai katika hiyo nafasi tena?
Hiyo ndiyo sheria mkuu. Soma post #23.

Kama hutaki ongea na mbunge wako abadilishe sheria.
 
Back
Top Bottom