Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS

Duh pole sana hao wapo daily Kuna mwanangu ni muaskari ana mdoshi wake kutoka huko.
 
Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS, ni wababaishajitu na watafuta sifa. Mtumishi mwaminifu wa imani ya TISS hajulikani na wala hutakuja hata kumhisi abadani.

Teeth Overrated.
 
We umekutana na BICHWA KOMWE mkuu ndio anatabia hizo hizo
 
Hivi ajira zao Huwa wanatangaza lini?.Maana nikiangalia kwenye mtandao Huwa siwaoni
TISS haifanyi open recruitment kama taasisi nyingine za serikali. Ajira zao hufanyika kwa njia za siri, na wengi wa maafisa wao huajiriwa kupitia vetting ya ndani, bila nafasi kutangazwa wazi. Mara nyingi, wanachukua watu kutoka taasisi za usalama kama Polisi (hasa CID), JWTZ, Immigration, na TRA, au wale waliomaliza vyuo vikuu katika fani kama sheria, IT (cyber security), uchumi, na uhasibu. Pia, baadhi ya watu hupatikana kwa mapendekezo kutoka kwa maafisa wa juu wa serikali.

Hutumia undercover recruitment, ambapo wanaweza kuajiri watu walioko kwenye sekta binafsi, mashirika ya kimataifa, au hata mitaani ikiwa mtu ana access ya taarifa muhimu. Kabla ya kuajiriwa, mtu anapitia uchunguzi mkali wa maisha yake (vetting), kuanzia historia ya familia, connections zake, tabia binafsi, na hata mawasiliano yake na watu wa nje ya nchi. Wanaopitishwa hupelekwa kwenye mafunzo ya siri ya ujasusi kabla ya kupewa majukumu rasmi. Hii si kazi ya kutuma CV. Ukihitajia,unaitwa.
 
Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS, ni wababaishajitu na watafuta sifa. Mtumishi mwaminifu wa imani ya TISS hajulikani na wala hutakuja hata kumhisi abadani.
Hakika
 
Wale uliodhani ni watumishi wa TISS sio watumishi wa TISS, ni wababaishajitu na watafuta sifa. Mtumishi mwaminifu wa imani ya TISS hajulikani na wala hutakuja hata kumhisi abadani.
Wewe TISS unawajua?? Mbona mimi ni TISS.s lakini sijisemi....
 
UNDER COVER ANAWEKWA KIPENGELE GANI HAPA MKUU?
 
Ikitokea wanamfuatilia mtu ambae hana elimu kubwa huwa wanaangalia nini.
 
Wanajikuta ndio wazalendo kuliko raia yoyote hapa tz
 
Wakati wa mwalimu ilikuwa TISS kweli kweli. Utakuta mpiga rangi viatu kumbe ni TISS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…