Wale wenye biashara za familia, hii ndio njia sahihi ya kulinda mali dhidi ya watoto wenye tamaa na majambazi wataoingia kwa njia ya ndoa

Wale wenye biashara za familia, hii ndio njia sahihi ya kulinda mali dhidi ya watoto wenye tamaa na majambazi wataoingia kwa njia ya ndoa

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Huwa inatokea mmiliki wa biasahara hasa baba anapotangulia mbele ya haki haya hutokea,
  • Mke hujimilikisha mali zote na pengine yeye kahusika kwenye kifo kwa tamaa ya mali
  • kuna mtoto hasa wa kwanza hupenda kujimilikisha biashara yote akiamini ni haki yake
  • Wengine wanaolewa au kuoa majambazi wanaotolea macho mali za biashara kwa lengo la kujimilikisha aidha kwa kuua au kuvunja ndoa.
  • Kuna ndugu vichomi wanasubiria siku ufe waje kunyanganya mali zako kwa kisingizio cha "mali za kaka ./ dada"
Kama una biashra ya familia ni vema kutengeneza kampuni au group, mfano biashara yako inaitwa Kasongo basi kaisajili iwe Kasongo Company au Kasongo Group.

Kwenye Bodi ya wenye kampuni wanachama inabidi wawe wanafamilia pekee, umemaliza mchezo.

Yani ni kwamba hata wazazi wasipokuwepo, Kampuni inaendelea kuwa ya watoto waliobaki

Ikitokea kaka wameshindwana na mke wake au mke wake kaamua kummaliza, hana haki ya kujimilikisha mali za kampuni au group, kufanya kinyume na hapo ni tiketi halali ya kumshughulikia kisheria kama mwizi

Maamuzi ya mali za kampuni / group inabidi yafanyike kwa pamoja, mfano kwenda kuchukua mkopo wa benki inabidi kila mwanafamilia apewe taarifa na aridhie kwa kusaini, ikitokea kaona mkopo hauna tija ana haki ya kuukataa.
 
Akiolewa na vijana wapiga deki umeisha labda wasiwe Hawa wamama wa mijini.

Huhitaji kuwa na mali iliyoandikwa kwa Jina lako. Weka kila kitu kinamilikiwa na kampuni. Na watu wanakwepa milolongo ya Kodi kwa Namna hii.

Vijana wengi ni wajinga Sana.
Wanafikiri Mama zao sio wanawake.

Alafu Muda huohuo wakiwa wamejisahau utawasikia wakiimba "mishangazi×3" kumbe mishangazi ni mama wa vijana wengine.
Au sio ajabu mama Zao kuna vijana wamawaita mshangazi
 
Hii ndio njia pekee ya kutunza utajiri na mali for generations has kwa sisi ngozi nyeusi ambapo mtu akifa naa vitu vyake vyote hupotea
 
Back
Top Bottom