Walimu Laki Mbili kugombea Nafasi elfu Kumi na Moja. Wanaotakiwa Oral interview NI elfu arobaini na nne

Dooo
 
NILITEGEMEA MPWAYUNGU NDO ALETE TAKWIMU HIZI.
 
Hata wakichujwa bado ufanyaji kazi serikalini ni wa mazoea tutarudi palepale
waweke mishahara ya kueleweka hata wakichuja ni yale yale TRA hakuna mafisadi, wazembe, Je wizarani... ukitaka kumkamua ngombe maziwa mlishe, na nikifanikiwa class naingia kwa wiki mara 3 siku zingine nipombe na mitkasi nyingine.
 
Halafu utakuta kwenye hizo nafasi elfu 11 zinazogombaniwa, nusu yake tayari zina vijana watakaopata hiyo kazi kupitia connection mbalimbali. Nchi ngumu sana hii.
 
Mkuu andika yote ila interview sio ombi, ipo pale pale.
Nawew kweli! kwahyo tuseme wote wamefeli ndo kada ya ualimu itafutwa?? Mtu kafanya pepa tokea vidudu sembesa maswali 50 ya kuchagua tena hakun passmark wenyew tu wanahtaji watu 3/4 waende oral ndo umtishe mtu???? point yangu ni kuwa cha kwanza kukifanya ni kuboresha masirahi ya walimu.
 
Hapo mkoa wa Kagera utoe kabisa kwenye hiyo orodha yako. Pia toa Njombe. Hivi unajua mkoa wa wala senene na Wilaya zake kwa upande wa ualimu na afya unagombewa kama maeneo ya majiji? Usiulize kwa nini bali subiri wafike kwenye usaili. Hiyo orodha yako ungeweka Manyara na Kilimanjaro toa Njombe na Kagera. Kingine matokeo ni jumuishi nchi nzima kama ulivyoona upande wa afya (assumption). Vipi kuhusu pass mark itakayochukuliwa kwa eneo husika?
 
Mkoa wa kimkakati akuna mana majibu ya written interview, watayaunganisha ya nchi nzima then watakata kwenye pass mark wanayoona kuwa watakuwa wamepata idadi kadhaa ya watakaoenda nao oral.
pasi na kujari mkoa Fulani wamepita wengi mkoa fulan wachache hizi sio ajira za afisa utendaji mitaa Kila halmashauri na matokeo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…