Walimu Mei mosi imekaribia, andaeni mabango ya maandamano ya Amani

Walimu ni watu muhimu mno ila walimu wa sasa mmetengenezwa kwa misingi ya hofu na kutokujiamin , kuna karia haina pesa kama ya mwalimu ila tu kujiamni tu kunawafanya wasionekane mbayuwayu , unaweza ukafika shuleni tu upo smart na kausafiri kako walimu wakatimua mbiyo kama wanafunzi wakahisi ni mkaguzi , hii karia ni muhimu mno inahitajika wazazi na serikali tuwatie moyo na sio kuwavunja ,hawa ni walezi wa taifa la kesho .
 
Ndonyie wachawi, haters of progress
 
Walimu Wana pesa, shida Ina baki Kwa mtumiaji wa huo mshahara

Wapo wengi kuliko watumishi wengine ndiyo maana inakuwa rahisi kuwa pinpoint kuliko watumishi wengine, mathalani afisa maendeleo wa Kata

Hapo nikukuuliza nitajie afisa maendeleo wa Kata Yako najua itakuwa shida kumjua Kwa haraka tofauti na nikisema unitajie mwalimu yeyote unayemfahamu hapo mtaani kwako

Mbona walimu waliofanikiwa hamuwataji,nchi hii imetoa karibu walimu wawili kuwa Marais mbona ilo hamlisemi!?
 
Utajiri ni namna unavyoamua kutumia pesa. Wapo walimu matajiri sana wana hadi kampuni zao zao kwa hiyo kila kundi lazima kuna rank hata uliko wewe siyo wote mna hela.
Hata wakulima, maaskari, wanasheria hawapo sawa.
 
Maisha magumu hata wasion walimu wanayo

NI mantiki Gani unayotumia kuona Hali ngumu Kwa mwalimu ni kitu Cha ajabu kuliko nesi au polisi akiwa na maisha magumu!?
Mkuu kuna uzi nilishaleta humu nikielezea kazi za hovyo kwenye nchi hii.
Mwalimu, polisi, askari magereza... hawa ndio tatu bora na ukumbuke hapa tunawaongelea waajiliwa na maisha yao..
Ukisema maisha magumu yapo kwa kila mtu unatoka nje ya point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…