Yaani ukiwa msomi alienda shule ukaandika vitu ambavyo hujawahi hata kuvifanyia uchunguzi angalau kidogo inakuwa inatia aibu. Ngoja niwaeleze kama mnataka kujua vizuri.
Mtaala wa elimu shule za msingi kwa mtu aliemaliza kidato cha nne akapata four ya 28 na kushuka chini,akaenda chuo miaka miwili anakuwa na sifa toshelezi kabisaaa za kufikisha kile kilicho lengwa kwa mwanafunzi. Darasa la kwanza ni KKK ,mwenye uwezo wa kufundisha vizuri watoto wakajua kusoma vizuri na kuandika vizuri ni wale waliova vizuri kimbinu chuoni ndio wenye uwezo wa kuwafundisha watoto vizuri.
Huku mashuleni walimu wenye shahada za ualimu wanashindwa kufundisha vizuri kwa sababu mbinu na njia nzuri za kufundisha hawazijui wao walifundishwa kwa ujumla.Wanafunzi wanaleta kero zao wanasema mwalim hawamuelewi lakini ukiangalia ni kweli kabisaa.
Kumaliza fofm six na kusoma shahada sio tiketi nzuri ya kuwa mwalm mzuri hasa kwa mtaala wa elimu ya msingi Tanzania. Tanzania shida iliyopo walimu hawafundishi wanafunzi kwa vitendo bali ni kuwakaririsha kitu ambacho ndoo kinauwa uwezo wa wanafunzi kwenye mashule yetu. Ukitaza maudhui yaliyomo ni ya kawaida sana kueleweka kwa mwanafunzi shida ni namna anavyofundishwa mtoto hasa walimu wengi wamekataa tamaa,hawajiandai kuingia kufundisha ,hawatumii zana za ufundishaji lakini pia watoto hawapelekwi field kufanyia kazi walivyo viona kwenye vitabu. Serikali ibadilile iwrke ufuatiliaji wa karibu sana na kuhakikisha angalau 50% wanafunzi wafundishwe kwa vitendo.