Walimu wa Tanzania ndio maana wanadharauliwa na kila mtu

Mkuu weka namba mwisho wa mwezi wanapata kiasi gani zaidi ya hapo walimu
Askari Magereza anayeanza kazi na elimu ya form4 analipwa:
Msha ha ra= 516,000 basic
Posho ya chakula 300,000
Posho vinywaji 100000
Mazingira magumu 86,000
Pango la nyumba 86000
Ujuzi 86,000 kama anao
Umeme na maji bure punde wanaanza kulipwa keshi.

Bima bure
 
Askari magereza WA nchi ipi?

Wangepewa pesa yote hii wasingekaa nyumba zile za mabati keko
 
Huyu anashinda na wafungwa ambao Mahakama zetu zinaamini ni Criminal (sijawahukumu mimi).


Turudi kwa ndugu walimu wanaoshinda na watoto wetu ambao tunaamini ndo Taifa letu la kesho....


B1 = Basic 419,000

Cwt = 8,390.
Pension = 20,950.
Income = 46,090.
Insur = 12,570
Take home = 331,000

Hana nyumba, hana chakula, hana usafiri na mahitaji mengine ya kibinadamu. Anaishi Tuwangoma na anafanya kazi Temeke


MPAKA HAPO TUNA TAIFA LA KESHO??


Watanzania tuwe serious
 
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]Hapa kazi tu
 
Mimi nawakubali walimu kwa mishahara hiyo hiyo ila anaishi smart kuzidi wa f1,we na f1 yako life hovyo bg up maticha wote tz wananidhamu ya kazi
 
Bila walimu ungepata elimu? au umeamua kujitoa fahamu tu hapa.....ulivyoanza la kwanza ulikuwa hujui chochote, kusoma, kuandika, kuhesabu mbona hukufundishwa na wazazi wako nyumbani? Au ukishavuka mto basi ni ruksa kumtukana mamba.​
 
Askari magereza WA nchi ipi?

Wangepewa pesa yote hii wasingekaa nyumba zile za mabati keko
Kwa taarifa yako hakuna wafanyakazi wa chini nchii wanaolipwa posho nyingi kama JWTZ Uhamiaji Magereza, Zima Moto, Polisi!!
Posho ya chakula kwa wale wa magamba magamba ni 380K bila kujali cheo.

House allowance ndo zinatofautiana kwa vyeo
Vinywaji ni 100k wooote.

Posho ya ujuzi kwa wenye ujuzi, mfano unakuta mwanajeshi ana degree ya ualimu na hajawai ingia darasani analipwa posho ya ualimu (nonsense)

Unakuta Askari magera kosomea Computer Science hawezi kushusha operating system au yuko Gereza la Kitengure hawana kompyuta analipwa posho ya ujuzi[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]


Afu wakija watetezi wa walimu wanataka kutuua!!

Kama nchi swala la Elimu yetu inabidi tulifanye liwe mjadala wa KITAIFA. WATOTO WA MACCM NA MACHADEMA wanasoma Cambridge Syllabus. Sisi wetu wanafundishwa kufundishwa kuuza kashata na andazi za mwalimu wa darasa.

Wanalima mashamba ya walimu wa zamu na kuchota maji ya kuwapikia walimu uji kwani chai inahitaji sukari na bei ya sukari imechangamka.
 
Bila walimu ungepata elimu? au umeamua kujitoa fahamu tu hapa.....ulivyoanza la kwanza ulikuwa hujui chochote, kusoma, kuandika, kuhesabu mbona hukufundishwa na wazazi wako nyumbani? Au ukishavuka mto basi ni ruksa kumtukana mamba.​
Soma vizuri na uelewe au acha kujitoa ufahamu!! Huu mjadala hauwadharau au kuwadhihaki walimu. Tunajadili masilahi yao. Huyo ulom quote ni mwalimu anakili maslahi yao ni mabovu!! Sasa wewe unatoka huko ushalambishwa asali unakuja kutufokea??
 
Tusiwaangushe moyo walimu wetu jaman ipo siku watu watataman kukimbilia ualimu tuiachie serikali itawaboreshea tu miaka haifanani
 
Hizi ni siasa

Mishahara ya walimu uliifafanua vyema kulingana na nama serkali inalipa,

Tupe mchanganuo kulingana na TGS
 
Labda kama hujasoma uzi wangu, umekurupuka baada ya kusoma Tittle.
Binafsi nimetumia jamiiforums.com kama reference! Kwenye jukwaa hili kuna nyuzi nyingi (idadi yake inatia shaka ) ambazo zinazungumzia walimu wetu negatively!! Kuna mpaka member wengi wamejizolea umaarufu kwenye jukwaa hili kwa kuanzisha nyuzi za walimu.

Mimi kama mtanzania mzalendo nikasukumwa kujua chanzo na sababu ya walimu wetu kubezwa.

Nisome mwanzo mwa uzi huu
 
Jamii forums kila member ana mshahara mkubwa/kipato kikubwa kasoro walimu.
Cha kushangaza ukija katika uhalisia huku mtaani walimu ndiyo wanakimbiza kwa kipato ukiondoa wakuu wa taasisi.
Huku kijijini nilipo walimu ndiyo wamewekeza kuliko kada yoyote
Hapa tunazungumza swala la kitaifa sio la kijiji chenu!! Mwenyewe na ishi kijijini na kipato changu ni cha kawaida lakini hapo kabla au wakata wa dharura za hapa na pale naenda kwenye miji na majiji. Niambie ukweli unamlipaje mwalimu wa jiji mshahara mdogo kuliko boom mwanafunzi wa chuo anayeishi hostel na kula cafeteria??

Hivi tuko serious na ELIMU YETU??
 
Sawa , ebu. tuone mwisho wenu utakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…