Walimu wa Tanzania ndio maana wanadharauliwa na kila mtu

Walimu wa Tanzania ndio maana wanadharauliwa na kila mtu

Huu ujinga (sina nendo mbadala) ndo mnauotumia kuwadanganyia walimu (alianza Rais Mkapa kwa kufuta Teaching allowance) eti kada flani wanalipwa kiasi kidogo kuliko nyinyi!!

Twende sawa
Tuseme Askari anayeanza kazi analipwa mshahara wa Tsh 400,000/= baada ya makato anabaki na 360,000 let say,

Baada ya hapo katikati ya mwezi anapewa laki 3 isiyo na makato kama posho, laki 1 ya vinywaji na anakaa line police. Utamfananisha na mwalimu sijui C hapo juu??

Njoo na hesabu sio siasa.

#Hatuwakejeli walimu, wananyonywa
Kada nyingi zilizochini ya tamisemi zilifutiwa posho na kuongezewa mshahara.
Hapo mwanzo walikuwa wanapewa mshahara mdogo (basic) kuliko huo pamoja na posho. Ikaja kuonekana kuwa kwenye Mafao wanapata kidogo sana. Ikabidi posho ziunganishwe na mshahara kuibust basic salary ili kukipandisha kiinua mgongo.

N.B
Wanasiasa pamoja na watunga sera huwa wanadai kada yenye wafanyakazi wengi zaidi ni waalimu hivyo ukiwaongezea kidogo tu bajeti inshoot high, hivyo ni rahisi kuongeza kwenye kada yenye watu wachache mf wabunge, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa idara n.k kuliko kuongeza kwenye kada yenye watu wengi
 
Askari Magereza anayeanza kazi na elimu ya form4 analipwa:
Msha ha ra= 516,000 basic
Posho ya chakula 300,000
Posho vinywaji 100000
Mazingira magumu 86,000
Pango la nyumba 86000
Ujuzi 86,000 kama anao
Umeme na maji bure punde wanaanza kulipwa keshi.

Bima bure
Marekebisho kidogo
Ni kweli posho ya chakula (ration) ni 300k lakini huwa inamegwa 50% inabaki kikosini kwa ajili ya chakula wanachokula wakiwa kazini/kikosini. Ule usile huwa inakatwa
Hivyo inayoingia kwenye account huwa ni 150k

Pia posho ya vinywaji haitolewi kila mwezi bali inatolewa kwa mzunguko kwa kupokezana mfano mwezi wa 1 jwtz wakipewa polisi hawawezi kupewa. Nadhani inachukua miezi 3 ama 4 mzunguko kumrudia muhusika
 
Mkuu, ukiwa na ajira katika sekta ya elimu, ukiwa na mzazi au mlezi, mume au mke, ukiwa na ndugu wa karibu, rafiki ama jamaa wa karibu ambaye ni mwalimu, huwezi kabisa kutumia lugha ngumu na isiyokuwa na staha kama uliyoitumia juu yao.

Hii ni mojawapo ya ajira nyeti mno hapa nchini. Akili na elimu yako yote imechakatwa kupitia mikono yao. Huwezi kupita katika daraja, kisha ukaanza kuridharau kutokana aina ya muundo wake.

Kumbuka ipo karma ambayo itakuandama katika maisha yako yote hapa duniani kwa kukosa utu na shukurani. Hata kama kuna baadhi ya walimu wamekukwaza kwa namna moja ama nyingine, haiewzi kuwa ni sababu ya wewe kuhalalisha kuwabagaza walimu wote nchini Tanzania.
Nikweli kabisa Yani, jamaa angeleta mada mhimu jinsi gani tujadiliane kuikwamua kada hii kutokana na unyonyaji unaoendelea.
 
Baada ya kuona kila leo kuna mijadala ya kuwadharau walimu ikanibidi niingie Google kujua walimu wanalipwa kiasi gani. Nilichokikuta huko ni aibu!!

Yaaani kwa mwezi mwalimu analipwa posho ya mbunge ya kikao kimoja?

Yaani serikali inaona poa kumlipa allowances askari magereza anayeshinda na wafungwa lakini mwalimu asubiri uchafuzi wa SISIEMU?

HII NI MISHAHARA YA WALIMU 2022/2023!!

B1 = Basic 419,000

Cwt = 8,390.
Pension = 20,950.
Income = 46,090.
Insur = 12,570
Take home = 331,000

C1 = Basic 530,000
Cwt = 10,600.
Pension = 26,500.
Income = 58,300.
Insurance = 15,900
Take home = 418,700

D1= Basic 716,000

Cwt = 14,320.
Pension = 35,800.
Income = 78,760.
Insurance = 21,400
Take home = 565,640

E1 = Basic 940,000

Cwt = 18,800.
Pension = 47,000.
Income = 103,400.
Insurance = 28,200
Take home = 742,600

F1 = Basic 1,235,000

Cwt = 24,700.
Pension = 61,750.
Income = 135,850.
Insurance = 37,050
Take home = 975,650

Source
Hayo makato ya CWT ndio yanawaumiza walimu skku zote. Hiki chama kimekosa muelekeo lakini ndicho kimekuwa chanzo kikuu cha kuminya uchumi wa mwalimu.
 
Ukikuta mtu anamkashifu Mwalimu mchunguze vizuri na huenda anakotokea ni ukoo wa mazwazwa. Kumfharau Mwalimu ni kiwango Cha mwisho Cha upumbavu. Kupeleka watoto Kenya hakuna ulichosaidia labda uhamie kanisa huko maana Kila nchi Ina utamaduni wake.
 
Umedanganywa hizo ni za kipindi cha Magufuli ila kwa mama Samia zinatofauti kidogo
Samia si aliwaongezea elfu 20?

Kisha gharama za tozo na gharama nyingine za maisha zikapanda kwa 200%
 
Ukikuta mtu anamkashifu Mwalimu mchunguze vizuri na huenda anakotokea ni ukoo wa mazwazwa. Kumfharau Mwalimu ni kiwango Cha mwisho Cha upumbavu. Kupeleka watoto Kenya hakuna ulichosaidia labda uhamie kanisa huko maana Kila nchi Ina utamaduni wake.
Ninyi mavuvuzela wa ccm au serikali ndiyo mnaowadharau walimu, mleta mada yeye hajawadharau bali amerejea mada nyingi humu jf zilizokuwa zikiwadharau.

Tukiachana na hilo, mleta mada ameweka chanzo cha dharau hizo, nilidhani ni vizuri kujikita kwenye chanzo kama mleta mada alivyodhamiria kinyume chake unakimbia mada halisi.

Ni kweli kuwa serikali inawadharau walimu wala hili halina ubishi, Je wewe hapoa ulipo ungelipwa sh 300000 na familia yako ungeweza kuishi?
 
Nchi ilikuwa na marais wawili tu. Nyerere na Magu. Kwisha. Huwez ukaona nchi inawanyonyaji ndani humohumo. Umekalia kitu unashindwa kimutumia kichwa. Mwinyi alidanganywa akaondoa, kikwete hakuifikiria kabisa aliangalia tu. Ninawahakikishia ukiona mungu hajakuchukua mapema, ujue anakupa muda wa kurekebisha. Only nyerere and magufuri. Otherwise tunakaa kimya kusubiri atokee. Mengine kuhusu kutumika wkt wa uchaguz hayo ni matokeo kuwaingiza watoto wa ndg zao waliofeli kufundisha ndio wawatumiao hao kwenye kazi zao.

Tena siku hizi benki zimeamua kujichotea nafasi. Kilichofutwa na mwingi, benk wanakifanya kwa jina la benk advance.

Kuna walimu wa nguvu waliofaulu enzi hizo wapo darasani mchana baada ya kazi, kwenye biashara. Wanafanya kazi na biashara. Hawana njaa zinazoongelewa hapa.

Waliamua kukaa kimya
 
Mimi ni mwanachi Wa kawaida Ila nimeamua kutoa maoni kwa lengo la kuijenga fikra Chanya juu ya mtazamo Wa heshima na dharau. Kuhusu taaluma ya MTU au watu .

Sasa wewe uwasilishaji wako Wa hoja umejaa kejeri ,dharau na kutweza utu Wa MTU.

Unabidi kubalidilika ili kuwa a complete human being
Kwahiyo Dr umeamua kuwa Racist kama Botha??

Kwamba I'm looking like human being?? Dah!!

Kwahiyo Dr hapo wewe umenisifia au??
 
Walimu sio watu wa kutetea, ni mara100 kutetea hata yule Mamba kule Rukwa, Walimu ni kundi limejaa wapumbavu, Wajinga, waoga, binafisi watoto wangu nimewapeleka Kusoma Kenya, kule wanajifunza ujasiri, Huku Tanzania wangefundishwa uoga na hawa walimu wetu, Pole yao ambao watoto wao wanafundishwa na aina hii ya walimu na kikubwa wanacho fanya wana transfer ujinga ule kwenda kwa watoto
hongera Kwa Kuwapeleka Watoto Wako Kusoma Kenya Ila Walimu Wa Tanzania Ndo Wamekufanya Leo Ugundue Kuwa Tanzania Ina Elimu Duni
 
Acheni kutetea ujinga, hata kama mleta mada pengine ana nia tofauti, ukweli uko wazi kuwa mishahara ya walimu ni midogo sana ukilinganisha na kada zingine

Wapo wengi humu wanaokubaliana na ukweli huu lakini wanadai kuwa, "eti"

Mishahara ya walimu ni midogo kwa kuwa wao hawana nyongeza ya ziada isiyo mishahara kama vile house, night allowances.

Kwa sababu hiyohiyo ya utetezi wao, hata hii ni sababu kuu ya kuwadharau. Kwa nini kada zingine zipewe hizo allowances na walimu wanyimwe huku wakikabiliwa na maisha magumu yaliyo ktk mazingira ya kada zingine.

Hapa mi sioni kuwa amewadharau bali ni ukweli mtupu. Hao mnao tetea mko kupalilia nafasi zenu serikalini na wala hamjui machungu anayopitia mwalimu.

Ktk hoja hii hakuna mwl anayeweza kupaza sauti ya kumbeza mleta mada maana yeye anjua uhalisia
Mimi sijawahi kukashifu achilia mbali mtu yoyote kwa hii jukwa ndo maana tangu nijiunge JF sijawahi kupigwa ban. Kichwa cha uzi kinasadifu yanayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali ya Jf lakini Uzi unaelezea lengo langu.

Mkuu nisome tena
 
Mwisho wa nini ndugu? Mbona unamtisha?
Uzi wake uko clear na ni ukweli mtupu.

Wewe kama unausoma kwa mtazamo hasi ni ajabu sana kwako unayejiita DR hata kama ni mtetezi wa serikali.

Ni aibu kwa mwl kupokea sh 300000 akaweza kufanya kazi huku akibanwa kila kona.

Usitishe watu som coments za wachangiaji unaweza faida.
Dr anakemea wachangiaji eti wanawadhihaki walimu, wakati huo huo yeye anawadhihaki wachangiaji zaidi.

Nyani haoni ngedere
 
Mkuu, ukiwa na ajira katika sekta ya elimu, ukiwa na mzazi au mlezi, mume au mke, ukiwa na ndugu wa karibu, rafiki ama jamaa wa karibu ambaye ni mwalimu, huwezi kabisa kutumia lugha ngumu na isiyokuwa na staha kama uliyoitumia juu yao.

Hii ni mojawapo ya ajira nyeti mno hapa nchini. Akili na elimu yako yote imechakatwa kupitia mikono yao. Huwezi kupita katika daraja, kisha ukaanza kuridharau kutokana aina ya muundo wake.

Kumbuka ipo karma ambayo itakuandama katika maisha yako yote hapa duniani kwa kukosa utu na shukurani. Hata kama kuna baadhi ya walimu wamekukwaza kwa namna moja ama nyingine, haiewzi kuwa ni sababu ya wewe kuhalalisha kuwabagaza walimu wote nchini Tanzania.
Mr/s Mbege nioneshe lugha ngumu niliyotumia kwa walimu. Lugha yangu ngumu ni kwa Serikali na wale wanaowabeza na kuwadhiaki walimu hasa hasa hapa jamiiforums. Nisome tena

Labda kama utakua utakua mgeni hapa JamiiForums lakini kila wakati inaletwa thread ya kuwadharau walimu na kuna kipindi JamiiForums walikua wanafuta threads zinazowathiaki walimu mpaka wachangiaji wakalalamika.

Sijawathiaki WALIMU, SISI KAMA JAMII YA GREAT THINKERS WA JAMIIFORUMS TUNAWEZA KUFANYA JAMBO JEMA KWA WALIMU KWA MASILAHI MAPANA YA ELIMU NA TAIFA LETU KWA UJUMLA.

NB Nisome tena
 
Walimu sio watu wa kutetea, ni mara100 kutetea hata yule Mamba kule Rukwa, Walimu ni kundi limejaa wapumbavu, Wajinga, waoga, binafisi watoto wangu nimewapeleka Kusoma Kenya, kule wanajifunza ujasiri, Huku Tanzania wangefundishwa uoga na hawa walimu wetu, Pole yao ambao watoto wao wanafundishwa na aina hii ya walimu na kikubwa wanacho fanya wana transfer ujinga ule kwenda kwa watoto

Kuwa na Adabu Mkuu unapowa address waalimu, ukiachana na kwamba wengine Tumezaliwa na kulelewa na Waalimu, lakini pia wana mchango mkubwa wa kutufukisha wengi wetu hapa tulipo so kuwa na heshima kidogo
 
Kada nyingi zilizochini ya tamisemi zilifutiwa posho na kuongezewa mshahara.
Hapo mwanzo walikuwa wanapewa mshahara mdogo (basic) kuliko huo pamoja na posho. Ikaja kuonekana kuwa kwenye Mafao wanapata kidogo sana. Ikabidi posho ziunganishwe na mshahara kuibust basic salary ili kukipandisha kiinua mgongo.

N.B
Wanasiasa pamoja na watunga sera huwa wanadai kada yenye wafanyakazi wengi zaidi ni waalimu hivyo ukiwaongezea kidogo tu bajeti inshoot high, hivyo ni rahisi kuongeza kwenye kada yenye watu wachache mf wabunge, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa idara n.k kuliko kuongeza kwenye kada yenye watu wengi
Nimesoma hiyo NB yako nimesikitika saana!! Yaani unaweka simenti nyingi kweye kozi za mwisho za matofali wakati foundation umejenga kwa matope ukiogopa gharama??

Mtu mwenye akili timamu (sina maneno mbadala) hawezi kufanya hivi!!

Tanzania tuko na WANAFIKI WENGI KWA SABABU YA ELIMU MBOVU
 
Back
Top Bottom