Walimu wa Tanzania ndio maana wanadharauliwa na kila mtu

Kada nyingi zilizochini ya tamisemi zilifutiwa posho na kuongezewa mshahara.
Hapo mwanzo walikuwa wanapewa mshahara mdogo (basic) kuliko huo pamoja na posho. Ikaja kuonekana kuwa kwenye Mafao wanapata kidogo sana. Ikabidi posho ziunganishwe na mshahara kuibust basic salary ili kukipandisha kiinua mgongo.

N.B
Wanasiasa pamoja na watunga sera huwa wanadai kada yenye wafanyakazi wengi zaidi ni waalimu hivyo ukiwaongezea kidogo tu bajeti inshoot high, hivyo ni rahisi kuongeza kwenye kada yenye watu wachache mf wabunge, mawaziri, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakuu wa idara n.k kuliko kuongeza kwenye kada yenye watu wengi
 
Marekebisho kidogo
Ni kweli posho ya chakula (ration) ni 300k lakini huwa inamegwa 50% inabaki kikosini kwa ajili ya chakula wanachokula wakiwa kazini/kikosini. Ule usile huwa inakatwa
Hivyo inayoingia kwenye account huwa ni 150k

Pia posho ya vinywaji haitolewi kila mwezi bali inatolewa kwa mzunguko kwa kupokezana mfano mwezi wa 1 jwtz wakipewa polisi hawawezi kupewa. Nadhani inachukua miezi 3 ama 4 mzunguko kumrudia muhusika
 
Nikweli kabisa Yani, jamaa angeleta mada mhimu jinsi gani tujadiliane kuikwamua kada hii kutokana na unyonyaji unaoendelea.
 
Hayo makato ya CWT ndio yanawaumiza walimu skku zote. Hiki chama kimekosa muelekeo lakini ndicho kimekuwa chanzo kikuu cha kuminya uchumi wa mwalimu.
 
Ukikuta mtu anamkashifu Mwalimu mchunguze vizuri na huenda anakotokea ni ukoo wa mazwazwa. Kumfharau Mwalimu ni kiwango Cha mwisho Cha upumbavu. Kupeleka watoto Kenya hakuna ulichosaidia labda uhamie kanisa huko maana Kila nchi Ina utamaduni wake.
 
Umedanganywa hizo ni za kipindi cha Magufuli ila kwa mama Samia zinatofauti kidogo
Samia si aliwaongezea elfu 20?

Kisha gharama za tozo na gharama nyingine za maisha zikapanda kwa 200%
 
Ukikuta mtu anamkashifu Mwalimu mchunguze vizuri na huenda anakotokea ni ukoo wa mazwazwa. Kumfharau Mwalimu ni kiwango Cha mwisho Cha upumbavu. Kupeleka watoto Kenya hakuna ulichosaidia labda uhamie kanisa huko maana Kila nchi Ina utamaduni wake.
Ninyi mavuvuzela wa ccm au serikali ndiyo mnaowadharau walimu, mleta mada yeye hajawadharau bali amerejea mada nyingi humu jf zilizokuwa zikiwadharau.

Tukiachana na hilo, mleta mada ameweka chanzo cha dharau hizo, nilidhani ni vizuri kujikita kwenye chanzo kama mleta mada alivyodhamiria kinyume chake unakimbia mada halisi.

Ni kweli kuwa serikali inawadharau walimu wala hili halina ubishi, Je wewe hapoa ulipo ungelipwa sh 300000 na familia yako ungeweza kuishi?
 
Nchi ilikuwa na marais wawili tu. Nyerere na Magu. Kwisha. Huwez ukaona nchi inawanyonyaji ndani humohumo. Umekalia kitu unashindwa kimutumia kichwa. Mwinyi alidanganywa akaondoa, kikwete hakuifikiria kabisa aliangalia tu. Ninawahakikishia ukiona mungu hajakuchukua mapema, ujue anakupa muda wa kurekebisha. Only nyerere and magufuri. Otherwise tunakaa kimya kusubiri atokee. Mengine kuhusu kutumika wkt wa uchaguz hayo ni matokeo kuwaingiza watoto wa ndg zao waliofeli kufundisha ndio wawatumiao hao kwenye kazi zao.

Tena siku hizi benki zimeamua kujichotea nafasi. Kilichofutwa na mwingi, benk wanakifanya kwa jina la benk advance.

Kuna walimu wa nguvu waliofaulu enzi hizo wapo darasani mchana baada ya kazi, kwenye biashara. Wanafanya kazi na biashara. Hawana njaa zinazoongelewa hapa.

Waliamua kukaa kimya
 
Kwahiyo Dr umeamua kuwa Racist kama Botha??


Kwamba I'm looking like human being?? Dah!!

Kwahiyo Dr hapo wewe umenisifia au??
 
hongera Kwa Kuwapeleka Watoto Wako Kusoma Kenya Ila Walimu Wa Tanzania Ndo Wamekufanya Leo Ugundue Kuwa Tanzania Ina Elimu Duni
 
Mimi sijawahi kukashifu achilia mbali mtu yoyote kwa hii jukwa ndo maana tangu nijiunge JF sijawahi kupigwa ban. Kichwa cha uzi kinasadifu yanayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali ya Jf lakini Uzi unaelezea lengo langu.

Mkuu nisome tena
 
Dr anakemea wachangiaji eti wanawadhihaki walimu, wakati huo huo yeye anawadhihaki wachangiaji zaidi.

Nyani haoni ngedere
 
Mr/s Mbege nioneshe lugha ngumu niliyotumia kwa walimu. Lugha yangu ngumu ni kwa Serikali na wale wanaowabeza na kuwadhiaki walimu hasa hasa hapa jamiiforums. Nisome tena

Labda kama utakua utakua mgeni hapa JamiiForums lakini kila wakati inaletwa thread ya kuwadharau walimu na kuna kipindi JamiiForums walikua wanafuta threads zinazowathiaki walimu mpaka wachangiaji wakalalamika.

Sijawathiaki WALIMU, SISI KAMA JAMII YA GREAT THINKERS WA JAMIIFORUMS TUNAWEZA KUFANYA JAMBO JEMA KWA WALIMU KWA MASILAHI MAPANA YA ELIMU NA TAIFA LETU KWA UJUMLA.


NB Nisome tena
 

Kuwa na Adabu Mkuu unapowa address waalimu, ukiachana na kwamba wengine Tumezaliwa na kulelewa na Waalimu, lakini pia wana mchango mkubwa wa kutufukisha wengi wetu hapa tulipo so kuwa na heshima kidogo
 
Nimesoma hiyo NB yako nimesikitika saana!! Yaani unaweka simenti nyingi kweye kozi za mwisho za matofali wakati foundation umejenga kwa matope ukiogopa gharama??

Mtu mwenye akili timamu (sina maneno mbadala) hawezi kufanya hivi!!

Tanzania tuko na WANAFIKI WENGI KWA SABABU YA ELIMU MBOVU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…