Walimuita Baba yangu majina ya ajabu, Freemason, mchawi

Walimuita Baba yangu majina ya ajabu, Freemason, mchawi

Simjui baba yangu kivipi, nilikuwa najua shughuli zake zote na hakuna chonzo chochote cha mapato ambacho kilikuwa na utata au kuhusiana na hayo mambo machafu.
Narudia tena humjui vizuri baba yako hiyo comment yako ni ushahidi tosha unamjua juu juu tu.
 
Habarini ndugu, Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Mzee wangu, nimeamua kushare story hii fupi inayohusu jambo ambalo lilimkuta enzi za uhai wake.

Kama ilivyo kawaida katika jamii zetu, mtu akiwa na mafanikio huitwa majina yote mabaya pasipo kujali uhakika wa madai hayo..

Siku moja ya jumapili, mzee alikuwa nyumbani na kama Kawaida yake jioni hupendelea kutoka na kwenda jirani kidogo na nyumbani kwa lengo la kukutana na kubadilishana mawazo na wadau ( kijiweni).

Baada ya kufika kijiweni, kwa bahati mbaya sendo aliyokuwa amevaa ikakatika na ikabidi ampe fundi viatu kwani hakuwa mbali na pale, alibaki na kiatu kimoja na alikataa kuvaa ndala ambazo alipatiwa na fundi.

Mwisho akaona amuachie fundi viatu vyote viwili ili arekebishe vyote, yeye akabaki peku kwa muda wa zaidi ya nusu saa huku akiwa bado anazunguka huku na kule.

Watu walimuona na kuanzia hapo maneno yakaanza, kwamba mzee amepewa masharti atembee peku, wengine wakaanza kusema ni Freemason.

Baada ya wiki kadhaa kupita, taarifa zikamfikia bimkubwa na akamweleza mzee kwamba mtaani watu wanasema hayo maneno, mzee hakupata wasiwasi na alicheka tu.

Ikafika jumapili nyingine, mzee akaona ngoja achochee moto vizuri kwani alikuwa ni mtu ambaye anapenda kucheza na akili za watu hasa wajinga, basi akaondoka nyumbani bila viatu (peku) akaenda kijiweni na akakaa huko kwa muda mrefu.

Watu walimuona na wakazidi kusema na kuzidi kumshutumu na ulozi, mzee hakujali na alifanya hivyo makusudi. Walikuwa na wasiwasi na mambo yake kwasababu hakuna aliyekuwa anajua mzee anafanya mishe au shughuli gani ambazo zinampa kipato.

Kwa sasa mzee wangu ni marehemu, Mungu amfanyie wepesi huko alipo, alikuwa mtu jasiri asiye yumbishwa na maneno ya walimwengu.

FUNZO: Wakiamua kukukanyaga kwa bahati mbaya na wewe walipue kwa makusudi.
Nilijua unaandika point kumbe utumbo
 
Alikuwa na mkwanja wa kutosha

Biashara kadhaa
Nyumba kadhaa
Pesa katika account kadhaa
MTU wa kutoa Sana na kusadia?


Mzee wako alikuwa MTU wa aina gani?
Alikuwa mfanya biashara, hata hapa mtaani alikuwa na nyumba kadhaa.

Lakini hakupenda kujitenga au kujiskia, alikuwa akikaa na watu wa aina zote na kuwasaidia kwa kile alichokuwa anaweza kusaidia
 
Wewe ndio unajua kuwa ni uongo ila jamii haijui hilo
Uongo ukirudiwa rudiwa watu udhani ni kweli
Hata jamii ikiamini hivyo nini kitabadilika? Maisha yanaendelea na Namuombea mzee apumzike kwa Amani
 
Huenda alikua na matatizo ya akili. Mtu na utimamu wake wa akili atembee peku tena mitaani kulivyo kuchafu??🤔🤔
Hao walikua sahihi kumuita hivyo mi ndo ningesema chizi kabisa
Alifanya hivyo ili kucheza na akili zao hao wajinga, hakuwahi kuwajibu ila hakuogopa kufanya kitu kwa kuhofia kusemwa
 
Siku hizi misukule ni kawaida, wewe jichunge tu wasiondoke na wewe. Zungumza na wazee wa busara wakuweke sawa. Kila atakaejaribu ngoma irudi kwake.
Kweli siku hizi kuna mambo mengi ya ajabu lakini mimi sina tatzo na mtu wala sidhani kama kuna mtu ana nia ya kunidhuru bila sababu
 
Back
Top Bottom