Walimuita Baba yangu majina ya ajabu, Freemason, mchawi

Walimuita Baba yangu majina ya ajabu, Freemason, mchawi

Habarini ndugu, Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Mzee wangu, nimeamua kushare story hii fupi inayohusu jambo ambalo lilimkuta enzi za uhai wake.

Kama ilivyo kawaida katika jamii zetu, mtu akiwa na mafanikio huitwa majina yote mabaya pasipo kujali uhakika wa madai hayo..

Siku moja ya jumapili, mzee alikuwa nyumbani na kama Kawaida yake jioni hupendelea kutoka na kwenda jirani kidogo na nyumbani kwa lengo la kukutana na kubadilishana mawazo na wadau ( kijiweni).

Baada ya kufika kijiweni, kwa bahati mbaya sendo aliyokuwa amevaa ikakatika na ikabidi ampe fundi viatu kwani hakuwa mbali na pale, alibaki na kiatu kimoja na alikataa kuvaa ndala ambazo alipatiwa na fundi.

Mwisho akaona amuachie fundi viatu vyote viwili ili arekebishe vyote, yeye akabaki peku kwa muda wa zaidi ya nusu saa huku akiwa bado anazunguka huku na kule.

Watu walimuona na kuanzia hapo maneno yakaanza, kwamba mzee amepewa masharti atembee peku, wengine wakaanza kusema ni Freemason.

Baada ya wiki kadhaa kupita, taarifa zikamfikia bimkubwa na akamweleza mzee kwamba mtaani watu wanasema hayo maneno, mzee hakupata wasiwasi na alicheka tu.

Ikafika jumapili nyingine, mzee akaona ngoja achochee moto vizuri kwani alikuwa ni mtu ambaye anapenda kucheza na akili za watu hasa wajinga, basi akaondoka nyumbani bila viatu (peku) akaenda kijiweni na akakaa huko kwa muda mrefu.

Watu walimuona na wakazidi kusema na kuzidi kumshutumu na ulozi, mzee hakujali na alifanya hivyo makusudi. Walikuwa na wasiwasi na mambo yake kwasababu hakuna aliyekuwa anajua mzee anafanya mishe au shughuli gani ambazo zinampa kipato.

Kwa sasa mzee wangu ni marehemu, Mungu amfanyie wepesi huko alipo, alikuwa mtu jasiri asiye yumbishwa na maneno ya walimwengu.

FUNZO: Wakiamua kukukanyaga kwa bahati mbaya na wewe walipue kwa makusudi.

ALIFANYA UTOTO MARA YA PILI KWENDA KIJIWENI PEKU PEKU. HAPO HAKUTUMIA BUSARA. HIYO SASA ILIMSAIDIA NINI ZAIDI YA KUMWONDOLEA HESHIMA? TUKIO LA KWANZA NAMUUNGA MKONO BUT LA PILI ALI BEHAVE KITOTO NA KUTAKA SIFA ZA KIJINGA.
 
Shida inanzia kwanini marehemu alikataa kuvaa ndala za fundi,wakati ni kawaida baadhi yetu kufanya hivyo
Hiyo sio shida ni maamuzi, inawezekana amehisi anaweza kupata fungus kwsbb zile ndala wanavaa watu wengi

Hata mimi huwa sivai
 
ALIFANYA UTOTO MARA YA PILI KWENDA KIJIWENI PEKU PEKU. HAPO HAKUTUMIA BUSARA. HIYO SASA ILIMSAIDIA NINI ZAIDI YA KUMWONDOLEA HESHIMA? TUKIO LA KWANZA NAMUUNGA MKONO BUT LA PILI ALI BEHAVE KITOTO NA KUTAKA SIFA ZA KIJINGA.
Sio kutaka sifa bali ni kuwaonesha kwamba hajali maneno yao hata wakizidi kusema, pia walianza muda tu kumsema kabla hata ya kufanya hivyo.

Mzee hakuwa mtu mnyonge hata kdgo, alijua kucheza na akili za wajinga hasa masikini. Anajua ni wivu umewajaa na alifanya mengi ili kuwapa maneno ya kusema na waendelee na umasikini wao.
 
Wewe humjui vizuri baba yako, watu sio wajinga mafanikio yana kona nyingi bado hujajua vizuri shule ya mtaani
Hamna kitu, Waswahili wana maneno sana na wana muda wa kujudge watu...wangekuwa busy na mambo yao ya huyu Mzee yasingewahusu

Hata ukiwauliza Freemasons ni nini hawawezi kukueleza

Ujinga tu
 
Sio kutaka sifa bali ni kuwaonesha kwamba hajali maneno yao hata wakizidi kusema, pia walianza muda tu kumsema kabla hata ya kufanya hivyo.

Mzee hakuwa mtu mnyonge hata kdgo, alijua kucheza na akili za wajinga hasa masikini. Anajua ni wivu umewajaa na alifanya mengi ili kuwapa maneno ya kusema na waendelee na umasikini wao.

ALIONESHA TU NI MJINGA NA ANATAKA SIFA ZA KIJINGA. WATU WALIZIDI TU MDHARAU NA TABIA ZA KITOTO. HAPO HAKUNA CHA KUONESHA KUWA SI MNYONGE. BWEGE YEYOTE ANAWEZA TEMBEA PEKU PEKU KWANI ANAKATAZWA? HAKUNA UBINGWA HAPO.
 
Atafute sifa kwa watu gani? Watu ambao wameshindwa kutafuta hela na kuishia kupiga majungu?

Hizo sifa zingemsaidia nini? Unajua ni figisu ngapi amewahi kufanyiwa na hao watu mpaka kufikia hatua ya kuwaonesha kwamba hajali na waendelee kusema wasemavyo?
 
SIFA ZA KIJINGA ANAONA FAHARI ETI KUITWA FREEMASON. ULIDHANI UNAMSIFIA BABA YAKO KUMBE UNAONESHA HAMNA AKILI.
 
SIFA ZA KIJINGA ANAONA FAHARI ETI KUITWA FREEMASON. ULIDHANI UNAMSIFIA BABA YAKO KUMBE UNAONESHA HAMNA AKILI.
Hukuna la maana unalo lisema zaidi ya chuki kwa watu usio wajua, kuita watu Freemason ni hulka ya masikini ambao hawajui hata kesho watakula nini.

Napata mashaka hata wewe ni mojawapo ya masikini...
 
Hukuna la maana unalo lisema zaidi ya chuki kwa watu usio wajua, kuita watu Freemason ni hulka ya masikini ambao hawajui hata kesho watakula nini.

Napata mashaka hata wewe ni mojawapo ya masikini...
Maskini baba yako anayetembea pekupeku akidhani anawatisha watu. Mmekutana wote hamna akili. Wewe ulidhani ni ushujaa kumbe upumbavu. Anaona sifa kuonekana ni freemason kijijini
 
Maskini baba yako anayetembea pekupeku akidhani anawatisha watu. Mmekutana wote hamna akili. Wewe ulidhani ni ushujaa kumbe upumbavu. Anaona sifa kuonekana ni freemason kijijini
Huna jipya zaidi ya chuki kwa watu usio wajua....

Napata mashaka hata wewe ni mmojawapo wa masikini....
 
WEWE NA MZEE WAKO WOTE NI MABWEGE MNA UJINGA MWINGI MNADHANI FREEMASON NDO UTAJIRI.
Huna jipya ndugu, hujui hata watu unao waita Mabwege wana uwezo kiasi gani, laiti ungejua ndyo ungezidi kuporomosha matusi zaidi.
 
Mimi uswaz kwetu vijana walikuwa wanajua mimi mjeda huku nikiwa sijui, sasa nilikuwa nabadilisha TV, hiyo niliyokuwa naitoa niliwaambia mafundi wanitafutie mteja, wakaja na mteja, wakanitambulisha huyu ndiyo mnunuzi mjeda mwenzio yupo kambi flani!...ha ha.
Ahaaaa
 
Na wewe katembee pekupeku kama mzee wako na upuuzi wa kutaka sifa za kijinga
Huna jipya ndugu, napata mashaka na wewe ndyo walewale maskini wenye wivu na kupata makasiriko kuona wengine wanaishi vizuri.
 
Back
Top Bottom