Walio karibu na Makonda wamwambie ni kosa kubwa kuwa maarufu kuliko Rais. Aache kabisa harakati

Anachofanya Makonda ni sahihi ndizo siasa zinazohitajika kwa mazingira ya sasa ya kisiasa, akina Sofia na waenezi wengine walishindwa na CCM ilikuwa inaenda shimoni kijana amefufua ari hususani kwa watu wa chini kanda ya ziwa na kwingineko.
 
Yuko kwenye kukijenga chama. Viongozi wake wanatambua hilo, na wanamakubaliano hayo.
Hakuna kiongozi yoyote duniani anayeweza kuruhusu hilo kaka. Hakuna. Anatakiwa kueneza yale yaliyoagizwa. Mfano akafafanue manufaa ya Mkataba wa bandari na Dubai. Huo ndio uenezi. Achukue lawama zote juu ya chama na Sifa zote ziende kwa mwenyekiti.

Angesoma historia ya Oscar Kambona angeelewa.
 
Of course ni sahihi ila kama Rais kaamua kujificha mgongoni kwake acha iwe hivyo.

Niliwaza kwamba ukiacha kwamba ni kosa kuwa Maarufu kuliko Rais pia ni hatari kwake kwenye msitakabari wa siasa yake Kwa sababu watu dizaini yake Huwa hawadumu ajifunze kwenye historia na Kwa yule anaemuita Role model wake.
 
Unauelewa mpana sana ndugu yangu,mwenye macho 2 hawezi kuuekewa huu mchezo, Mwenezi hafanyi hayo kwa bahati mbaya,
 
Anachofanya Makonda ni sahihi ndizo siasa zinazohitajika kwa mazingira ya sasa ya kisiasa, akina Sofia na waenezi wengine walishindwa na CCM ilikuwa inaenda shimoni kijana amefufua ari hususani kwa watu wa chini kanda ya ziwa na kwingineko.
Ni sahihi lakini ataje jina la Rais kadiri inavyowezekana na asema kabisa kwamba Rais kamtuma vinginevyo Kwa maigizo yake mara Bajaj,mara baiskeli anaweza pata hata Ajali ya mchongo akapotea.

Hii ni Dunia acheze Kwa akili walikuwepo kina Sokoine,Omar Juma,Karume, Mwendazake nk nk.
 
Ajitahidi kutaja jina la Rais kadiri inavyowezeka walikuwepo kina Sokoine kabla yake,mwambieni ukweli kumsaidia.
 
Inaweza kuwa Mpango maalum au Mpango usio ratibiwa, vyovyote ilivyo hili suala haliwafurashi Mawaziri, hasa ambao walitakiwa watatue kero badala yake Mwenezi anatenda kuingilia Kati.
 
Inaweza kuwa Mpango maalum au Mpango usio ratibiwa, vyovyote ilivyo hili suala haliwafurashi Mawaziri, hasa ambao walitakiwa watatue kero badala yake Mwenezi anatenda kuingilia Kati.
Bora lisiwafurahishe Mawaziri ila likamfurahisha Rais.

Mawaziri ni watu wadogo wanaweza fukuzwa wakati wowote na wakadhibitiwa na mfumo wakileta chokochoko but yeye kikubwa aheshimu ana mamlaka ya Rais , Waziri Mkuu.

But amejitahidi kusaidia chama Kwa sababu pia yeye ni binadamu ambapo Kila binadamu ana hulka zake,mtu kama Kamkonda ni mtu wa msimamo mkali.
 
Hata kwenye Roman Catholic Huwa ni hivyo. Padre hapaswi kutoa mahubiri ya kuvutia sana kumzidi askofu wake ni kosa na anaweza kuhamishwa parokia na kupelekwa kufundisha seminari kubwa au ndogo. Wanaofundisha seminarini mara nyingi ni adhabu
 
Mara tu alipoteuliwa mlisema hataweza. Leo ashakuwa maarufu zaidi ya Rais. Ahahahahaha!!!!
 
Kama eneo lako la kazi wewe ni kiongozi subordinate wako watakuwa wanakuombea mabaya kila kukicha!
Upo na akili ya ujima sana,
 
Una hoja,Usipuuzwe!
 
Hata kwenye Roman Catholic Huwa ni hivyo. Padre hapaswi kutoa mahubiri ya kuvutia sana kumzidi askofu wake ni kosa na anaweza kuhamishwa parokia na kupelekwa kufundisha seminari kubwa au ndogo. Wanaofundisha seminarini mara nyingi ni adhabu
Ahahahah..Bas na mimi nimegundua emzi zile kwann kanisani pastor alikua hanipi nafas ya kuhubir madhabahuni ila wemgine wanapewa but mimi ni ioe mara moja moja sana hali ikiwa tete na ya dharura ndio napewa pasi nitikise nyavu, na Mungu alikuaga anasimama sana upande wangu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

NB.
Nishaachana na mambo hizo siku hizi
 
Mkuu,umesahau kumtaja Augustino Mrema,alipata umaarufu kuliko Boss wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…