Walio karibu na Makonda wamwambie ni kosa kubwa kuwa maarufu kuliko Rais. Aache kabisa harakati

Makonda ni maarufu? Tuanzie hapo, maarufu ni mtu mmoja tu nchi hii, na mtu huyo ni Rais wa JMT ambaye kwa sasa ni Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan.

“Never outshine the Master/Boss” this is the greatest law of Power…!!
 
Tulia wewe

Lengo la Makonda ni kuwafanya wapinzani waache kujadili mambo ya maana

Na wamjadili yeye tu
 
Samia alianza kwa upole, kwa kuwaacha huru, lakini kizazi hiki kilivyo cha hovyo kutokujielewa wamemuona samia hajitambui, wakanza kumtukana nk.nk.
Sasa kaona alipokosea na kama angebadilika na kuanza kuwapelekesha mngemshangaa.
Hivyo ameona yeye kama mama ameona sio vuzuri kugombana na watoto wake.hivyo kaamua kuwaletea kijana wake mtukutu awakumbushe kua uwezo wa kufikiri anao na vijana wa kumulinda anao.
Hii iwe ndani ya chama, au kwenye serikali.
 
Ufafanuzi murua
 
Thumbs up
 
Tena ni Aloe Vera bomba sana
 
Hii ni ishara yakwamba kuna mmoja amepwaya kwenye nafasi yake..hoja sio makondo aache anacholifanya..ni hivi huyo mama ache kunyanyasa wamasai na aplay part yake.
 
The First Law katika 48 Laws of Power kitabu kilichoandikwa na Robert Greene inseama;

NEVER OUTSHINE THE MASTER.

In your quest to impress the people above you, don't flaunt your talents too much. If your superiors feel insecure, they'll find ways to replace you. Even if you're currently in favor, don't take it for granted as you can easily fall out of favor with the wrong moves
 
Umaarufu uwe wa kweli na sio kusanifu, ni umaarufu wa chama na sio mtu. Mwisho umaarufu unaenda kwa mwenye kiti. Kuna kosa gani?

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Watu hamjui siasa kwa ustawi wa taifa na protokali huwezi kuagiza
Makonda ni maarufu? Tuanzie hapo, maarufu ni mtu mmoja tu nchi hii, na mtu huyo ni Rais wa JMT ambaye kwa sasa ni Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan.

“Never outshine the Master/Boss” this is the greatest law of Power
Mikutano anayofanya, Wafuasi anaotengeneza na Aina ya siasa anayoifanya naona kama kuna mpango mbadala. Sababu haongei, hasemi na hafanyi kama aliyemtuma.

Hii inamtengenezea jina. Ila likitaka kuwa kubwa kuliko raisi au kuwa sawa na rahisi hiyo ni kitu kingine kabisa. Ndio maana CCM kwa kujua hilo mamlaka yote kapewa Malkia. Na malkia kwenye kundi la nyuki huwa ni moja tu
 
Tulia wewe

Lengo la Makonda ni kuwafanya wapinzani waache kujadili mambo ya maana

Na wamjadili yeye tu
Upeo finyu sana wa kufikiri.
Watu wakianza kumsikiliza yeye na kumuelewa yeye kuliko ata mama maana yake watataka agombee uraisi.
Amekuwa na mamlaka ya kuagiza na hata kuhoji mawaziri hadharani. Hii sio siasa. Tunamkumbuusha tena Sokoine aliogopwa kila alipopita kuliko ata nyerere. Aliagiza, kamata na kushugulika na kila aina ya uovu.
Na alipoondoka hakuna waziri mkuu tena aliyekuja kuwa na umaarufu zaidi ya Rowasa na Mrema waziri. Na wote sasa umaarufu uliwaponza
 
Hizo ni hofu zenu nyie

Wanaccm hatuna shida naye
 
Nilikuwaga hatasijui mwenezi ana kazi gani?? Kuingia Bashite tu watu wamejua makali ya mwenezi 😂🙌🙌
 
Wazungu wanasema, "never outshine your master".
 
Kumsaidia raisi ni kufafanua hoja za bandari, kufafanua mambo Ambayo Raisi kafanya kama kujenga madarasa, Miradi inayoendelea kutekelezwa na serikali. Kuwaponda wapinzani na kutoa kasoro zao. Kufafanua uzuri wa kikokotoo cha wastafu kwa taifa.. Faida za Hamkosi na Maslahi ya watu wanayoshugulikiwa na serikali ila kamwe. Narudia kamwe
1. Asihoji au kuagiza chochote kwenye mkutano wa hadhara.
2. Asikubali kabisa kupokea kero ya watu hadharani na kuzijibu moja kwa moja. Majibu yawe ntafikisha kwa Raisi ili lipatiwe ufumbuzi.

Dunia nzima hakuna taasisi yenye wivu kama uraisi.
Sudan kusini Raisi na Waziri mkuu walikuwa na ushawishi sawa ikagawanyika. Kongo kinshasa makamanda karibu 20 walikuwa na ushawishi sawa.

Ethiopia pia viongozi wa majimbo walikuwa na ushawishi mkubwa kwenye majimbo yao kuliko waziri mkuu wakamgeuka waziri vita vikaanza.

Siku makonda akikengeuka akiwa maarufu basi kazi ipo. Yasije ya Mrema na Mwinyi.
 
Sio Africa tu bali dunia nzima. Yesu alipozaliwa tu. Nyota yake ilipoonekana tu HERODE alimsaka amuue na wazazi wakamtoreshea Misri. Kwanini? Unakuwaje maarufu kuliko mfalme sasa.
 
Mim nafuatilia sana toka ziara zianze nadhan bando zamgu zimeenda sana. Naona ni watu wanafunga barabara mfano hapo nyegez walifunga barabara. Sasa hapo mwenez ana kosa gan?
 
Sasa ukweli ni upi kwa sababu wapo wanadai Kambona aliondoka nchini kwa kutokukubaliana na sera ya ujamaa na kujitegemea - yaani baada ya kutangazwa Azimio la Arusha mwaka 1967. Mgomo wa wanajeshi uliotokea 1964 au vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…