Waliochapwa na DC Arusha na kulazimishwa kulipa fedha bila kufikishwa mahakamani waombe msaada wa kisheria kumshtaki DC

Waliochapwa na DC Arusha na kulazimishwa kulipa fedha bila kufikishwa mahakamani waombe msaada wa kisheria kumshtaki DC

Unajua mwizi wa madawati anafanana na yule mwizi anayehujumu reli barabara wote hawa ni wahujumu uchumi wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi ambayo sheria ndio inastahili iwe hivyo.
Ukishawachapa viboko maana yake ushatoa ashabu mzee ilibdi mapema angewapeleka mahakamani mzee

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Sisi tulisoma enzi zetu, tena tulitunza madarasa, mabweni, maktaba na hata kusafisha bwalo na vyoo...
Sasa wa siku hizi LAZIMA WAIBE AU KUCHOMA MOTO?! Halafu watu wanadai wapewe haki?!
Ndorobo kabisa, wafanyiwe kazi kama wale waliochoma kituo cha polisi labda wanafunzi watapata adabu...
 
Mkuu muulize tu taarifa kazitoa wapi atupe majibu,akishindwa kujibu achana naye. Unamuuliza kwa kejeli yeye ni nani akikutafuta Akijitambulisha halafu akawa ni jitu la kutisha kuliko wewe utajificha wapi? Usisahau tupo kwenye fake id na yawezakuwa Humu hadi mzee baba yupo na saa zingine anamponda aliyemteua maana hakumuagiza atende aliyotenda.
Itakuwa katumwa huyu mkuu,sio buree
 
Wewe ndiye DC mchapa watu? mbona unatoa povu? Udc tu unachapa bakora wenzio, ukipata kile cheo si utawapiga risasi!!!
Yani wewe inaonesha wazi kabsa ni miongoni mwa wale waliochapwa na dc,pole sana mkuu..vp maumivu bado au zimeshapoa??😂😂😂
 
Serikali ijayo itapata tabu sana kulipa fidia ya wahanga wa utawala huu wa mkoloni mweusi
Huyu dogo Kenani ni mjinga sana amebahatika kupata teuzi akiwa kijana badala ya kutengeneza CV yeye analeta uongozi misifa .
 
Kama wameiba walipe tu,,hawa ndio wanakataga taa za barabarani kupata chuma chakavu,,huo ni uhujumu uchumi pure and simple,,walipe tu
 
Unajua mwizi wa madawati anafanana na yule mwizi anayehujumu reli barabara wote hawa ni wahujumu uchumi wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi ambayo sheria ndio inastahili iwe hivyo.
Naunga mkono hoja
 
Watu Kama hawa Bwn.DC wanakipa tabu Sana Chama kuomba kura kwa wananchi kipindi cha Uchaguzi.

You can imagine unamchapa mtu halafu huyo huyo unategemea kwenda kumuomba kura 2025.

Hizi ni hujuma kwa Chama na Serikali.

Mamlaka za uteuzi zikemee mambo kama haya.
 
Pole, Ili 'kushinda', wenzio wanahitaji WAIBA KURA na sio wapiga kura
 
Mahakama zilipokubali kuagizwa na wanasiasa wenye viburi vya madaraka kuweka watu ndani, na kuwanyima dhamana hata kama wanastahili, dharau dhidi ya mahakama nilijua lazima ziwepo. Leo hii wananchi hatuna imani na mahakama, na wakati huohuo waliozifanya mahakama zisiaminike, nao wanazidharau!
Watanzania kwao bado Uhuru,Haki na Utu wa binadamu ni msamiati mgumu.Eti ukiwapa maendeleo mengine yote wanasamehe hata kura zikiibwa inakuwa sawa kwao ilimradi anayeiba kura anawaletea maendeleo.
Haya maajabu yanapatikana hapa Tanzania pekee na dunia inatakiwa kuna kutalii kuona sisi ni binadamu wa aina gani ambao tumeuza Utu wetu kwa ajili ya lami,reli,mabwawa ya umeme,majengo au madaraja!
Watawala wa sasa wamejipa madaraka/vyeo karibu vinavyokaribiana na shetani halisi.
 
Hii siasa ya sasa wanacopy toka China, ndio maana sasa kila mfano wa maendeleo ya nchi hii, mifano yake inakuwa ni China.
 
who are you by the way??
Kwahiyo baada ya jana kukiri wamepita kwako wakakuambia kuwa wanaenda kushtaki?? Hizo akili mnazitoa wapi kwa mfano?? Inamaana hapo ufipa mmekuwa Duni kiasi hiki??
Wewe ndiye mwehu kabisa hili suala siyo la kisiasa bali ni la kisheria. Ni haki mwenye mamlaka kujichukulia sheria mkononi??
 
Pole, Ili 'kushinda', wenzio wanahitaji WAIBA KURA na sio wapiga kura
Ndiyo mkakati na Sera mpya inayowafanya watawala watuone Wananchi/wapiga kura mabwege tu.Wanaobahatika kuingia kwenye uongozi kihalali ni asilimia chini ya kumi,zaidi ya asilimia tisini ni magumashi kuanzia kutia nia,mchakato wa kura za maoni,kuteua wagombea,kura feki na matokeo feki.
Bila Katiba Mpya ya Wananchi ambayo itasimamiwa na Wananchi,Taifa hili limeangamia mazima.Jukumu la kupigania Katiba Mpya ni la Watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa.Tuwajibike!
 
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.

Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.

Uongozi huo ulienda mbali zaidi nakushinikiza kuwafungulia kesi zisizo na dhamana ikiwemo uhujumu uchumi wakiambiwa wamehujumu Mali ya umma na wasipotii nakulipa watawekwa ndani bila dhamana kwa kipindi kisichojulikana. Baada ya vitisho hivyo ambavyo hata vyombo vya habari vimehoji nakujiridhisha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hakuna chombo kiliripoti ukubwa wa kadhia hii badala yake vyombo vyote vya habari vimesimama na DC na kumfanya DC aonekane kuwa yupo sahihi.

Rai inayotolewa na familia za wahanga nikupata uwakilishi wa kisheria waweze kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria ya kile ambacho wametendewa ikiwa Ni pamoja na kuangalia njia yakupata fidia kwa madhara waliyopata.

Ikumbukwe hata watumwa baada Uhuru kwenye baadhi ya Mataifa walikuja kufungua kesi na mahakama za Dunia wakatoa maamuzi lengo likiwa nikuheshimu utu na haki za binadamu.

Kwa upande wa pili, mkuu wa wilaya kutamka adharani kuwa mchakato wa kisheria dhidi ya watuhumiwa ni kupoteza muda inaleta tafsiri kwamba serikali haiamini Kama muhimili wa mahakama una heshima yake. Kitendo Cha mahakama wakati wote kudharaulika wakakaa kimya nacho kinatia ukakasi.

Niwaombe watu wa haki za binadamu waache kukaa ofisini na kutuletea taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu waingie kwenye vyombo vya kisheria nakuwatetea wanaoumia, atutaki takwimu za uvunjifu wa haki tunataka kusikia wamefungua kesi ngapi kutetea wananchi wanaoumizwa na ngapi wameshinda, fidia kiasi gani nk
Tano zaidi tafadhali.
 
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.

Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.
Si unajua kuna mhimili umejichimbia zaidi huko chini mkuu. Siku hizi inategemea kama kesi ina usiasa ndani yake
 
Wewe ndiye mwehu kabisa hili suala siyo la kisiasa bali ni la kisheria. Ni haki mwenye mamlaka kujichukulia sheria mkononi??
Wanufaika mara zote wao niwaimba mapambio ilimradi wapate kile wanachotafuta use halali ama haramu.
 
Back
Top Bottom