Waliochapwa na DC Arusha na kulazimishwa kulipa fedha bila kufikishwa mahakamani waombe msaada wa kisheria kumshtaki DC

Watu Kama hawa Bwn.DC wanakipa tabu Sana Chama kuomba kura kwa wananchi kipindi cha Uchaguzi.

You can imagine unamchapa mtu halafu huyo huyo unategemea kwenda kumuomba kura 2025.

Hizi ni hujuma kwa Chama na Serikali.

Mamlaka za uteuzi zikemee mambo kama haya.
Mamlaka mpaka sahivi kimya ukiona hivyo mtumishi basi ameungwa mkono

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Ni miaka karibia mitano sasa viongozi wamekuwa wakijichukulia sheria mikononi na hakuna kiongozi wa kisiasa wa juu anayekemea Jambo linaloashiria wahusika wanatekeleza msimamo wa serikali.

Wahanga wa tukio la Arusha wamelazimishwa kupigwa na kisha kulipishwa fedha zaidi ya milioni tano ambazo taarifa zinadai wamelazimishwa kuuza baadhi ya Mali zao pamoja na ndugu kuwachangia kutokana na vitisho na shinikizo lililotolewa na uongozi wa wilaya dhidi yao.

Uongozi huo ulienda mbali zaidi nakushinikiza kuwafungulia kesi zisizo na dhamana ikiwemo uhujumu uchumi wakiambiwa wamehujumu Mali ya umma na wasipotii nakulipa watawekwa ndani bila dhamana kwa kipindi kisichojulikana. Baada ya vitisho hivyo ambavyo hata vyombo vya habari vimehoji nakujiridhisha kuwepo kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hakuna chombo kiliripoti ukubwa wa kadhia hii badala yake vyombo vyote vya habari vimesimama na DC na kumfanya DC aonekane kuwa yupo sahihi.

Rai inayotolewa na familia za wahanga nikupata uwakilishi wa kisheria waweze kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria ya kile ambacho wametendewa ikiwa Ni pamoja na kuangalia njia yakupata fidia kwa madhara waliyopata.

Ikumbukwe hata watumwa baada Uhuru kwenye baadhi ya Mataifa walikuja kufungua kesi na mahakama za Dunia wakatoa maamuzi lengo likiwa nikuheshimu utu na haki za binadamu.

Kwa upande wa pili, mkuu wa wilaya kutamka adharani kuwa mchakato wa kisheria dhidi ya watuhumiwa ni kupoteza muda inaleta tafsiri kwamba serikali haiamini Kama muhimili wa mahakama una heshima yake. Kitendo Cha mahakama wakati wote kudharaulika wakakaa kimya nacho kinatia ukakasi.

Niwaombe watu wa haki za binadamu waache kukaa ofisini na kutuletea taarifa za uvunjifu wa haki za binadamu waingie kwenye vyombo vya kisheria nakuwatetea wanaoumia, atutaki takwimu za uvunjifu wa haki tunataka kusikia wamefungua kesi ngapi kutetea wananchi wanaoumizwa na ngapi wameshinda, fidia kiasi gani nk
Wewe wadanganye watingishe kiberiti,
Ni kama wamesamehewa, maana wangefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi!!
Kumbuka hiyo kesi haina dhamana
 
Jeuri,kibri, dharau na vitisho vya ma-DC na ma- RC ni ishara tosha kuwa UTAWALA WA RAIS MAGUFULI NI UDIKTETA KWENDA MBELE......!!!
Baadhi ya Ma-DC na Ma-RC wanajifanya miungu watu kama alivo mteuzi wao!!!
 
Wewe wadanganye watingishe kiberiti,
Ni kama wamesamehewa, maana wangefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi!!
Kumbuka hiyo kesi haina dhamana
Kesi itafunguliwa mahakama ipi,zetu au nyingine?
 
Unawatetea hao wajinga? Wanashiriki kuhujumu uchumi wa nchi yetu kwa kuiba na kuharibu madawati ya shule zetu! Madawati yaliyopatikani kwa nguvu za wananchi. Wadanganye kama hutawasikia wanapigwa miaka 30 kwa kosa la uhujumu uchumi.
Tuondolee upuuzi wako hapa.
Ni sheria gani inayompa DC kuchapa watu Fimbo kwa kuharibu madawati?
Kulingana na Utawala wa sheria DC kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinxi na Usalama alipaswa kuwasiliana na vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo na siyo kuchapa watu fimbo.
 
Kwanza mimi siwezi kuwasaidia chochote hawa , ni mabwege sana ! unakubalije kuchapwa na DC duni kama yule , kwa lipi hasa ?
Mkuu, wasaidie basi waende mahakamani wakajiibulie na kesi ya msingi huko mahakamani ili wafungwe jela kabisa tupunguze wahujumu uchumi mitaani.
Honestly, wamshukuru dc aliyewacharaza viboko akawaacha huru, wakienda mahakamani wakapigwa mvua za kutosha.
 
who are you by the way??
Kwahiyo baada ya jana kukiri wamepita kwako wakakuambia kuwa wanaenda kushtaki?? Hizo akili mnazitoa wapi kwa mfano?? Inamaana hapo ufipa mmekuwa Duni kiasi hiki??
DC amepata wapi mamlaka ya kuchapa watu fimbo? Unaweza kuleta kifungu cha sheria kinachoruhusu hayo!?
 
Unajua wamwkiri katika mazingira gani?Unataka kusema sasa MaDC wageuke mahakimu wanakoongoza?Waendeshe mashtaka na watu wakikiri waadhibiwe!
Hapo hakuna kesi. Wakili au mwanasheria yeyote atakayetia pua yake hapo ataishia kupoteza muda coz lazima kesi ya ngedere itupiliwe mbali tu
 
Acha kutuona wapumbavu wewe mwehu,Jana nimewasikiliza wahusika wote ,wamekiri makosa yao na kutoa faini ya tsh 5000K,halafu unakuja na stori za kwenye kahawa huku..nyambafu kabsa😡😡😵😵😵
Kikiri kosa haina maana wachapwe hadharani mbele ya camera , kuna watu wana kesi za mauaji hata kufinywa tu hawajawahi sembuse hilo

Kama unabariki upumbavu ilio fanywa na huyo mhehe mjinga asiye jielewa basi na wewe ni mpumbavu zaid yake.

Ndio maana kuna mahakama na vyombo vingine vya kushughulika na wahalifu vinginevyo polisi wangekuwa wanaua wahalifu wote wanao wakamata na kesi kama wangekuwa na akili mbovu kama za huyo DC
 
Unajua wamwkiri katika mazingira gani?Unataka kusema sasa MaDC wageuke mahakimu wanakoongoza?Waendeshe mashtaka na watu wakikiri waadhibiwe!

Viongozi wakiendelea hivi basi soon tutapata " Mwamwindi" mwingine
 
Back
Top Bottom