Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Mzee Halima yeye kazawadia nafasi gani ili tuendelee kumshukuru Mungu kwa ajili hiyo?
Wewe endelea kumwita mzee Halima hapo nyuma ya keyboard mwenzio yupo kama alivyo Halima na anachapa kazi.
 
Huku ni kuinajisi Katiba ya nchi yetu waziwazi - hili suala kinakiuka katiba ya nchi kwa asilimia mia - kama hatuwezi hata kuheshimu katiba na sheria zetu je hivi kuna siku tutaweza kujitegemea na hata kuwasaidia weangine?

Kujitegemea kwa maneno mengine ni pamoja na kufuata misingi ya utawala bora kwa asilimia mia - hawa si wabunge halali maana hawatokani na chama cha siasa kama katiba yetu inavyoelekeza - hawa ni wabunge wa CCM wakikumbatiwa na Spika ambaye na yeye pia Ubunge wake una uwalakini mkubwa!
 
Bunge haramu, msitegemee kipya chochote kutoka kwenye hili Bunge haramu. Bora tu Mkoloni angerudi kuliko kuwa na hawa wahuni.
Mhuni kiongozi na wa kwanza ni wewe jomba
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya, ukila nyama ya mtu, utaendelea kula nyama ya mtu!

Tulikuwa wadogo, tukidhani huyu Mwalimu ana maana gani?
Kua uyaone!

Sasa pamoja na heshima yetu yote, Marekani imeitangazia ulimwengu kuwa uchaguzi wetu wa Oktoba 2020 ulikuwa na dalili za kughushi.
Hii si nzuri .
Nyama ya mtu hiyo.

Sasa Ndugai, licha ya malalamiko mengi, kawaingiza CHADEMA-GHUSHI bungeni.
Nyama ya mtu hiyo!

Tunamkumbuka Mwalimu kwa kweli!

Hivi hatuwezi kujisahihisha?
Huu ni msemo mwingine wa Mwalimu!
 
Bado wangali wanakula nyama ya mtu kwa raha mustarehe! Sisi wengine tupo kimya.
 
Ila ruzuku zitokanazo na hawa wabunge Chama kimechukua?

Hebu CHADEMA kuweni na misimamo ili tujue moja.
Tamaa nyingi,anataka hela kutokana na uwakilishi wa wanamama 19,lakini huku amewafukuza uanachama kwa kukiuka taratibu za kuwakilishwa bungeni.

Yawezekana hapa wajanja wanavuta subira ili hasira ya wanachama ipoe harafu wasamehewe kimya kimya.

Chadema na CCM wote wanahusika kwa namna mmoja au nyingine kuwaapisha Covid-19
 
CHADEMA ina Mbunge mmoja aliyeshinda Ubunge ktk Jimbo la Namanyere.Inashangaza kusikia BUNGE limeteua Wabunge kutoka CHADEMA kuongoza KAMATI za Bunge Je hao Wabunge walipataje Ubunge Wao Bila Kupitishwa na Chama Chao?

Na kama ni Wale 19 wa Viti Maalum Mbona CHADEMA ikiwafukuza? Au kuna Chadema Mpya imeanzishwa? Spika hebu heshimu KATIBA ulioapa Kuilinda Acha siasa kwenye masuala ya Sheria kuna Maisha baada ya Uspika. Nchi yetu haina Mbunge pasipo kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa.
 
Chadema ina Mbunge mmoja aliyeshinda Ubunge ktk Jimbo la Namanyere.Inashangaza kusikia BUNGE limeteua Wabunge kutoka CHADEMA kuongoza KAMATI za Bunge Je hao Wabunge walipataje Ubunge Wao Bila Kupitishwa na Chama Chao? Na kama ni Wale 19 wa Viti Maalum Mbona CHADEMA ikiwafukuza? Au kuna Chadema Mpya imeanzishwa? Spika hebu heshimu KATIBA ulioapa Kuilinda Acha siasa kwenye masuala ya Sheria kuna Maisha baada ya Uspika. Nchi yetu haina Mbunge pasipo kuwa Mwanachama wa Chama cha Siasa.
Hayo maswali waulize Kaijage na Mahera pale NEC!
 
Back
Top Bottom