Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Waliofukuzwa CHADEMA waanza kupewa vyeo Bungeni, Grace Tendega awa Mwenyekiti wa LAAC

Hii ndio plan tangu siku wanahatch hiyo plan. Zile kamati ni lazima ziongozwe na wabunge kutoka Upinzani
 
Ila ruzuku zitokanazo na hawa wabunge Chama kimechukua?

Hebu CHADEMA kuweni na misimamo ili tujue moja.
Nani kakuambia Chadema wana shida na ruzuku?? Nani kakuambia zimepokelewa na kupangia kazi?? Au wewe ni Mhasibu wa Chadema?? Siku Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atakapozikagua ndiyo utajua kama ziliguswa au la. Yule aliyeziweka atazikuta pale pale na atazirejesha alikozitoa.
 
Ni swali zuri sana.

Pili, wanaenda Bungeni kwa kutumia chama gani? Kama wanatumia CDM, kuna kila sababu ya kufungua kesi ya kupinga matumizi ya jina lao. Wanaweza kuitwa Wabunge wa Spika , pindi wakiitwa Chadema kuna tatizo

Tatu, hivi hapa hakuna ukikwaji wa katiba? Wako wapi wanasheria au taasisi zinazosimamia mambo haya?
Hivi haiwezekani kufungua kesi

JokaKuu tindo
Jukumu la kuhakikisha sheria za nchi hii zinafuatwa na kuheshimiwa ni la kila mmoja wetu mkuu
 
..hoja zako zinafikirisha.

..tatizo ni kwamba cdm hawakutuma maombi wapewe ruzuku.

..pia hatuna uthibitisho wowote kwamba cdm wametumia fedha za ruzuku.

..mwisho, ccm wamepoke mabilioni ya fedha za ruzuku wakati kuna crisis ya wanafunzi kukosa madawati.

..tunajisifia kununua ndege wakati hatuna madawati, na wanaotuuzia ndege wanafunzi wao wanasoma kwenye madarasa yenye viyoyozi.
CCM wanaweza kujibu kwamba wao wanatoa ruzuku kutimiza matakwa ya katiba hivyo huwezi wakatalia,
Tatizo linakuja pale kwa mpokeaji wa hiyo ruzuku ambaye alisema wazi kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki.
Watu waliouwawa, walitekwa na kura ziliibwa: Kupokea ruzuku iliyotokana na uchaguzi ni kuhalalisha uharamia wa CCM.
 
Nani kakuambia Chadema wana shida na ruzuku?? Nani kakuambia zimepokelewa na kupangia kazi?? Au wewe ni Mhasibu wa Chadema?? Siku Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atakapozikagua ndiyo utajua kama ziliguswa au la. Yule aliyeziweka atazikuta pale pale na atazirejesha alikozitoa.
Kama chama kikuu cha upinzani basi kitoe tamko kwamba hiyo ruzuku imeletwa lakini CHADEMA hatuikubali.
Mbona ni suala rahisi sana kimaadili na kikanuni: Mambo mengine CHADEMA wanatoa tamko na hili pia watoe tamko.
 
Idadi ya kura ktk uchaguzi mkuu uliopita
CHADEMA inasema kwamba uchaguzi haukuwa halali na Mwenyekiti na Makamu walitoa tamko kabisa.
Sasa kwanini Chama kichukue ruzuku zinazotoka na matokeo ya uchaguzi ambao siyo halali ???
 
CCM wanaweza kujibu kwamba wao wanatoa ruzuku kutimiza matakwa ya katiba hivyo huwezi wakatalia,
Tatizo linakuja pale kwa mpokeaji wa hiyo ruzuku ambaye alisema wazi kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki.
Watu waliouwawa, walitekwa na kura ziliibwa: Kupokea ruzuku iliyotokana na uchaguzi ni kuhalalisha uharamia wa CCM.
Una haraka sana !
 
Mbona ni suala rahisi sana kimaadili na kikanuni: Mambo mengine CHADEMA wanatoa tamko na hili pia watoe tamko.
Sio rahisi hivyo. Ndio maana ubunge wa yule mama wa Nkasi unatambulika na ni kama vile umeshapata baraka za chama japo nae alipatikana kwenye process hiyohiyo inayopigiwa kelele
 
Nitaweka pressure kubwa hizo pesa zirudishwe haraka sana. Ukitaka kuwa msafi mbele ya jamii kwa kukataa uchaguzi haramu hivyo hivyo pesa haramu ikataliwe.
Yesu na Maria, ukifaulu kwenye hili tutakupa mji, nani arudishe Fedha! Ndesa iliyomuuza Yesu,haiwezekani?!
 
CCM wanaweza kujibu kwamba wao wanatoa ruzuku kutimiza matakwa ya katiba hivyo huwezi wakatalia,
Tatizo linakuja pale kwa mpokeaji wa hiyo ruzuku ambaye alisema wazi kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki.
Watu waliouwawa, walitekwa na kura ziliibwa: Kupokea ruzuku iliyotokana na uchaguzi ni kuhalalisha uharamia wa CCM.

..Unaposema Cdm wamepokea una maana gani? Je, una taarifa rasmi toka Cdm?
 
Mara nyingi mimi na wewe huwa tukishindanisha hoja na kutopata muafaka husema hivi: Muda ndiyo msema kweli !!

..Kwa kweli hatukustahili kushindana ktk hoja rahisi kama hii.

..Wanaosababisha tufike ktk hali hii ni waandishi uchwara wa habari wa Tz.

..Mara nyingi huandika habari za upande mmoja.

..Tusubiri muda utasema ukweli.
 
Grace Tendega, mmoja wa Wasaliti waliojiteua na kuapishwa na Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum kutoka Chadema, leo ametunukiwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ( LAAC )

Bado haijafahamika kama aliomba nafasi hiyo au amepewa bure.

Bali swali kubwa ni hili , ni yupi mwingine atayekikwaa cheo cha bure miongoni mwa wasaliti waliosalia ?
Iringa nzima hakuna hospitali ya umma yenye CT Scan, Iringa mjini hata za binafsi hazina hiyo kipimo, na kinauzwa kuanzia shilingi milioni 400 tu. Ewe mwenyekiti wa LAAC waambie wakupe hiyo mashine Iringa tupunguze adha ya kusafiri nje ya mkoa kwa ajili ya vipimo tu. Naamini kwa sasa hawawezi kuchomoa ukiwaomba
 
Back
Top Bottom