Hesabu ni somo linalochukiza sana.
Tangu napata ufahamu nikiwa primary nilikua nafeli tu hesabu. Darasa la 4 mpaka la 7 nilikua napata 10% mpaka 20%, yaani 5/50 mpaka 10/50. Inshort primary nilikua mbumbumbu na mwonekano wa kimbumbumbu, mpaka nikawa nafananishwa na kilaza wa darasa, nikawa naitwa kwa jina la huyo kilaza.
Nilivyoanza sekondari nikaanza kujifunza mwenyewe kwenye kitabu bila kufundishwa. Nikawa najifunza mwenyewe kwa muda mrefu, kidato cha pili NECTA nikapata C (49%). Kutoka 10% - 20% mpaka 49% nikaona kumbe inawezekana!, likizo ya form 2 kwenda form 3 nikakazana nikawa najifunza mwenyewe kitabu cha form 3. Midterm ya form 3 nikapata 78% kumzidi aliyeongoza shule nzima kidato cha pili, yeye midterm alipata 77%, nikapata moyo zaidi. Nikamaliza book 3 na book 4 harakaharaka nikiwa form 3, nikiwa form 3 nikaanza kufanya mitihani ya form 4 na wanafunzi wa form 4, nikawa nawakimbiza form 4, grade As zikawa za kumwaga. Form 4 NECTA usiulize, nimetoka na banda la number.