Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Hii imekaa vizuri mkuu. Umesema so vyema kujengea maji ya chumvi. Sisi wakazi wa Dom kwa kiasi kikubwa tuna maji ya chumvi. Unashaurije?
 
Ndio nmejenga na shimo la choo tena kwa tofali zile za round nmenunua moja 1200 na ni included kwenye hyo hyo 10m.

Hongera sana mkuu. Naomba kuuliza, tofali za kulala kabla ya mkanda wa chini ( za msingi zilikua nnchi ngpapi na ziliteketetea ngapi?

Mkanda na linter zote umetumia nondo tatu au nne?

Naona kama umefanikiwa sana kupata vitu bei rahisi.

Ardhi yetu mfinyanzi 10 iliteketea kwenye msingi tu, ikijumuisha kifusi cha kuweka sawa.
 

Tofal za msingi kama 1300 za inch 5, nmetumia nondo tatu tatu juu za 12mm na chini za 10mm kwenye nguzo za barazani ndio nmeweka nondo nne nne!
 
Ni kweli kabisa, mimi pia msingi na rinta pamoja na kifusi tu ilishakatika zaidi ya m7, sijui jamaa ametumia mbinu gani kufika hapo kwa m10? daahh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…