Waliomsindikiza Mwalimu Nyerere safari ya kwanza UNO 1955

Labda kwa vile hakuvaa baibui.
Yeye hamfahamu kama wewe unamfahamu si useme ni nani. Pia si una wazee wako wanaweza mfahamu si uwaulize?

Mnataka kulazimisha kitu ambacho mtu hakielewi?

Mbona kaandika kuwa Daisy kwenye kitabu chake ameandika kuhusu mama Maria Nyerere kuwa alikuwa na duka la mafuta ya taa mtaa wa Livingston na Mchikichi kwani huyo bibi alikuwa akivaa baibui?
 
Kweli familia ya Sykes unaitukuza. Hivi unajua kuwa Nyerere Aliipoanza kazi Tabora nani alimpokea akaa kwake hadi akamuoa Mama Maria nyumbani kwake? Hizi simulizi zako zimeegemea upande mmoja. Tungependa simulizi neutral
Oooooh tuelezeee bwana tuelewe maana wengine hatuna habari kuwa Nyerere alioa alipokuwa Tabora.

Umeona post namba 11? Ina picha na jina la kitabu.

Maana yake nini kiitabu hicho kubeba jina na picha ya Abdul Wahid Sykes?
 
Maalim Faiza,
Hayo usemayo siku zote huwafahamisha kuwa historia ya uhuru imefungamana pakubwa sana na maisha ya wazee wetu.

Kama ninavyowaeleza kuwa ni vigumu sana kudhani inawezekana kuandika historia ya TANU ukaikwepa African Association au Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kwani viongozi wake ni hao hao.

Chuo Cha CCM Kivukoni imejaribu na matokeo yake ndiyo haya nawasomesha upya historia ya TANU na uhuru.

Sasa wanakutana na majina ya wazalendo hawajapata kuyasikia hata siku moja.

Akili zao zimefadhaika na katika mfadhaiko huu wanataabika kuukubali ukweli.

Ndipo Maalim unawaambia kama nanyi mnayo historia mfano wa hii mnaotia shaka ileteni tuisome.
 


= dhahir(i)
 
Hiyo picha ya kwanza juu ,umewataja majina hao wakina mama wengi waliovalia mabaibui lakini umemuacha huyo aliyevaa sketi humjui? Huyo mama ni Lucy Lameck!!!!
Sio kwamba hamjui, mzee huaga ana aleji na Wakristo so kamuacha kwasababu maalumu
 
Sio kwamba hamjui, mzee huaga ana aleji na Wakristo so kamuacha kwasababu maalumu

Katika Watu waliomsaidia sana hayati Mwalimu kwenye harakati zake za kupigania uhuru wa Tanganyika hakuna mtu aliyemzidi marehemu Mzee John Rupia; huyu ndiye aliyekuwa financier mkubwa wa Mwalimu na alikuwa na uwezo kifedha kuliko hao wengine waliokuwa wameajiriwa!! Lakini hapewi prominence na sheikh anayostahili kama wanavyopewa wakina Abdulwahid na Ally!!
 
Mwalimu wako alikuhusia mambo matatu ya hekima na busara sana; endelea kumuenzi kwa kuyazingatia katika maisha yako!!


Qur'an 2:263. Kauli njema na usamehevu ni bora kuliko sadaka inayo fuatiliwa na maudhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha na Mpole.
 
[


Endelea na darasa, kwani ndio kujifunza kwenyewe!! Wengine lafudhi ya kiswahili inatuponza!

Nafahamu, kwani si kila mmoja wetu mwenye kuweza kumudu vizuri lafdhi za Kiswahili hususan wenye lugha mama isiyo Kiswahili na hawajapitia madrasa kupata kufundishwa matamshi ya irabu.
Siku za nyuma niliwahi kuleta mada hapa JF kuhusu hilo, pakawaka moto. Jionee...

Hapa ni darsa ("roughly" kinachofundishwa). "Darasa" ni kile chumba cha kufundishia.
 

Haya mambo ya madrasa yanakuhusu wewe, mimi la muhimu ni kufikisha ujumbe unaoeleweka!
 
Haya mambo ya madrasa yanakuhusu wewe, mimi la muhimu ni kufikisha ujumbe unaoeleweka!
Hakuna tatizo. Madrasa isikutishe ni hiyo hiyo madarasa tu ki sekyula.

Tunausubiri huo ujumbe wako unaoeleweka. Bado sijauona wala sijaona history kutoka upande wako au hujanisoma vizuri juu hapo?
 
Sio kwamba hamjui, mzee huaga ana aleji na Wakristo so kamuacha kwasababu maalumu
Wewe ambae huna "aleji" mbona humtaji?

Au hata hututajii historia japo fupi ya "wakristo" wakati wa kudai Uhuru uijuayo.

Ilete tu hata kama ilikuwa ya upande wa pili wa shillingi. Usiifiche.
 
Hakuna tatizo. Madrasa isikutishe ni hiyo hiyo madarasa tu ki sekyula.

Tunausubiri huo ujumbe wako unaoeleweka. Bado sijauona wala sijaona history kutoka upande wako au hujanisoma vizuri juu hapo?

Nimekusoma vizuri na nimekujibu kuwa hatutakaa kimya pale mnapotaka kutulisha matango pori kuwa nyie peke yenu ndio mlikuwa vinara wa kuleta uhuru wa nchi yetu kwa kupitia imani yenu!! Darasani hawavai vipedo hilo ni vazi la madrasa!!
 
Umetaja jina ukaandika bila ushahidi wowote. Una uhakika mohamed Saidi hajaandikia kuhusu John Rupia?

Kwanini wewe usimpe "kipaumbele" kwa kutuletea ya ziasa kuhusu John Rupia.

Hivi alipataje jina la pesa za kihindi "Rupia" na ilhali nijuavyo ni msukuma?

Leta vitu.
 
Nimekusoma vizuri na nimekujibu kuwa hatutakaa kimya pale mnapotaka kutulisha matango pori kuwa nyie peke yenu ndio mlikuwa vinara wa kuleta uhuru wa nchi yetu kwa kupitia imani yenu!! Darasani hawavai vipedo hilo ni vazi la madrasa!!
Kimya hujakaa nakubaliana na wewe 100% kwa hilo. Lakini hujaleta historia yoyote ile iwe ya wazee wako au ya wazee wa wenzako.

Ndiyo maana nikakueleza kuwa labda walikuwa upande wa wapinga uhuru. Ndivyo? Ndiyo maana unapata kigugumizi cha mikono kuwaandika?

Upingaji wako unaelekea unataka kujuwa usilolijuwa lakini unaona haya kuuliza. Sababu tu, ulikuwepo wakati huo tena una akili sana lakini inaonesha kwa bahati mbaya kabisa hukuwa upande wa "winners". Huna wa karibu yako aliyekuwa kwenye upande wa kudai uhuru? Kama yupo muelezee. Hii ni challenge. Leta hata kama walikuwa upande wa pili wa shillingi, yote ni historia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…