Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

Walioruhusu picha hii itumike hawakuwa wajinga

I hope y'all are doing just fine, It has been long time since I was here[JF Inteligence]
View attachment 2545863
Kuna mtu alileta mada humu akiuliza kwamba picha inayotumiwa na wakristo hasa wakatoliki ya mtu mmoja mzungu kua “ndie” yesu, je hiyo picha ni ya Yesu kweli? Akaongeza kwa kusema kwamba wakati yesu akiwepo kulikua hakuna teknolojia ya Photography wala Motion Picture…So wao waliitoa wapi picha hiyo na wana ushashidi upi kwamba yule ndio Yesu mwenyewe??

I’m glad you asked coz I would like to use this moment to Splendid Explain these stuffs to you!


Toka dunia kuumbwa, dunia imeshuhudia kuzaliwa kwa watu wawili wenye akili zaidi.watu hao walikua wenye uwezo wa kujifunza mambo wao wenyewe yaani Autodidacts na walikua wana uelewa na uwezo wa kufanya mambo meengi kwa wakati mmoja yaani Polymaths…watu hao si wengine bali ni Imhotep kutoka Misri ya zamani (Ancient Egypt) na Leonardo Da’Vinci kutoka Sicily Rome.

Imhotep alikuwepo duniani Zaidi ya miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Da’Vinci, Da’Vinci kazaliwa miaka 600 iliyopita yaani 1400s.Imhotep alikua kuhani mkuu wa mungu mkuu wa wamisri aitwaye mungu jua Ra, mbali na hayo jamaa alikua mbobevu katika hesabu,fizikia na biology hivyo alijikita sana katika usanifu wa majengo na tiba mbalimbali. Ukiziona Pyramids zilizopo misri wala usidanganyike kua alien ndio wamejenga bali ni huyu Inhotep ndio alizisanifu.

Wagiriki walimuabudu huyu mtu kama mungu wao wa tiba kutokana na mchango wake mkubwa katika tafiti zake zi kitabibu.

Kwa waliosoma mada zangu kadhaa zilizopita nilielezea jinsi utawala wa Ugiriki ulivyotokea na kuanguka na matokeo yaliyotokea baada ya ugiriki kuanguka. Kwa ambao hawajasoma nitaelezea kwa ufupi sana nini kilitokea.
Miaka ya nyuma ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo 100 na kila mji na ulikua na utawala wake japo walikua wakiungana na kusaidiana pindi uvamizi unapotokea, enzi hizo superpower wa dunia alikua Persia yaani Iran ya sasa. Iran ilikua inajitanua kwa kuvamia maeneo na kuyachukua hapo ndio alipoikaribia Ugiriki akitaka aanze kuchukua mji baaada ya mji, hapo ndio unakutana kisa cha mfalme Leonidas wa jiji la Sparta.

Vumbi ilitimka kweli kwa wapenzi wa muvi waliotazama muvi ya 300 na 300 Rise of Empire wanaelewa.
Baada ya vamizi kadhaa zilizokua zinafanywa na nchi kubwakubwa wagiriki wakaamua kuungana na kutengeneza nchi moja ya Greece. Mikaka ikaenda akatokea alexander the great akaikuza sana Greek, akaanzisha mji wake ulioitwa Alexandria katika nchi ya Misri. Kipindi hicho misri ilikua ndio hazina na kitovu cha Elimu dunia nzima.
View attachment 2545869
[Mwigizaji Gerald Butler aliyeigiza kama mfalam Leonidas wa sparta kutoka muvi ya ]

Wanafalsafa wengi na walienda hapo kusomea, hata mwandishi wa injili Luka alisomea hapo. Miaka ikaenda baada ya Ugiriki kuanguka Superpower aliyeibuka akawa Rome, Rome ilienda kuchukua kila kitu kilichokua misri wakakihamishia kwao. Maarifa yote yaliyokua Misri kwenye Maktaba ya kwanza kuanzishwa duniani yalihamishiwa Rumi.

Wakati nchi ya Israel ikitawaliwa na Rumi anazaliwa Yesu anafanya kilichomleta duniani kisha anafariki miaka 33 baadae, wafuasi wa Yesu wanaongenzeka na kupata ushawishi mkubwa katika serikali na maeneo mengi duniani.

Kwa wanaopenda Conspiracy, inasemaekana baada ya utawala wa Rumi duniani kuanza kuanguka watu wenye kufikiria mbali (futurist) wakiongozwa na mfalme Nero walikabidhi madaraka kwa wafuasi wa Yesu Kristo wa kipindi hicho ili Rumi iendelee kutawala dunia kupitia mlango wa nyuma (indirectly) ndipo ukristo ukatambuliko rasmi duniani kama Roman Catholic na wakapafanya Rumi kama ndio makao makuu ya Ukristo badala ya Yesrusalemu. (Sina uhakika kama nadharia hii ina ukweli ndani yake ila ina make sense sana maana wote twafahamu nguvu na ushawishi iliyonayo RC katika mataifa mbalimbali)

Miaka kadhaa tawala ya Rumi inaanguka, Ukatoliki ukawa umeenea maeneo mengi na ushawishi mkubwa ulimwenguni anazaliwa Leonardo Da’Vinci 1452, kutokana na uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali kila alichokifanya kiliweza kua Perfecto. Davinci aliweza kuifanya tasnia ya uchoraji kua kubwa na yenye thamani sana kutokana na kazi zake bora na zenye kufikirisha za uchoraji.

Ni moja kat ya wachoraji wakubwa kuwahi ktokea hapa duniani kuna vitu kachora hakuna mwingine anayeweza kuchora labda urumie Powerful software…kama utanibishia jaribu kuchora duara na pembe nne vikiwa pamoja kama alivyochora mchoro wake wa Vitruvian man… Jamaa alikua anaweza kujichora yeye mwenyewe sura yake…Baadae anazaliwa Michelangelo ambae na kwa kiasi Fulani alijitahidi sana katika uchoroja unaweza kujionea michoro yake ya Sistine Chapel iliyopo hapo Vatican, lakini pia nae alibobea katika uchonganji (sculptures)
View attachment 2545902
[Sistine Chapel]
Inahusiana vipi na Picha ya Yesu…?

Kama nilivyoeleza huko juu Baada ya Ugiriki na Misri kuanguka na Rumi kuibuka kama Superpower alibeba maarifa yote yaliyokua Rumi na Ugiriki na kuyahamishia Roma, hivyo baada ya rumi kuanguka kanisa katoliki likabaki limeshikilia maarifa kutoka pande zote za dunia hasa misri,ugiriki na Israel. Leo hii hakuna taarifa au maarifa ambayo hayapo Vatican…Vatican inamiliki moja kati ya eneo lenye kulindwa Zaidi duniani ambalo hua haiingii huko mtu bila ruhusu maalumu…Hata Pope inabidi apate kibali kutoka kwa kiongozi wa Jesuists ndio anaweza kwenda huko.

Hivyo basi sidhani kwamba kanisa katopliki wanaweza kua wameshindwa kupata piacha ya yesu wakati wameweza kumiliki taaroifa za kutoka kila pande ya dunia. Kama Plato,Socrate, nk picha zao zipo na waliishi miaka mingikabla ya yesu haiwezekani yeye picha yake isiweze kupatikana.

Nimesema kipindi hicho taaluma ya uchoraji na uchongaji ilitumika Zaidi katika kuweka kumbukumbu za watu mbalimbali ndio maana leo ukiitaka picha ya Plato unaipata, kuna watu wamejaliwa uwezo mkubwa wa uchoraji unaweza kumuelezea kwamba Fulani sura yake ipo hivi na hivi na akaichora kama ilivyo. Njia hii hutumiwa sana na mashirika ya usalama hususan FBI na polisi. Tena sasa hivi kuna msaada wa softwares yaani ukimuelezea mtu anakutulea mchoro kama picha halisi…hivyo basi natumaini hata picha ya yesu watu wa zamani walitumia njia hiyo kuhifadhi taswira ya Kristo.

Ndio maana utakuta picha hiyo inayotumika sura yake ipo mahali pote sio tofauti. Hata miaka ya 1970s wakati wanaandaa filamu ya yesu walijaribu watu Zaidi ya waigizaji 200 ambao watafanana na Sura hiyohiyo ni Brian Deacon pekee ndio alifanikiwa kufit kwenye role hiyo kutokana na sura yake kufanana na sura inayotumika kuwasilisha taswira ya Kristo.
Ndio maana wasiojua wanapoona hiyo taswira ya yesu hua wanasema kwamba ni sura ya mwigizaji Brian Deacon…Si kweli, kwa maarifa waliyonayo RC hawawezi ruhusu hilo.

So kwa kuhitimisha ni kwamba Wakatoliki kukubali kuruhusu picha hiyo ya Yesu kutumika sio wajinga hata kidogo kwamba hawafahamu taswira halisi ya Kristo.
Na sisi wa Tongereni pia tunae yesu wetu! alipogundua tunamvizia ili tumtoe uhai na afufuke siku ya tatu akakimbilia polisi! daaadeki hatutaki maskhara sie[emoji3][emoji3]
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa, Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Umeongea mengi ila hapa umekosea pakubwa sana kuhusu usabato,
1-Sisi tuna amini katika utatu mtakatifu, na katika mafundisho yanayo define kanisa letu, utatu ni fundisho la pili. na linasapotiwa na mafundisho mengine matatu.
2-Tuna amini katika kifo cha kristo na marejeo yake ya mara ya pili, refer maana ya neno 'ADVENT'. ambalo ndio limejenga Adventist.
3-Kuhusu fumbo la imani sijui una maanisha nini labda ufafanue.
NB: wewe unachanganya Judaism na Usabato.
 
Ameweka kitabu hapo juu. Mathayo 26:48

Kwamba askari walikua hawamjui Yesu, ilibidi Yuda ambusu ndio wamtambue!


Leta hoja zako tuone Chief!
Nina maswali mawili
1.Yuda alilipwa Pesa ya kumsaliti Yesu na askari au makuhani??

2.Askari walimkamata Yesu kwa amri Yao au au ya Warumi au kwa amri ya makuhani??

Baada ya hayo maswali nitakuletea maneno ya yule askari aliemshuhudia Yesu akikata roho na mazingira yaliofuatia kifo Cha BWANA YESU KRISTO pale msalabani e.g Giza,, earthquake nk ili ujiridhishe kwamba askari walikuwa wanamjua au walikuwa hawamjui!!
 
Nina maswali mawili
1.Yuda alilipwa Pesa ya kumsaliti Yesu na askari au makuhani??

2.Askari walimkamata Yesu kwa amri Yao au au ya Warumi au kwa amri ya makuhani??

Baada ya hayo maswali nitakuletea maneno ya yule askari aliemshuhudia Yesu akikata roho na mazingira yaliofuatia kifo Cha BWANA YESU KRISTO pale msalabani e.g Giza,, earthquake nk ili ujiridhishe kwamba askari walikuwa wanamjua au walikuwa hawamjui!!
Kwenye hoja ya umaarufu wa Yesu, niko neutral. Sina upande wowote, nasoma hoja zenu.

Hebu jibu hiyo hoja ili nijifunze badala ya kuniuliza maswali.
 
Simfahamu Faizafoxy, ila fahamu fika kwamba ukweli hauna dini, kabila na haujali hisia zako.
You can put this in a pipe and smoke it.
Wadini wadini wengi ji wale wa elimu ahera, eti wako duniani ila elimu ya dunia hawaitaki wanataka ya ahera😂😂😂😂😂😂😂😂
Wameahidiwa makira sijui 72, aisee
 
Kwenye hoja ya umaarufu wa Yesu, niko neutral. Sina upande wowote, nasoma hoja zenu.

Hebu jibu hiyo hoja ili nijifunze badala ya kuniuliza maswali.
Nikianza na kitabu Cha matayo nitaanzia Matayo 26:3-5 wazee wa watu na wakuu wa makuhani wakipanga mpango,,ktk mstari wa 5 wakajiridhisha ''Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia ktk watu.'''

Kwamba jambo lao walitaka Liwe la low profile kwa sababu walijua implication ya huo mpango.Kama wangekuwa wanataka kumwua mtu asie maarufu wasingepanga wakati sahihi wa kumwua Yesu KRISTO.

Jambo la pili walioenda kumkamata Yesu sio askari walikuwa wahuni waliotumwa na wazee wa makuhani.

Nitaendelea........
 
Ukimsoma Matayo 26:47 waliokuwa na mapanga na marungu wakiwa wametumwa na wakuu wa makuhani walikuwa sio askari yaani wakati Yuda akimsaliti Yesu hakufanya hivyo kwa askari ila watu wahuni waliokuwa wanamfuata Yuda sio kwa kuwa hawakumjua Yesu ila kwa kuwa lilikuwa tukio lililofanyika usiku porini ilibidi mtu wa kuwaongoza Hadi sehemu ya tukio na kuwaongoza mpaka mlengwa alipokuwa.

Kuhusu askari tunamwona
Matayo 27:54 kitu Cha ajabu kuhusu huyu askari ni maneno yake,,,""Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu"""
Kwamba huyu akida sio TU kwamba alikuwa anamjua YESU Bali pia alikuwa anamfahamu.
Ukiona mtu anasema YESU ni Mwana wa Mungu basi jua anamjua kiundani.
 
Ethiopia
Misri

Hizi nchi zina historia kubwa sana juu ya imani zilivyopindishwa hapa Duniani.

Waafrika turudi kwenye asili yetu.
 
Ushabiki ukizidi unakuwa uzuzu.

Mimi ni Mkristo lakini napenda Facts
Wewe sio mkristo nenda uislam unakufanania sana,,huna zaidi ya chuki iliyojificha dhidi ya Yesu KRISTO na sijui shida ni nini.Kazi Yako ni kutwist Ukweli ili uendane na chuki Yako lakini katika Hilo mapema ulishafeli kama kina dada Vinci na vitabu vyake vya kipumbaf ambavyo mauzo yake yalishadorora hasa kutokana na tabia yake chafu ya kuwa mshumaa.
 
Umeongea mengi ila hapa umekosea pakubwa sana kuhusu usabato,
1-Sisi tuna amini katika utatu mtakatifu, na katika mafundisho yanayo define kanisa letu, utatu ni fundisho la pili. na linasapotiwa na mafundisho mengine matatu.
2-Tuna amini katika kifo cha kristo na marejeo yake ya mara ya pili, refer maana ya neno 'ADVENT'. ambalo ndio limejenga Adventist.
3-Kuhusu fumbo la imani sijui una maanisha nini labda ufafanue.
NB: wewe unachanganya Judaism na Usabato.
Je mnamuamini mtume Paul?
 
Kuna kitu kinaitwa Sanda la torino imebeba vitu VINGI sana ni kama negative ya picha ya MTU lakini ina umri mkubwa sana ili fanyika mbinu nyingi za kuteketeza ikashindikana
Hii kitu ipo kiimani ni ngumu zaidi kuaminika kwa wanaopenda kutumia facts
 
Labda angejadiliwa Imhotep ningeridhika zaidi,,da Vinci tabia yake ya ushoga ilimfanya credibility yake kuwa tarnished maana anaweza kuwa pia alikuwa na kichaa,, na watu wengi wachonga vinyago wanasema hizo taswira wanazochonga Huwa wanazipata kwa zenyewe kuwajia ndotoni.Kwa hio hizo picha za da Vinci atakuwa pia aliletewa ndotoni na Pengine hao viumbe waliomletea ndio watakuwa ndio walioanza kumpakua....

NB..Tumeshauriwa tusinunue vinyago na kuviweka ndani,,,,nadhani pia ni hatari kwa mtu asie na uhusiano na Siri za dada Vinci kuweka mapicha yake ndani fate yake haikuwa nzuri.
Hua sikubaliani kwamba D alikua shoga. Sema alikua hajihusishi sana na mapenzi kama ilivyo kwa watu wenye maakili mingi
 
Na sisi wa Tongereni pia tunae yesu wetu! alipogundua tunamvizia ili tumtoe uhai na afufuke siku ya tatu akakimbilia polisi! daaadeki hatutaki maskhara sie[emoji3][emoji3]
Yehova wanyonyi kutoka kisii 😂
 
picha hiyo ya Yesu
Sawaa kuhusu umbo la kichwa , kuna uwalakini kwenye nywele na macho ya huyo mtu.
Wayahudi wana nywele nyeusi tii kama waarabu sasa mbona yeye na nywele za blonde.
Wayahudi macho yao yana uris nyeusi tii, mbona yeye ana blue eye, watu wenye blue eye huwa ni wazungu.

Mwanadamu always yupo biased can't help it,

Na Wakatoliki ndio imani inayojua vyema sana juu ya mapungufu ya mwanadamu, kila siku kila sala lazima waombe kusamehewa, wanakiri ni wadhambi, tuka wapo tumboni, HII DUNIA wanadamu tumefichwa mambo mengi sana.
 
Nashindwa kuelewa mnapo sema Yesu hakuwa maarufu. Vitu vipo very clear, inahitaji very simple logic kulink the dot na kupata a clear picture ya umaarufu wake.

Advancement of Technology
Lazima muelewe kwamba tunaongelea miaka 2000 A.D iliyopita ambapo maendeleo ya teknolojia yalikuwa madogo lakini bado still haikuzuia umaarufu wake. Leo hii katika karne ya 21th century tunaona mapinduzi makubwa ya sayansi na teknolojia, dunia ipo kiganjani. Jambo linasambaa duniani kote with in a minute or with in a single digit, maajabu ya World Wide Web inavyofanya kazi yake.

1. Kwa mantiki iyo kwa nini Mwamposa asijulikane mpaka uso wake?
2. Kwa mantiki iyo kwa nini Kuhani Mussa asijulikane mpaka na kanisa lake?

Huku vitu kama radio now days unaweza ukatune online listening or offline listening kwa nini asijulikane mpaka na vocal sound yake?

Leo hii tukimfufua mtu aliyeishi miaka 2000 A.D iliyopita akakukuta unawasiliana na simu, wewe upo Mwanza muda huo huo unawasiliana na mtu yupo Mbeya immediately wewe ungeitwa mchawi namba moja. Lakini this day's ni jambo la kawaida mtu yupo Bongo anawasiliana na mtu yupo Nevada - Marekani through telecommunications hakuna anayeshangaa wala kushtuka.
That is power of Technology my dear.

Imagination is more powerful than knowledge.
Imagine, miracles za Yesu zingefanyika katika karne hii, unafikiri neno famous lingeweza kumfit kwa maana angekuwa "more than famous" that's it!

Let's move our attention katika Injili Takatifu.
Marko 3:7-12
Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

"7 Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya na Yudea. 8 Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposikia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9 Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye maradhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11 Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.”12 Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu."

Ukisoma Injili Takatifu unaona kabisa umati mkubwa wa watu ulimfwata kutoka miji mikubwa ya Galilaya, Yudea, Yerusalemu, Idumaya, pamoja na Yordani.
Hauwezi kusema Yesu hakuwa maarufu?

Pia ukisoma Marko 3: 9 anawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua hili asisongwe na kubanwa sana na watu. Hii inakuonyesha jinsi gani umati ulivyokuwa mkubwa mpaka anatafuta alternative space kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwa ponya matatizo yao.

Lakini ukisoma Marko 3:12 Yesu aliwapa maagizo wanafunzi wake wasimtambulishe kwa mtu yeyote. Hii inakuonyesha hakuja dunia kusaka Fame, kuwa Celebrity au A Top Richest man in the world. Alisimamia katika mission yake ya "kuokomboa ulimwengu" na hakutaka show-off za Dunia hii, tofauti na wafalme au watu mashuhuri wa zama hizo walilewa sifa za fame, starehe na show-off za kila namna.

Umaarufu wa mtu sio lazima mpaka uwe, ama kuwepo na picha zake.
Mtu akisema Buddha - unajua alikuwa spiritual teacher wa South Asia na founder wa Buddhism.
Mtu akisema Lao Tzu - unajua alikuwa Chinese philosopher na founding figure wa Taoism in China.
Mtu akisema Griselda Blanco Restrepo - unajua Cocaine God mother wa Colombia.

Watu wazamani walisifika kwa matendo yao kuliko muonekano wao. Now days watu wanatumia sana muonekano wao kuliko matendo yao kuwa fame & celebrity.

I'm done
🙌

Robert Heriel DeepPond Da'Vinci
Splendid narration, you said it all Sir.
Gratitude ✌️✌️
 
Wasabato mnaupinga utatu mtakatifu, mnapinga fumbo la imani. Kristo alikufa, Akafufuka na atarudi tena. Nyie ndio wapinga kristo
Umehamia mada nyingine kabisa ambayo huwezi kuitetea. Nakushauri hili la picha ya kikatoliki lishikilie, na naona umeenda nalo vzr.
Lakini kuhusu mada za mpinga kristo hapo umeingia sio.
Maana mpinga Kristo ana sifa zake na ni Rc tu anafit hakuna mwingine
 
Back
Top Bottom