Mkuu kwa heshima kabisa sikubaliani na fikra yako kwasababu zifuatazo;
Yesu wakati wa uhai wake hakuwa mtu maarufu bali umaarufu wake umekuja miaka mingi baada ya yeye kufariki na habari zake kutangazwa. Sasa kama hakuwa maarufu ni wazi watu walimpuuzia ndio maana hata wakamuua kama waalifu wengine.
Ilihitajika awe mtu maarufu ndipo kumbukumbu zake ziwepo kwa watawala hasa picha sababu alitakiwa kulipia achorwe, kumbukumbu za Yesu zilizopo ni stori za mambo aliyofanya. Ni sawa na stori za babu wa machifu kabla ya kuja mkoloni kamwe hutaona picha zao bali stori tu.
Angalau kwa Mtume Mohammed yeye alieneza dini ya uislamu, ingekuwa rahisi sana kwa picha za Mtume kuwepo sababu yeye ndio mtu aliyekuwa nyuma ya uislamu tofauti na Yesu ambaye hata Ukristo wenyewe hakuuhubiri sababu yeye alikuwa myahudi na alitumwa kwao wayahudi.
Hii picha ni dhana tu au ndoto za wanadamu wa kipindi cha utambuko wakaamua kuileta tuitumie.
Jambo lingine ni uvaaji, huo uvaaji sio wa miaka hiyo watu wa zamani naweza kusema walikuwa rafu sana kuanzia nywele kichwani, ndevu zao hadi mavazi sasa yeye ilikuwaje akawa smart hivyo?, wakati alikuwa ni mtoto wa seremala tu? Mfano mzuri ni vikkings angalia walivyokuwa rafu na miaka waliyoishi ndio sembuse Yesu aliyeishi 2000 nyuma?.
Tubaki tu na imani ila hakuna uhalisia hapo.