Waliosoma shule za Ufundi (Technical schools) Tukutane hapa

Bongo ukiwa umenyooka hutaki konakona unaitwa mnoko after all hizi tech schools naona zilikuwa zamani sahvi hamna kitu hawa vijana wa tech nilikiwa nawaona vipanga ila advance weupe sana tu watoto wa kata tumejipigia tu.
Tech wale TOP vipanga wao wanakuwaga wa moto sana advance ,ila hawa wanaotoka na Div 1.15 hawa huwa ni wa kawaida sana huku mbele
 
Mkuu mkongwe sie mchikichini tulikuta pindi 300 mpka namalza form pindi likawa 400 badae si tuko advance tunalipa kwa topic pindi likawa jeroo....

Mbuga Mungu amuweke yule mjamaa ana roho safi sana
 
Partical ya Moshi Technical nipo hapa from KARUME 33.

Moto " KUTII, KUWAJIBUKA NA KUZIBUNI MBINU ZA KAZI"

Nimesoma Plumbing (CIVIL).
Engineering science ilinifanya niione Mechanics ya Advance ni nyepesi sana wakati wenzangu wanalia.
we acha tu kaka Eng inanoga sana hasa ukiweza kusolve hesabu zake basi unajitundikia A afu Physics unaitandika vibaya sana
 
cha ajabu wanakuja kusumbua sana kwenye vyuo vya Engineering
Tech wale TOP vipanga wao wanakuwaga wa moto sana advance ,ila hawa wanaotoka na Div 1.15 hawa huwa ni wa kawaida sana huku mbele
 
Nilikipiga Ifunda tech wakati huo, majengo yalikuwa hayana nuru kabisa kimuonekano japo yapo very strong.

Tulipiga sana prac kwenye somo la Plumbing tukiwa na Mwl Milinga(Mungu ambariki sana huyu mwalimu popote alipo)

Somo nililokuwa nikienjoy sana ni architectural draughting, nilikuwa naipiga sana michoro aisee.

Mitihani ya trade test ilikuwepo ila sjui kwa nini sikuipiga aise. Block A ilinihusu wakati ule.
 
Tanga Technical Secondary school
service not self
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…