Kiukweli changamoto zipo nyingi sana katika shule za umma.
Changamoto hizo zinajumuisha Kwa uchache, ukosefu wa walimu, vifaa vya kujifinzia na kufundishia, Hali duni ya malazi Kwa wanafunzi wa bweni, shida za kibajeti n.k.
Lakini pamoja na changamoto hizo, tulijaribu kutafuta utatuzi. Mfano, sisi tuliokuwa tunatoka kwetu kupitia Dar, tuliweka kambi Kwa ndugu na jamaa Dar Ili kuendelea na tuition pale maeneo ya Mchikichini na Shule ya Uhuru Mchanganyiko.
Na hapa niwashukuru sana watu kama kina Mbuga, Hidden Agenda na wengineo ambayo walituwezesha kusoma tuition zao Kwa malipo ya Tsh. 200 Kwa kipindi. Walitusaidia sana.
Na baada ya kutudi shule, hatukuwa wachoyo. Tulijaribu kuwafundisha wenzetu ambayo hawana access na walimu hawa wa tuition Kwa sababu hawakuweza kwenda Dar wakati wa likizo. Tulisaidiana kupitia group discussions na wakati wa usiku wengine tulishika chaki ubaoni kama walimu. Waliosoma Mtwara Tech ni mashahidi.
Naamini kuwa Mwalimu hawezi kutoa 100% Ili mwanafunzi afaulu. Ni lazima mwanafunzi mwenyewe ajitafutie kama kuku au mbwa.
Pia tulikutana na changamoto za kukaa Kwa ndugu wakati wa likizo pale Dar. Tulikomaa na mihogo na viazi vya kukaanga pale Mchikichini mpaka jioni unaenda kulala ubavu Kwa masimango lakini asubuhi ukiamka unarudi tena kupambana tuition. Ila Leo tumetoboa na tumepiga hatua Kwa uvumilivu.
Hivyo basi, ni lazima mwanafunzi ajengewe spirit ya kujitafutia wakati yupo kwenye mbio za kushinda vita ya ufaulu.