Tulipotelewa na mwanafunzi mwenzetu ziwa Victoria tulipokuwa kidato cha Pili, hakupatikana hadi leo.
Tulikuwa na kawaida ya kwenda kuogelea mida ya jioni pindi maji yakikatika shuleni.
Walienda kuogelea na wenzio(siku hiyo mimi sikwenda) hakurudi shuleni.
Tulikuja kugundua kesho yake kuwa fulani hayupo.
Wenzake waliokuwa nao wakatafutwa na kuhojiwa, ila hakuna majibu ya wazi yaliyopatikana.
Tulianza msako kumtafuta kwenye eneo lile kwa kushirikiana na wavuvi pamoja na wanakijiji, tulitoka kapa.
Wazazi wakataarifiwa wakaja, wakapinga kambi pale kwa wiki 2 huku msako ukiwa unaendelea. Wakafanya na mishw za kimila ila hakuna lolote lililozaa matunda.
Baada ya hizo wiki 2 tukaamua kuendelea na shule, huku wazazi wakiondoka kurudi nyumbani. Ishu ndio ikaisha hivyo, jamaa hatukumuona tena hadi leo hii zaidi ya miaka 12 imekatika.