Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Kwa mtu aliyewah kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu aje atoe experience. Nikiona mtu anatangaza kupotelewa na ndugu ua nashikwa na uchungu sana mpaka najiuliza nduguze hali ikoje.
Mwenyezi Mungu atuepushie na mitihani ya namna hii.

Polen Sana mliowahi patwa na mitihani ya namna hii
 
Aisee kuna shida ipo ndani msikilizeni. kila mtu anapenda kuwa karibu na ndugu zake ila sasa kuna mambo ya ndani ndio yanafanya mtu unachukua maamuzi magumu
Ni tabia zake tu za kilast born hakuna shida serious, hajishughulishi na chochote hata ukimuuliza tu "utakaa hivi hadi lini dogo si ufanye kazi" yani hili ni kosa kubwaaaa mnoooo la kutosha kumfanya atoroke kwamba ananyanyasika.
 
Mimi mwenyewe nimepotea nyumban tangu 2017 hakuna ndugu yangu anayejua nilipo. Kuna siku kwenye mishe zangu nilipata mteja anataka frem ya biashara nikapanga nae aje aangalie sasa nikasave ile namba kuja kuchek whatsap wakat nataka kumtumia picha kumbe ni brother niliifuta na kublock ile namba yake. nilishawahi kuona wamenipost hadi facebookk wananitafuta. Nipo dar lakini hakuna anayejua mkoa nilipo sio ndugu tu hata marafiki
Jamani,fanya kurudi nyumbani au kuwa na mawasiliano nao.
Mimi nina ndugu yangu amepotea miaka zaidi ya kumi ,yaani inauma jamani
 
Kuna maswali huwezi kukwepa hasa kutoka kwa mama. Unawajua mama zetu...
Utaishia kumuonea huruma unajikuta unarudi😀
Mie pia huwa napenda kukaa mbali na ndugu tutembeleane tu mara chache chache ila walau nawasiliano yawepo.....kukaa nao karibu huwa sitaki mambo ni mengi. Kukerana kwingi
 
Back
Top Bottom