Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Mi nimejipoteza hapa enyewe ingawa wanajua nilipo ila sitaki mazoea na ndugu wala mzee wangu!
Mwaka wa nane huu napambana na life yangu na sina mastress ningeendelea kukaa na wale makima wangeniua taratibu
Kima ndio ndugu zako? Au ni kina nani hao 🤣🤣🤣🤣
 
MAMBA
 
Bila shaka we ni Nsumba boy. Kama ni hivyo basi ulikuwa form 3 maana kipindi hicho hapakuwa na form 2. Tukio la Nsumba lilikuwa 2010 siku ya uchaguzi mkuu
 
Mm sikumbuki ni mwaka wa ngapi toka nimeondoka home, wanajua mji nilipo ila exact location hawajui, mawasiliano nilikata, kuna koo na ndugu ni konyo kabisa..U better live your own life angalau utapata amani ya moyo.
NAKAZIA HAPA.
 
Pole sana, niliwah kupitia changamoto hii kama masaa 4 hivi.... Huwa sipendi kukumbuka, ukichaa niliuona live ni mbaya sana ndugu au mtoto kupotea ghafla. Poleni sana mliwahi au mnaopitia changamoto hii.
 
Kuna wakati ndg ni nuksi sana unatamani uanze na watu wapya ndg ni km mate ya kutemwa hayarudishiki mdomoni mnaojitenga nao siwalaumu hata kidogo mi mwenyewe ningeweza ningepotea tu .....famba
Ndugu huwa na maneno sana hasa unapokuwa jobless huwa wanaongea maneno mengi sana ya kukudharau na sometimes wazazi nao wanasapoti huo ujinga. Ndyo maana raia kama DALALI MKUU wanaamua kujilipua na kuwapotezea mazima.
 
Kupotelewa kunauma kuliko msiba.....poleni wote nliopotelewa na ndugu, jamaa, na marafiki zenu

Hii thread inatia huzuni, ukiisoma huku umekunywa kidogo waweza bubujika machozi kama maji
Just imagine kuna situation unapitia kimaisha huna kazi maneno yanakuwa mengi kutoka kwa ndugu zako na kukudharau unakereka unatishia kuondoka wanakwambia ondoka na maneno kibao ya dharau km vile wa kuondoka utakuwa wewe!

Sasa siku ukifanikiwa kuondoka kila ukifikiria maneno ya ndugu zako hata hamu ya kurudi nyumbani inaisha kabisa

Ndyo maana mi huwa nasema tuchunge sana ndimi zetu hasa kwa watoto au ndugu zetu wanaopitia changamoto za kimaisha.
 
Kuna jamaa tukiwa wadogo miaka ya 90 alikuwa ndio mtoto wa mwisho kwao kati ya 7. yeye mkubwa kidogo kwetu. Sasa hakuwa na hela kama ndugu zake. Baba yake akamwambia nenda kamuulize mama yako akuonyeshe baba yako. Mimi watoto wangu wana hela. Wazee wa Moshi nyoko zao, yule jamaa wala hakuaga alipotea mazima. Kama Bahati ya Mungu nikaja kumkuta Namibia Windhoek miaka ya 2008 kashaoa na uraia kabadili na ana hela hatari. Akawa mwenyeji wangu hakuna kipind kwenye maisha yangu nikula bata kama Wakati huo. Nilikuja kuwaambia nyumbani kwao nimemuona kijana wao hawakuamin walitoka ndugu zao wanne kumfuata na Baba yao na Jan la sale. Jamaa walivyoonana ni kila mtu kulia baba yake akaomba msamaha mengine code. Long live Masssawe. We ni mtu na nusu nilijifunza sana vitu vingi kwako bro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…