2006 Kipindi Nimemaliza kidato cha nne nilienda moshi kwa demu wangu nilikaa wiki 4 sionekani nyumbani nimetafutwa kote sionekani,ndugu wamenitafuta hospital zote za dar sionekani wakajua nimekufa.
Wakati nipo moshi mjini nakula bata na uyu demu kumbe kuna jirani aliniona ikabidi apige simu nyumbani kuwa ameniona! ndugu wakamwambia mpeleleze mpaka anapokaa,kweli akajua ninapokaa akawapa taarifa nyumbani siku ile ile bonge moja la crew la watu 8 wametoka dar mpaka moshi.
Sielewi ili wala lile ghafla nikasikia mlango ukigongwa kwenda kufungua nakutana na ndugu zangu,aisee nilichezea kichapo sio cha Dunia hii nilikula bakora nilichezea mbata balaa, kuna jamaa alinipa hifadhi kwake nae akajumuishwa katika kichapo tukachukuliwa msobe msobe mpaka moshi police .
ila uyo demu ndio mama chanja wangu nimemuoa