Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Tisha sana mkuu, ukimkumbusha lazima mbavu zivunjike kwa kicheko😀😀
 
Mkuu watu tunastress ww unatuchekesha?🤣

Sema mdada ambae umepita nae katika mbanga kama hzo then mkaja kuoana aisee hyo bond ni ngumu sana kuvunjika
 
Mm sikumbuki ni mwaka wa ngapi toka nimeondoka home, wanajua mji nilipo ila exact location hawajui, mawasiliano nilikata, kuna koo na ndugu ni konyo kabisa..U better live your own life angalau utapata amani ya moyo.
Watakaoelewa hapa na waelewe ndugu wengine bora watu baki kabisa
 
Ni tabia zake tu za kilast born hakuna shida serious, hajishughulishi na chochote hata ukimuuliza tu "utakaa hivi hadi lini dogo si ufanye kazi" yani hili ni kosa kubwaaaa mnoooo la kutosha kumfanya atoroke kwamba ananyanyasika.
Kazi mnazotaka afanye zipo? Kama hana kazi akipotea mahitaji yake anayamudu vipi?
 
wateseke tu mtu ninayemuonea huruma ni mama yangu ila nikimuambia nilipo atawambia na ndugu zangu kitu ambacho sitaki.
Lakini kaa ujue wengi mnaopotea .... huwa mnarudi mkiwa hoi... kwa sababu kujitenga na wanandugu huwa kuna mapungufu fulani hivi...
 
Ndugu mkikaa pamoja ngumu sana kwenda sawa. Majungu na maneno ya kutafutana hayawezi kuisha.

Kuna familia jirani yetu uyo mbaba alikuwa anakaa na watoto wake wote apo hom. ao watoto hadi wameoa wakiwa apo hom. nakumbuka kesi ndogondogo zisiso kichwa wala miguu zilikuwa haziishi. Inaisha kesi ya huyu inafata ya yule. baadaye wale watoto wakahama pale na familia zao saivi wanatembeleana tu. Kesi zimeisha wana hususiano mzuri tu. somo apo ni ukijiweza basi nenda ukaishi kwako hata kama utashindia uji.
 
Hahahahah inachekesha, ila inafundisha pia 😂😂😂 sipatii picha mkiwa na mama chanja wako mkikumbuka tukio hilo 😂😂😂😂
 
Huyu mpuuzi, kaja kuzeekea na kutunzwa wakati ujana kala alone
sure, kuna stori live km iyo ilitokea Kenya jamaa aliitelekeza familia wakati akiwa kijana akaenda kuishi mijini huko kwa miaka mingi sana adi alipojiona ameshazeeka yani amekongoroka kabisa hana wa kumtunza kule town ndo akarudi bushi kwa familia yake. Amekuta watu hawamjui maana wale wa umri wake hawapo tena walishakufa wale watoto aliowatelekeza ndo kabisa wameshakuwa watu wazima nao hawamjui wanamshangaa.
 
Kuna jamaa ni jirani yetu walipotelewa na bro wao miaka zaidi ya 20 iliyopita hlf inasemekana huyo jamaa bado yuko hai ila hakuna ndugu aliyewahi kuonana naye live. hata dingi yao alipofariki jamaa hakutokezea. duh siri ya mtu ni kichaka.
 
Kazi mnazotaka afanye zipo? Kama hana kazi akipotea mahitaji yake anayamudu vipi?
Sijui huko huwa anapambana vipi anajua ye mwenyewe, kazi anatafutiwa ila anajizungushaaa visingizio kibao.....last born wengi wana akili zao wanazojua wao.

Last born wangu hapa nikimwambia kalale chumbani kwenu ananijibu "kabati la chumbani kwetu ni dogo" na haendi sasa kabati na kulala vinahusiana nini
 
Ni kweli maneno huwa yanaumiza na hayasahauliki.....kama hamna maneno mazuri ya kumwambia mtu ni heri kukaa kimya
 
Pale nyumbani kwetu..moshi mjini kuna familia ya kisomali...sasa mama ana watoto wa kiume watatu
Mpambanaji ni kaka mkubwa na mke anae na ana watoto wawili...
Sasa mama hampendi mtoto wa kwanza yule mpambanaji...anampa maneno ya kejeli yeye anampenda wa pili...wakati nyumba,kula shule kila kitu ni mtoto wa kwanza...yule jamaa akaona isiwe tabu
Akasepa! Hiyo 95'
Kaacha mkewe ana mimba...hapa tunavyoongea mshkaji hajawahi kurudi, mama kafa,mdogo aliekua anapendwa kafa..watoto wa jamaa ni watu wazima aliwaacha kama na 2 and 3 yers hv...yule wa tumboni nae mtu mzima....kabaki yule mdogo wake na jamaa ambe ni age yetu now...like 45-46
Sasa jamaa aliku wa mjini sana pale moshi..style za kina sawaya,john lekule au babu sambeke...ikabidi sisi watoto wa mtaani tuchekeche vibaya sana...
Kumbe jamaa alisepa akaenda kwenye machimbo ya dhahabu chunya imagine 95' hiyo..
Akapataga kichocho or kipindupindu....akadead! Akazikwaga huko huko na kaburi liko aisee!
Alietupa story ni jamaa alikuaga nae chunya na anamjua na kaburi analijua...! Hatuthubutu kuwaambia familia yake kabisa....
Huwa nawaangalia wale watoto (nikiendaga home) nafikiria mengi sana..nawahakikishia kuna siku nitawaambia ukweli wa kila kitu...RIP SAID...!
 
Rafiki yangu mmoja nilisoma nae jamaa amepotea kwanzia mwaka 2017 hadi leo hajawahi kurudi nyumbani kwao, tulikua tumemaliza Olevel hapo sasa mimi nilikua naendelea na mishe za kusoma ye aliishia hapo siku nilivyorudi nyumbani likizo nikasema niende kwao kumsalimia mama yake akanieleza kuwa jamaa alipotea ghafla wamemtafuta kila sehemu hadi mochwari lakini hawakumuoana hawajui yuko hai au amekufa, siku aliyopotea ndo siku hakupatikana tena hata kwa simu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…