Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

Waliowahi kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu mje mtupe experience

DALALI MKUU ni mshaka wa kaa kabisa. Aledisha kaa toka 2017, usikute ni yeye huyo kama yako.

Namuonea huruma mama, mtoto gani hajali mama yake anapitia sonona. Mzazi anaona amefeli kweli
Alipatikana, simu tu ilizingua. Ndo maana nakwambia Hawa washeku wakikosa watoto wao wanachangangikiwa aisee.
 
Kwa mtu aliyewah kupotelewa na ndugu au mtu wa karibu aje atoe experience. Nikiona mtu anatangaza kupotelewa na ndugu ua nashikwa na uchungu sana mpaka najiuliza nduguze hali ikoje.


Jambo gumu sana, ni maombi yangu Mungu anipe Neema nisipitie hiyo experience.
 
Kaeni vizuri na kaka yenu aseme ukweli
Ahaha umewaza siko kabisa chief. Ni mtu wa kawaida kabisaa hana maisha haaayo ni humble person kaz yake ni driver wa halmashauri..hana biashara kusema kafanya kafara. Ni mtu wa average kabisa. Na hii kitu mpaka leo huwa inam stress sana kuna muda unaona kabisa hayuko sawa
 
Ila kusema ukweli kuna mambo fulani mtu unapitia hasa kutoka kwa ndugu mpaka unatamani kujipoteza ukimbilie zako huko mbali ukaanze maisha upya na ukutane na watu wapya, Ni kwavile tu kuna watu wawili watatu ukifikiri utakavyo watesa kwa mawazo ya kupotea unaona bora kukomaa tu
 
2006 Kipindi Nimemaliza kidato cha nne nilienda moshi kwa demu wangu nilikaa wiki 4 sionekani nyumbani nimetafutwa kote sionekani,ndugu wamenitafuta vituo vyote vikubwa vya police sionekani,radio free africa mpaka ITV kile kipindi cha matukio,hospital zote za dar sionekani wakajua nimekufa.
Wakati nipo moshi mjini nakula bata na uyu demu kumbe kuna jirani aliniona ikabidi apige simu nyumbani kuwa ameniona! ndugu wakamwambia mpeleleze mpaka anapokaa,kweli akajua ninapokaa akawapa taarifa nyumbani siku ile ile bonge moja la crew la watu 8 wametoka dar mpaka moshi.
Sielewi ili wala lile ghafla nikasikia mlango ukigongwa kwenda kufungua nakutana na ndugu zangu,aisee nilichezea kichapo sio cha Dunia hii nilikula bakora nilichezea mbata balaa, kuna jamaa alinipa hifadhi kwake nae akajumuishwa katika kichapo tukachukuliwa msobe msobe mpaka moshi police .
ila uyo demu ndio mama chanja wangu nimemuoa
Alikuona, akakupeleleza na ndugu wakafika siku hiyohiyo.

Unafaidika na nini?
 
Kipindi kile Mkuu wa mkoa Makala aliposema ukimkosa mwanao politics nenda hospitali. Kipindi hiki kulikuwa na panyaroad sana

Kuna mdogo wangu mtoto wa baba mkubwa alipotea. Tulizunguka hospitali zote Dar, mochwari ndo usiseme. Tukaenda polisi Ostrrbay na vituo vingine wapi.

Kijana hakuonekana kwa siku tatu. Kila unapopita walimuona majuzi yake. Tukajua tu huyu sio kawaida take kipotea atakuwa amekufa

Siku ya nne huyo karudi yuko job hana hili wala lile. Napigiwa simu namfata namuliza kwa nini hukuwa unapatikana kwa siku 3? Ananijibu "mwanaume hatafutwi, umuliizaje mwanaume alikuwa wapi?"

Yule dogo no kum* kweli niliapa hata apotee miaka 20 simtafuti. Tutakutana Rombo kwenye matukio
Yupo sahihi Lakin. Mwanaume hatafutwi. Na pia hapaswi kujua kazaliwa lin
 
Back
Top Bottom