Waliowahi kuwa wanene au vibonge, tukutane hapa

Waliowahi kuwa wanene au vibonge, tukutane hapa

Niliwahi Kuwa mnene hadi nikawa najikatia tamaa jinsi nilivyo,unene usikie kwa jirani unachosha sana,kilo zangu hazikuwa chini ya kg120.sasa hivi Nina kg70.,kama unapiga gym na wewe ni mnene usinyanyue vyuma we pendelea kukimbia na kuruka kamba au kuendesha baskel Mazoezi haya yanapunguza mwili kwa kasi kuliko ..unapotoa jasho jingi ndivyo na uzito unashuka kwa haraka,Mimi nilifikia kuondoa hadi kilo 1 kwa siku.!
Kilo moja kwa siku...hahaha....hapana....
 
Ninafanya mazoez roho inaniuma kweli kuamka alfajir ila ntafanyaje lakin nlipungua kilo mbili nimepumzika wiki mbili et Nina 73 ndo nimeanza tena nataman niwe na 55. Lakin sijui nifanyaje kuitwa binge ni kero
 
Mimi nashindwa kufanya mazoezi wala diet, Nikifanya mazoezi two weeks haziishi naingia majaribuni napumzika[emoji21]
Mazoezi pekee mazuri ni lukimbia na kuogelea, mm kila nikiongezeka uzito nikiogelea Mara mbili au 3 napungua faster, Njoo huku bahari beach kila jioni tupeane kampani ya kuogelea baharini, its free of charge
 
Nimeanza Maji ya moto, kupunguza kipimo cha chakula jioni, kuna kilima hapa kwangu nimeamua kukipanda kila siku jioni pia, diet ni mtihani mwingene ktk Maisha
 
Mimi nilishawahi kufikisha kilo 85,kwakuwa ni mfupi kidogo nilikuwa napata mateso ya ajabu sana,sikuweza kukimbia na nikikimbia moyo unaenda mbio sana,nikinyanyuka ghafla napatwa na kizunguzungu,nikilala nilikuwa nakoroma hatari,nilkuwa siwezi kufunga kamba za viatu na nikifanikiwa kufunga basi ni kwa taabu sana,nikiwa toilet hasa hivi vya kuchuchumaa ni mateso tupu,bado kwenye mambo yetu yale,ukimaliza moja unakuwa hoi sana,ila sasa hivi nacheza na 72kg duh ni hatari,niko vizuri ajabu,mpaka kuna wakati mwingine huwa nakuwa kero...
 
Mazoezi pekee mazuri ni lukimbia na kuogelea, mm kila nikiongezeka uzito nikiogelea Mara mbili au 3 napungua faster, Njoo huku bahari beach kila jioni tupeane kampani ya kuogelea baharini, its free of charge
Kuogelea sijui hataaa, Bahari beach ndo wapi huko? Maana huku kijijini kwetu hakuna ziwa wala bahari
 
Ratiba ya kupunguza uzito na unene :
Kwanza Unatakiwa ukichukie kile unachokipunguza na uheshimu maamuzi yako... Then Katika siku yako ya mchana,I mean 12 hours Uwe unatumia 30 minutes kujiunguza kwa mazoez..
1.Kimbia mwendo wa kawaida kabisa ambao unakuwa haukuumizi wala kukutia uvivu kuendelea Kukimbia... Unatakiwa ukimbie kwa muda wa dakika 15 kwenda na kurudi bila kujutia Mbio hizo... Usijikomoe Kukimbia kwa speed Kali... Just maintain.

2.Ukirudi Kukimbia usisimame wala kujiinamia... Chukua kamba urukeruke angalau mara 100 bila kusimama....

3.Ukimaliza kuruka kamba,chukua kamba uifunge Katika pande mbili iwe usawa wa Chini kidogo ya goti lako then uanze kuruka kama warukavyo watoto wakicheza mchezo wa kuruka kamba... Uruke kuanzia Mara 20 ( kila upande mara 10 kwa mpigo)... Ukimaliza kuruka nenda sehemu flat na ujilaze kwa kurelax.

4.Ukimaliza kujilaza kwa kurelax kwa dakika 1.,Anza Kupiga skwash 20 kwa mpigo ukiunganisha na push up 30 hadi 45 kwa mpigo (hapa kwenye push ups lazima upige kutokana na jinsia yako... Kuna push ups za kike na kiume...na usipige haraka haraka nenda taratibu ).

5.Malizia kwa kunyoosha viungo vya mwili wako wote taratibu kabisa...hakikisha unanyoosha
Shingo
Kiuno
Nyonga
Tumboni
Mgongo
Joint zote za mwili
Vidole Vyote vya mwili.
Ukifanya hvyo kwa muda wa wiki 2 Utajikuta unaanza kuwa addicted na mazoezi kwani Utakuwa unapiga zoezi ambalo halikuumizi wala kukukera... Na Kadri siku zinavyokwenda Utajikuta unaongeza muda wa Kukimbia na utaongeza mazoezi pia kwan utajengeka na sio kujikomoa... Wengi hushindwa kuendelea na mazoezi kutokana na kufanya kwa pupa ili wapungue kwa kasi bila kujua kuwa Moyo hauko tayari kupokea mazoez makali kwa Ghafla hvyo kujikuta wakikimbia au kuacha kabisa zoezi
 
Kuogelea sijui hataaa, Bahari beach ndo wapi huko? Maana huku kijijini kwetu hakuna ziwa wala bahari
Oh sorry nilijua Upo Dar, Bahari beach ni maeneo fulani ya kishua huku Mjini, huku Tunaishi watu wenye test ya kikoloni tu.

Ukija nitakuleta usijali mtoto mzuri
 
Pia kila asubuhi na jioni kunywa maji yenye uvuguvugu mix na ndimu,nusu kikombe katka empty stomach...usiache kunywa Chai kwa kudhani ndo kujikondesha... At least skip menyu ya mchana na jion kula Kiasi na vyakula Laini
 
Mimi niliwahi kuwa mwembamba sasa hivi nafukuzia kilo 100.

Yaani kama nimepewa tenda ya kunenepa.🙄
Mwenyewe nilikuja kushtuka nakaribia kupasuka nikaona sasa hapa ntakosa na wachumba.[emoji2]
 
Nineanza kufanya hivyo nakaribia wiki sasa, Nipo mrefu kiasi
Urefu-100=Average weight(AW). Kuongezeka au kupungua 5kg kwenye hiyo Aw sio mbaya. Ila zaidi au nje ya hapo. Ni NOUMAAAAAAAAAAAAAAA
 
Unene ni shida mimi nina kg 117.2 mwaka wa 3 sasa last year nilijitahidi kupunguza kidogo ikafika 14.5 ila juzi nimepima iko pale pale wakati mimi natamani kufikia 85-90 hapo ndio nitakuwa vzr.. thou mimi ni mrefu lakini weigh hii hapana aise
 
Back
Top Bottom