Yule Boss wangu wanamkumbuka na mdada fulani alikuwa Head of Department yetu...Kuna boss wangu alikuwa mdini sana ,tena mlokole wa kuweka vifungu vya biblia kwenye status kila siku.
Alikuwa mzee wa kupiga domo na ushauri kama yule Mtaka ,sijui ni DC au RC ..Wanafanan kwa kujifanya wanapenda kutoa ushauri wa maisha na mambo ya uchumi..Huyo boss alikuwa katili sana na mnafiki hakuna ,kuna project zake ilikuwa hana jinsi ananiteua kama Chairman ,naandaa mpaka Minutes za kikao ila kwenye malipo anamuita mgalatia mwenzie wanapeana ,walikuwa wawili ila nashangaa wananitenga wala sipo hivyo.
Yule mzee alikuwa safari anaenda yeye na jamaa ,yaani anambeba mpaka Mhasibu , marketing officer na wengine ambao wako chini yangu ila mimi ananifungia vioo ,kisa ni dini. Siku fulani aliniita akiwa serious maana alikuwa ananitafutia kosa ,akaniambia wewe unaabudu majini ila nilicheka sana na wala sikumjibu.
Kabla ya kuletwa hapo kwetu ,kuna jamaa alinipa tahadhari kama huyo jamaa ni mdini sana ,hivyo jiandae.