Nafikiri Wizara ya Kazi, Ajira, na Maendeleo ya Vijana ndiyo hasa inawahusu wamachinga. Katika maeneo yote inawagusa, suala la wao kujishighulisha na kazi zao za uchuuzi, ajira zao zisizokuwa rasmi katika sekta binafsi na pia fursa za maendeleo zilizopo kwao kwa kuwa wengi wao bado ni vijana.
Machinga tunawaona wakijibiidisha kutafuta maisha, ni vijana wenye nguvu na afya. Kamwe huwezi kuwaweka katika kundi maalum, yaani wao pia watambulike kama watu wenye "special needs". Hapana! Hapana! Hapana hata kidogo.
Ushauri mwingine unapaswa kuchujwa na wahusika kabla ya kupokelewa na kutamkwa hadharani. Hata fanani mwenyewe anapaswa kuwa na ufahamu mzuri wa mambo anayotaka kuyaongelea kabla ya kwenda hadharani na kutoa tamko kwa hadhira.