Wamachinga kuwekwa kundi moja na wanawake watoto na walemavu ni matusi kwao

Wamachinga wetu wamefurahia nakupiga makofi
Hao waliopiga makofi sio machinga ni uvccm waliokuwa wamepangwa. Amini nakwambia chinga wa kweli Kama Mimi siwezi kumpigia makofi hangaya kaharibu mfumo wa maisha yangu kwa kunivunjia kibanda na kunipeleka mapolini ambako hakuna wateja mtaji umefirisika Sacco's wananichukulia vitu ndani kwakukosa rejesho....naichukia Sana awamu hii
 
Hata mm nimewaza wale ni watu wa mchongo tu wanatumika kufanya siasa
 

Inawezekana, kimantiki na kwa perception, huo uamuzi unaonekana sio sawa, lakini kama hiyo wizara itapewa tools zinazohitajika kuwasaidia machinga, lengo lililokusudiwa bado linaweza kufikiwa.

Kumbuka, hata wakiwekwa kwenye wizara ambayo, kimantiki na kwa perception, ndiyo wizara sahihi, lengo lililokusudiwa bado halitafikiwa iwapo hiyo wizara haitapewa tools zinazohitajika. Jina la wizara pekee yake halina uwezo wa kuwasaidia machinga!
 
Wamachinga ni mradi mbaya kufanywa na serikali, ni sawa na mgonjwa anayepewa pain killer ila hapelekwi hospitali. Ipo siku huu mradi utaizidi nguvu CCM na serikali yake.
 
Let's call a spade a spade, ishu sio kupatiwa tu tools za kuwasaidia hivi unaweza ukamchukua mtoto wa kiume uamue umpeleke shule ya st francis mbeya simply kwamba kuna tools za kumwezesha kufaulu vizuri?
Tambua kwamba kila wizara imeundwa kwa mantiki yake na kila wizara ina tools na instruments za kutekeleza majukumu yake.
Haiingii akilini kwa wamachinga kuwekwa kwenye hiyo wizara ambayo majukumu yake ya kimsingi yanajulikana
 

Analogy yako ya “…mtoto wa kiume…” sio appropriate kwa case ya machinga. Hapelekwi machinga mmoja kwenye hiyo wizara. Labda useme “…watoto wa kiume…”, kitu ambacho kinawezekana kabisa provided that shule inakuwa equipped kukidhi mahitaji ya watoto wa kiume.

Instruments za wizara sio static. Hubabadilishwa kujibu mahitaji ya wakati husika!
 
Soma miongozo ya nchi ndugu yangu, usiongee kwa hisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…