Wamama wananguvu kubwa ya ushawishi kwa watoto, kuwa makini kama umezaa na mwanamke ambaye hauishinaye

Wamama wananguvu kubwa ya ushawishi kwa watoto, kuwa makini kama umezaa na mwanamke ambaye hauishinaye

Naufahamu sana na maisha .... ni kwa asilimia chache sana mtoto akutafute na hata akikutafuta bado ile bond haitokuwepo . Futa huo mtazamo wako
Bond gan unaongelea wewe? Bond iko kwenye chromosomes za mtoto tayari.
 
Kwahiyo wewe tu ndiye umeletwa duniani na unaelewa kuhusu maisha?.

Au ni wewe tu toka uzao wa kwanza wa Adam hadi leo, so mambo ya familia wengine hawana uzoefu nayo?.
Hebu endelea kumpa shule huyu. Na inaelekea ni singo mama ambaye anataka kumtumia mtoto kuchuma kwa kigezo cha nadharia hii feki

Wababa msihofu, pigeni mimba halafu mama mtu akizingua mpotezee mazima. Lkn mtoto atakutafuta tu!
 
Hebu endelea kumpa shule huyu. Na inaelekea ni singo mama ambaye anataka kumtumia mtoto kuchuma kwa kigezo cha nadharia hii feki

Wababa msihofu, pigeni mimba halafu mama mtu akizingua mpotezee mazima. Lkn mtoto atakutafuta tu!
Nina hakika kwa asilimia mia moja wewe utakuwa umetelekeza watoto wako na hauwahudumii 😀😀😀
 
Nina hakika kwa asilimia mia moja wewe utakuwa umetelekeza watoto wako na hauwahudumii 😀😀😀
Hapana. Kwanini unasema mtoto atakosa bond wakati yeye ndiye kawazaa?

Halafu hiyo nadharia yako umeitoa wapi? Mbona huku kitaa tunaona watoto wakiwatafuta baba zao ambao hawakuwa wakiishi nao?
 
Hapana. Kwanini unasema mtoto atakosa bond wakati yeye ndiye kawazaa?

Halafu hiyo nadharia yako umeitoa wapi? Mbona huku kitaa tunaona watoto wakiwatafuta baba zao ambao hawakuwa wakiishi nao?
Inatokea lakini mara chache sana , kama mama mtu alikukandia kwa mtoto wake ile sumu inakuwepo kwa mtoto ni ngumu kukutafuta
 
Inatokea lakini mara chache sana , kama mama mtu alikukandia kwa mtoto wake ile sumu inakuwepo kwa mtoto ni ngumu kukutafuta
Wamama wa hivyo unakutaga ni wale maskini, kwahiyo hata watoto wa hivyo huwa hawana future nzuri.

Sasa unataka mtoto ambaye anaishia kuwa mama ntilie, bodaboda, barmaid au konda atamsaidia nn baba hata akimtafuta?
 
Nitamuhudumia na kujitahidi kadri niwezavyo nimuwezeshe ki elimu na ki uchumi. Aidha kwa yeye kutokujua au kwa kujua. Akikua badaye na kuona mimi sifai wala I don't care as long as nimetimiza wajibu wangu hata nikirudi kwa Mungu narudi nikiwa nimenawa.

Bahati nzuri nowadays tunawasaidia watoto kwa ajili ya faida yao. Huko uzeeni nitakula nilichowekeza nilipokuwa kijana.

Siogopi mama yake atamwambia nini na wala sina haja ya kumuaminisha kwamba mimi nilimsaidia. Sifanyi ujinga huo aisee. Akitaka aamini na asipotaka kuamini basi
 
Kwa Dunia ya Sasa hivi Kuna mtu anazaa watoto ili waje kumsaidia?
 
Hahaha .. kwahiyo issue muhimu mshua ujiweze kiuchumi
Sio kiuchumi tu,
Huyo mtu anaweza kuja kuwa na famili na watoto wengine huko.Huwezi jua nani atakuja kuwa nani.
Kikubwa tafauti za wazazi, watoto wasihusishwe.
Kuhusisha watoto kwenye tofauti hizo ni ishara ya namna gani ulikuwa tatizo kwa mwenzio
 
Hebu endelea kumpa shule huyu. Na inaelekea ni singo mama ambaye anataka kumtumia mtoto kuchuma kwa kigezo cha nadharia hii feki

Wababa msihofu, pigeni mimba halafu mama mtu akizingua mpotezee mazima. Lkn mtoto atakutafuta tu!
Huyo kijana yamemfika na madogo (wanae) hawamtambui for a longer hivyo kaja na kaevidence kake hapa akidhani yeye ndiye wa kwanza kuzalisha na kukimbia mtoto.

Ni kweli wamama wana kapower ka kuharibu watoto lakini siyo kuharibu hadi mtoto ashindwe kuhoji mamake "kuwa ulibebaje mimba kuwa ni ya hospitali au kitandani?.

Moto wa volcano
Dunia imehama pakubwa sana, kutoka kwenda kijijini sijui Burkima huko kufuatilia babako, now unaingia social media unaandika habari zako za kumtafuta na umfaham babako ili umchambe tu 😁!.
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Kuna jamaa yangu mwaka jana alipata kazi kampuni kubwa sana alinipa story yake nilishangaa sana.

Ananambia katika maisha yake mama yake alimuaminisha kwamba baba yake ni mbaya mpaka ikafikia hatua baba akawa anakosa ujasiri wa kumshauri au kumwambia chochote jamaa. Lkn nyuma ya pazia kumbe jamaa alivyokuwa Primary baba ndo alimlipia ada na kila kitu cha shule. Lkn alivyofika sekondary mzee akaona ili isilete ugomvi huku kwenye familia yake (baba tayari alikua ameshaoa mke mwingine) na wakati mwingine kuna kukosa pia ili mwanaye asikwame ada akamfungulia mama biashara nzuri ya mtaji mkubwa tu. Na akamwambia kabisa kwamba hii biashara ni kwa ajili ya mwanangu asikwame ada

Jamaa anasema katika kukua kwake amemkuta mama anafanya hyo biashara na jamaa anasema nilikua nikimuona mama anatoa hela kwenye hyo biashara analipa ada. Jamaa anasema yeye pia amekua akihusika kwenye hyo biashara na mama yake anamkandia sana mzee kwamba hamsaidii chochote. Na jamaa anasema kweli nikiangalia ni mama ndo anakomaa na biashara ananilipia ada. Kumbe kuna ukweli ambao mama hakumwambia mtoto.

Sasa funga kazi jamaa alipigiwa simu na mtu mmoja akamwambia kuna kazi kampuni flani jaribu utume maombi, akamtumia na tangazo. Jamaa ananambia hakutaka hata kujua aliyemtumia hlo tangazo ni nani maana mchongo wa kazi ukishakuja mezani kikubwa ni kufanya application.

Kumbe huyo alomtumia hlo tangazo alitumwa na baba yake. Baba kumbe ashasuka mchongo kila kitu, kama mnavyojua kazi za mjini wakati mwingine inabidi upasuke ili uipate. Mzee kumbe kashatoa hela kibao kwa ajili ya kumsafishia njia mwanaye. Jamaa ananambia anashangaa namna interview ilivyokua kuna namna flani mambo yalikua smooth mchizi kaingia kazini.

Jamaa anasema alikaa miezi sita hajamwambia mzee kama amepata kazi na wala hajamtumia chochote mzee kwa kuamini kwamba mzee anazingua maana kapambaniwa na na mama yake mpaka amepata kazi kwa hustle zake binafsi.

One day walienda Arusha kikazi huko walikutana staff kutoka branches za nchi nzima. Ananambia HR mmoja yeye yuko branch ya Dodoma alipata taarifa kwamba anamuulizia. Walivyokutana ndo akamuuliza wew ni mtoto wa fulani? Jamaa akasema ndiyo unamfahamu? katika story story ndo akaja kujua kwamba mzee ndo alisuka mchongo mzima na hata lile tangazo la kazi alotuma ni yule HR. Ndo jamaa ikabidi agutuke akaona pengine baba kuna vitu vingine anaweza kuwa amefanya kimya kimya bila yeye kujua.

Jamaa ananambia alikuja kujua vitu vingi ambavyo mzee alikua anamfanyia lkn kwa kupitia kwa mama wala hakutaka kuonesha kwamba amefanya.

Jamaa alinia?ambia alimtafuta mzee akamuomba msamaha sana. Mzee alisema mimi nilishakusamehe hata kabla hujanikosea kilio changu ilikua ni kuona wew una maisha mazuri na kazi nzuri. Mengine namuachia Mungu tu ndo anajua ukweli.

Hii scenerio ya huyu jamaa ilinifundisha sana. Yani jamaa anakwambia wanawake siwaamin aisee. Yani hata girlfriend wake huwa anamuangalia ananambia hata huyu kuna siku atanigeuka huyu .😀
 
IKUMBUKWE NYAKATI ZIMEBADIRIKA SANA,
ZAMANI WATU WALIKUA WANAZAA WATOTO WENGI ILI WAJE KUPATA USAIDIZI UZEENI.
ZAMA HIZI, WATOTO NDIO WANAWEZA KUHITAJI USAIDIZI WA WAZEE WAO!
MWELEZE MTOTO WAKO BABA YAKO NI SHETANI, MBWA, NYOKA, MAREHEMU, NK NK.
HALAFU UNAKUJA KUKUTA HUYO HUYO MZEE ANA UCHUMI MZURI, CHEO KIKUBWA,KIASI WEWE NDIO WA KUMTEGEMEA!

Mithari 18: 20-23 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi.
Mkuu herufi ndogo una ugomvi nazo?
 
Back
Top Bottom