Wamama wananguvu kubwa ya ushawishi kwa watoto, kuwa makini kama umezaa na mwanamke ambaye hauishinaye

Ndo maana inatakiwa tuoe wanawake wenye dini hapa maandiko Yana maanisha afya njema ya akili
 
Zama zimebadilisha live your own life hata ukiwa nao karibu lakini usiweke mategemeo nao.
Ukiwa masikini hata wanao na mkeo watakutenga.
 
Zama zimebadilisha live your own life hata ukiwa nao karibu lakini usiweke mategemeo nao.
Ukiwa masikini hata wanao na mkeo watakutenga.
Ni kweli usemalo maana hata maandiko yanasema mtu maskini atatengwa hata na ndg zake . Lakini jambo la muhimu ni kuithamini damu hako usiruhusu watoto wateseke wakati uwezo wa kuwahudumia unao
 
Ili kuepuka yote hayo muwe mnalea watoto sio kuwatelekeza baadae wakiwa na mafanikio mnajisogeza
 
Labda wa kwako ndugu hawatakutafuta ila hata ikiwa umebebesha mimba na kupotea iko siku utatafutwa tu, whatever ulitoa au hukutoa matunzo.

Kitanda hakizai haramu.
Sasa hata akikutafuta unadhani itabadili nini? Kama hukuwahi kutengeneza bond wakati akiwa mdogo unadhani utaweza wakati akiwa mkubwa? Kwanza unakubali vipi mwanao afundishwe maadili, Mila na desturi na baba mwingine? Atakapokuja kila mtu atamuona mwenzake stranger na hapo ili mambo yende inabidi wewe baba ndio uwe mpole!
 
Labda wa kwako ndugu hawatakutafuta ila hata ikiwa umebebesha mimba na kupotea iko siku utatafutwa tu, whatever ulitoa au hukutoa matunzo.

Kitanda hakizai haramu.
atakutafuta aone hilo sura lako limekaa kaa kivipi baba mwenye roho mbaya wewe! Halafu atapotea kabisa. Labda kama ndugu zake watampokea ndiyo anaweza kujiunga nao kifamilia.
 
Haijalishi unaishi nae ama huishi nae. Unataka watoto wakuseme vizuri lazima mama yao awe anakusema vizuri kwao.

Mwanaume hakikisha una vitega uchumi vyako mwenyewe vya kukufanya uishi kama mwanaume hata ukiwa na miaka 100 watoto watakuheshimu tu hata kama hauishi na mama yao.
 
Hili halina ubishi...
 
atakutafuta aone hilo sura lako limekaa kaa kivipi baba mwenye roho mbaya wewe! Halafu atapotea kabisa. Labda kama ndugu zake watampokea ndiyo anaweza kujiunga nao kifamilia.
Pole kwa kukimbiwa na babako, naona umekuja na povu kumalizia hasira kwangu.
 
We acha tu!
 
Ili kuepuka yote hayo muwe mnalea watoto sio kuwatelekeza baadae wakiwa na mafanikio mnajisogeza
Kosa kubwa tunafanya wanaume ni kuacha mwanamke! Unatakiwa mwanamke akuache yeye, hapo hakutakuwa na shida. Ila ukimuacha wakati bado anakutaka, hakuna rangi hutaaacha kuiona hapa duniani, na hata ukifa kaburi lako akiliona lazima alichape na fimbo.

Si wote hatutoi matunzo, tunatoa hadi wanafika 20 years ila shida ipo pale pale. Ukizaa na mwanamke unalo hilo hadi Golgota.
 
Inatokea lakini mara chache sana , kama mama mtu alikukandia kwa mtoto wake ile sumu inakuwepo kwa mtoto ni ngumu kukutafuta
akiwa bado mdogo mama anaweza kumlisha sumu za maneno kadri awezavyo. Lakini mtoto akikua akawa mtu mzima akaweza kupambanua mambo na kujua kati ya baba na mama ni nani mjenzi wa familia na ni nani hubomoa familia. Hapo ndipo mtoto hufuta maneno ya mama yake kichwani na kumuuliza baba yuko wapi mama nipeleke kwa baba!
 
Pole kwa kukimbiwa na babako, naona umekuja na povu kumalizia hasira kwangu.
Baba yangu mimi hakupotea bali alifariki nilipokuwa na umri wa miaka 7. Lakini kwa hiyo miaka michache niliyokuwa naye alitupenda sana na kutushughulikia kwa kila hali.

Unaweza kuamini kuwa katika miaka ya sitini kabla ya kufariki sisi tayari alikuwa ametufungulia account bank, kila mtoto na account yake, kila mwezi deposit Shilingi 5 kwenye kitabu (zilikuwa nyingi sana enzi zile). Mungu akupe baba wa aina gani tena? Ni bahati mbaya kwamba alifariki wakati sisi tukiwa wadogo lakini mimi namshukuru Mungu na kumuombea dua ya kumpa malazi mema peponi.

Hao mababa wa design za generation Z ndiyo munaohangaika hivyo.
 
Kama baba alikimbia mimba na malezi mtoto akiwa mdogo sioni haja ya mtoto kumtambua. Ila kama baba aliwajibika mwanamke anaemjaza mtoto upuuzi wa kumfanya amchukie baba ni shetani mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…