Wamiliki wa lodge kuweni serious

Wamiliki wa lodge kuweni serious

12. Bed sheet jeupee, godoro limechakaa na limevunda
13. Makahaba wanaruhusiwa kiholela kuja kusumbua wateja, Jambo linaloweza kuhatarisha usalama wa mteja na Mali zake.
14. Kibao Cha Lodge kimeandikwa kuna breakfast na TV lakini hakuna kitu.
15. Kiti Ni kibovu, unakikalia unajikuta umeanguka kwa kisogo, unazirai ukija kuzinduka umeibiwa kila kitu
Bora kuibiwa kuliko kuzinduka hauna mshipa wa taarabu.
 
Mwisho kuna wateja wasumbufu, hawana hekima unakuta taulo zipo na ni safi lakini wake kwa waume wanajifutia mashuka au foronya, sio ustaarabu, ni vyema mteja unapodai huduma bora na wewe mwenyewe ujiheshimu na kutunza kila kitu kwa ufasaha kama ulivokikuta
 
Kuna lodge nililala Kakola Shinyanga eeeh bwana chumbani aliingia yule mdudu mweusi kama mpanzi.

Huyo mdudu Kelele zake zinatakiwa azipigie nje kwenye uwazi sio chumbani aisee triiiiiiiiiiiiiiiìiiiiiiiiìiiiiii triiiiiiiiiiiiiiiiiiìi usiku kucha sauti yake nilikuwa naisikia kwenye ngoma ya sikio.

Niliamka kichwa kinaniuma Asubuhi, mawazo yangu nilijua mdudu yuko nje ya dirisha. Wakati navaa viatu nikamwona aisee nilimkanyaga kwa hasira.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa wakuu nitachomekea machimbo ya ifakara, mbinga, kahama, ambayo yana sifa bora na masafi mkifika huko direct mnaenda hapo mtahidumiwa vizuri sana kwa weledi mkubwa na bei kote ni 25k

Haya machimbo ya mbinga, kahama na ifakara, yana maji ya uhakika yaani ukiacha maji ya bomba lakini wana visima na maji ya moto masaa 24, ukitaka ya barid pia masaa 24, lakini wasafi sana
 
Siku moja Moshi mjini mitaa ya Majengo nilichukua room kwenye lodge moja, 20k. Nilipoingia tu nikafunga mlango wa room kwa funguo, nikavua nguo direct kuoga bafuni. Huko bafuni nililazimika kurudishia mlango maana bafu ni dogo sana. Ile nafunga mlango nikasikia kitu kinaanguka upande wa pili wa mlango (upande wa chumbani). Sikujali nikaendelea kuoga.

Nimemaliza kuoga nafungua mlango haufunguki. Kumbe handle ya kitasa upande wa nje na kile kijichuma kinaunganisha handles na kitasa ndio vinedondoka.

Niliita wahudumu kwa nguvu sana ila wasisikie mpaka koo likauma na matusi yote hapo nimeshamaliza, na hakuna hata mteja mwingine room jirani anisikie awaambie. Wamekuja baada ya nusu saa hivi ila hawawezi kuingia chumbani kwangu kwani nimefunga. Funguo za akiba hawana anazo boss mwenye guest house. Boss amepigiwa yupo mbali, shambani. Alikuja baada ya kama 3hrs hivi. Muda wote huo nipo chooni tu.

Walipofungua nikatoka. Jicho nililowakata wakaelewa namaanisha nini. Wakanirudishia hela yangu bila kusema chochote nikaondoka kutafuta lodge nyingine.
hahahahh pole sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila inabidi uwe wazifuatilia mara kwa mara maana wahudumu lazima watazipindisha ili wale pesa za short time

Ukiona lodge inatumika sana kwa short time ujue haina uongozi bora, yaani hapo kwanza kama ni 25k mtu akija na 10k aruhusiwe, hapana bei ni moja kama ni 25k ni hiyo hiyo hata ukikaa dakika kumi na tano ni wewe na zaidi kinachofanyika kuna vyumba ambavyo unavitenga kabisa kua hivi viwili au vitatu ni vya dharura ikitokea lakini vingine vinaheshimiwa ni vya kulala na hata room hizo za dharura pamoja na kuvitenga hivo ni siri ya uongozi na lazima vifanyiwe usafi mara kwa mara, akitoka mmoja kufanya mambo yake ni muhimu kubadili mashuka na kila kitu, na zile nyingine zifuliwe ndio maana room moja walau iwe na pea tatu hadi nne za shuka ili usilete usumbufu na zile airfreshner ndio huapply hapo sasa
 
Back
Top Bottom