Wamiliki wa mabasi wapandisha nauli kwa wanafunzi, SUMATRA na Polisi wabariki kadhia hii

... unayemsifia ni failure. Angekuwa smart kama unavyotaka tuamini angejenga mifumo imara hata baada ya kuondoka kwake mambo yangeenda sawa. Badala yake was busy kuji- brand yeye. Alidhani angeishi milele? Na hilo ndio tatizo.
 
Jambo la kupanda kwa gharama za vitu ni kawaida sana ukilinganisha na kupanda kwa bei ya mafuta (fuel). Kiuchumi inafanya nchi kuwa imara, kuimarika kwa nchi hakui kwa bidhaa kuwa rahisi. Nchi inaimarika kiuchumi kupitia kodi na mneso wa bei za vitu vya lazima kama mafuta ambayo serikali yenyewe ndiye mteja mkubwa. Sasa kwenye upande wa kodi raia tumepata hauweni hivyo tutegemee upande mwingine huku mseleleko hautokuwepo, shariti tujikaze tu. Kwani kama na huku kwenye mafuta kukipooza nchi itadorora kiuchumi hivyo kutufanya tusipate katiba yetu mpya ambayo mambo yakijiseti tunakuwa nayo mezani.
Hivyo watanzania wenzangu tuweni wapole na tuwe na subira...! Ile topic ya Isostacy kwenye georaphy ina maana sana..!
 
Wa Bajaj mbona bei yao ni kubwa na wanatumia barabara hizihizi? Kwanini tuwabane wenye mabasi tu?
 
Wamekwamia stand ipi?

Afu unakumbuka kipindi cha risiti za kielekroniki awamu ya Jiwe nauli zilioanda? Maendeleo yana gharama..hii nchi imejaa walalamishi na wakulaumu,lazima kutoa kodi kuchangia maendeleo no way out.

Mwingine alikuwa analalama kodi ya kindergarten utafikiri alilazimishwa kupeleka mtoto private
 
Kwani Kuna nauli maalum ya wanafunzi kwa mabasi ya mkoa?? Ilianza lini
 
... unayemsifia ni failure. Angekuwa smart kama unavyotaka tuamini angejenga mifumo imara hata baada ya kuondoka kwake mambo yangeenda sawa. Badala yake was busy kuji- brand yeye. Alidhani angeishi milele? Na hilo ndio tatizo.
Magufuli hakuwahi kifeli wewe kilaza. Ndo maana unabweka hapa kumfatilia kila siku. Waliofeli hawajadiliwi kila siku kama wewe nyumbu ambavo hutajadiliwa.
 
Mkuu, siku hizi haiitwi SUMATRA(Surface and Marine Transport Regulatory Authority), bali ni LATRA (Land Transport Regulatory Authority). Asante.
 
Wakati wake vitu havikupanda? Unakumbuka aliikuta sukari ikiwa shilingi ngapi? Mafuta ya kula je? Petro, dizel na mafuta ya taa je? Wacheni kujiambatanisha na watu waongo. Uongo ndicho pekee huyu ndugu alichofanikiwa.
 
Mafuta yamepanda so almost every thing kitapanda tu sijui hawakufikiria hili na waziri wa fedha eti ni mchumi loh
 
Hahahaaaaa mamaa anaangushwa bila yeye kujua
 
Kwamba asingefanya haya angeweza kubadili jambo pale bungeni? [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Mkuu ile bajeti ilipita kama tonge kwenye mrenda!

Fikiria wana harakati wote tangu twitter, jf, facebook, Instagram na kwenye magroup yote ya chadema kulikuwa na kampeni yakusaini petition ili Diamond atolewe tuzo za BET kisa alimpigia kampeni Magu!

Na wengine wakawa wanademka na mama wakimsifu kwa hatua yake ya Sabaya kukamatwa. Wakisema mother anaupiga mwingi sana.

Wakati haho yakiendelea bajeti ya mwigulu ikapita bila kelele zozote!
 
Wakati bungeni Mwigulu anawasilisha bajeti na kuongeza shilingi 100 kwa kila Lita moja ya petrol mlikuwa bize kupiga Umbea Instagram.


Sasa hayo ndio matokeo yake Hadi pale mtakapokuwa serious na Mambo yanayogusa maisha yenu. Natamani nauli za mabasi zifike Hadi 500,000 ili mpate akili.
 
kodi ya mafuta imepanda, unategemea wenye mabasi wafanye nini? Anayeuumia ni final consumer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…