Wamiliki wa mabasi wapandisha nauli kwa wanafunzi, SUMATRA na Polisi wabariki kadhia hii

Wamiliki wa mabasi wapandisha nauli kwa wanafunzi, SUMATRA na Polisi wabariki kadhia hii

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ulikuwa busy kushangilia Sabaya kupelekwa kisongo na kusaini petition ya kumtoa Mondi Bet, so shut up

Hata asingeshangilia ingemsaidia nini? Bungeni si mmejazana machangu wa kijani tupu?
 
Wewe ulitakaje? Au Serikali Ina mabasi?
Mama ameshawaachia wafanyabiashara waongoze nchi yeye ale maisha
Tangu nimeanza kununu petrol sijawahi ona hii bei
 
Jiwe alikuta sukari kilo inauzwa 1500 mwaka 2015, mwaka 2018 sukari ilianza kuuzwa 2500 mpaka leo.
Yaani hizo kodi na tozo kibao wabunge wenu walivyokuwa wakizigongea meza bungeni, watz mlitegemea nini kitatokea baadae.. kubalini maumivu tu.
 
Naomba kutoa ufafanuzi kwenu wademkaji, nauli zilizowekwa na serikali zinajulikana. Leo Hadi mid next week shule zinafunguliwa. Serikali kupitia LATRA na Polisi walipaswa kudhibiti upandaji holela wa nauli kinyume na nauli elekezi lakini awakufanya hivyo. Leo hii mbezi nauli ya Mbeya 80,000, Arusha 50,000 ,Mwanza 80,000 kitu ambacho nikinyume kabisa na taratibu.

Wanapaswa kufanya msako kwa kuhoji abiria huko njiani wamelipa nauli shs ngapi nakuchukua hatua kwa mabasi yote yaliyozidisha nauli. Hi nikuwakomoa wananchi na kuwanufaisha matajiri wachache.

Wasipochukua hatua Hali hii yakujipangia nauli itawaumiza watu na hakutakuwa na umuhimu wa bei elekezi
 
Inahuzunisha sana, lakini ndiyo huvyo, mafuta yamepanda...
 
SUMATRA na Polisi mnaposhindwa kudhibiti kadhia ya ongezeko holela la nauli kipindi hiki Cha kurejea mashuleni kwa wanafunzi tunashindwa kuelewa mnapewa nn na wamiliki wa mabus.

Wanafunzi wasio na fedha wamekwama stendi mikoani kwa kushindwa kupata huduma, mabus yanakata tiketi kwa bei wanazojiamulia na mnajua kabisa ila hakuna udhibiti. Tunafika ofisini kwenu mmefunga ofisi mmelala mnatusaidia nn? Stend kuu Dar Hali Ni tete watoto wamekwama kwenda shule kisa ukubwa wa nauli.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani unamsubiri Waziri na Mhe Rais aseme? SUMATRA mnasubiri nn kutoa taadhari kwa umma Kama miaka ya nyuma, au mnatingisha kiberiti?

Naamini hii kadhia itaondoka na watu msipowakamata wale wote waliopandisha nauli. Simamisheni mabus muhoji wamelipa nauli kiasi gani abiria mtagundua bei siyo elekezi Ni bei tapelezi
Ni vizuri ungetoa mfano halisia kama kuna mtoto alikuwa anakwenda shule fulani mkoa fulani, nauli kawaida ni x lakini Leo ilikuwa Y na bei elekezi ni Z.
Kwa uelewa wangu mdogo Leo imekuwa siku kurudi shule za bweni, na mabasi Mengi yamekodishwa, na shule nyingi kwa utaratibu wao wanafunzi wanasindikizwa na mwalimu au kiongozi aliye chaguliwa na shule, hivyo gharama zaidi ni kwa sababu ya uwepo wa msindikizaji na uzuri mwingine basi linawashushia wanafunzi shule.
La kama unaona hii ni dhuluma unaweza mpandisha mtoto basi lingine akajiongoza mwenyewe au ukasafiri naye na ukashuka naye stand , ukatafuta Usafiri wako au jumuiya kumfikisha mwanao shule.
 
Mamlaka za nchi hazijawahi kulala. Zinawachora tu wanaopandisha bei kiholela. Muda sio mrefu watalia na kusaga meno.

Mama hataki dhuluma na uonevu.

Acha kujipendekeza na kujikombakomba kwa mwanadamu!

Kama hujui kuwa kwa kuongeza bei ya mafuta serikali ilijua pia itakusanya kozi ya VAT kwenye nauli basi u mjinga sana!! Subiri kusikia SUMATRA ikitoa bei elekezi sasa hivi.

Ongezeko la bei ya bidhaa za mafuta huongeza bei ya bidhaa na huduma!! Ujinga wa kiasi hiki mnautoa wapi jamani??
 
Back
Top Bottom