Wamisionari waliofika Tanganyika walikuta watu wamestaarabika na wanajua kusoma na kuandika

Wamisionari na wakoloni waliwaonea wivu waislam kwa kuajiriwa na wajerumani,au mimi ndo sijaelewa?
 
Wamisionari na wakoloni waliwaonea wivu waislam kwa kuajiriwa na wajerumani,au mimi ndo sijaelewa?
Nan...
Wamisionari mfano wa Johann Krapf wamekuja Afrika wakiita Dark Continent wakiamini wanakuja kuwastaarabisha watu waliokuwa washenzi hawana mila, desturi wala historia.

Krapf alipofika Zanzibar akapewa barua na Sultan Barghash ampelekee Chief Kimweri Vuga.

Anafika Vuga Chief Kimweri anaipokea barua na anaisoma.

Barua imeandikwa kwa Arabic Script.

Chief Kimweri yuko katika Barza yake anahukumu kesi na anajua kusoma na kuandika na ni Muislam anamuamini Mungu Mmoja.

Alikotoka kwao Ujerumani kaacha shule Vuga anakuta madrasa zinasomesha watoto zile 3Rs, yaani Reading, Writing na Arithmetic.

Liko wapi hilo Black Continent.

Haliko Zanzibar wala Vuga kote kakuta utawala unaoendesha serikali na raia wanatii hizo mamlaka.

Ikiwa hujaelewa usione tabu kuuliza.
 
Sultan Barghash wa Oman ndio alikua mtawala enzi hizo unaambiwa hata hio Dar es Salaam ilikua chini ya Sultan Majid bin Said yeye ndio Founder wa Dar es Salaam, elewa neno Founder
Wazungu wakituita waafrika shit hole country mnasema wanatubagua.

Yani mtu katoka Oman anakuja kutawala Dar es salaam alafu unaona kitu Cha kujivunia.

Waarabu wamekuja waliwakuta wazee na dini zao za asili, lakini kwa ujinga wa wazee wetu wanaacha asili na wao wakaanza kujiona waarabu. Vivyohivyo kwa wakristu.

Hii issue ya Samia ya Samia kukutana na Papa, Mimi kama mkotoliki naiona issue ya kawaida kabisa Haina uzito wowote, lakini huyu Mzee mleta mada anachambua kama siyo kitu Cha kawaida.

Ninashangaaga sana kwanini waislamu wanakuwa watu wa kujishtukia sana. Wakati hao wanaowaongelea hawana hata habari nao.
 
Kiongozi una interview ulizowahi kufanya kwa kingereza naomba link nikakusikilize tafadhali
 
Kwako unaona ni kitu cha kawaida Ila kwao ni endorsement moja kubwa sana,
 
Mtu ukishakua mdini, hata uandike maandiko ya maana watu watayapuuza tu
πŸ˜πŸ˜…πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜…πŸ˜…Ndiyo Ukweli Wenyewe, Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Madrasa hufundisha Quraan na Kiarabu na sio English,Hisabati au sayansi.... Watoto wa Kiislam wengi walizuiwa na wazazi wao kusoma shule za misheni kwa kuwaambia kuwa watakuwa wakristo..... Kama kusoma na kuandika ni Kiarabu lakini sio lugha ingine.Kumbuka kuwa Vatican ni Nchi kama Nchi ingine na Mataifa yote yana Balozi zake Vatican.Tatizo la Waislam ni kuona kila kitu wanadhurumiwa , mnalalamika sana bila kuchukuwa hatua za kujikwamua na madhira yanayowakabili
 
Tupe link za English mzee , tusibitoshe kama kweli wewe ni msomi na Wakaloni walikukuta unajua soma na kuandika English na kijerumani
Hahaha
Unataka kusema nini?

Kuwa vitabu vyake vya kizungu kaandikiwa?

Au hajawahi kuhojiwa na VoA?

Sijajua mantiki ya hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…