Uchaguzi 2020 Wana Arusha tumrudishieni Dkt. John Magufuli asante ya kufikisha usafiri wa treni Arusha, kwa kuifuta CHADEMA hapa mjini

Hamna kitu kinachoitwa leli..sijui unaongelea kitu gani..pia maandishi yako yapange vizuri.
 
Arusha ni jimbo la Lema na hayo maendeleo kayaleta yeye mbunge wetu sifa na pongezi ziende kwa Lema
 
Arusha ni jimbo la Lema na hayo maendeleo kayaleta yeye mbunge wetu sifa na pongezi ziende kwa Lema
Akili ya Lema ni ndogo kuliko unyeti wa mji anaungoza..ndio maana hakuweza kufanya kitu chochote Arusha mpaka sasa.
 
Tajiri Tanzanite,

Mmmmh! Kumbe hujui siasa wewe, bila kuwepo kwa Chadema nyingi Arusha hiyo reli isingefufuliwa Leo Wala kesho. Kuifufua reli Ni njia ya kukutongoza wewe. Vijana kuweni na akili, siasa sio Kama Simba na Yanga. Bila lema hiyo reli unayosema isingepelekwa, hata elimu ndogo Kama hiyo huna?
 
Arusha tunamchagua Lema sababu tunamtaka mchapa mdomo mzur kuhusu kero zetu nikukumbushe we jamaa maendeleo yanaletwa na kodi zetu na haijawai tokea chadema wakawa wakusanya kodi wa nchi hii,Lisu tunamchagua sababu ya uboya wenu huu mnakusanya kodi zetu alaf mnatakwa muabudiwe wakati sisi wananchi kiuhalisai ndo maboss wenu ila siku izi ata uhuru wetu wakuongea mnaubana mmelewa madaraka nyie
 
Tajiri Tanzanite,
Reli ilikuwepo Arusha tangu tunapata Uhuru, kwani ilikwenda wapi? Nani aliiharibu? Nani aliiachia ife? Sababu zipi ziliiua?
 
Shuka Madini mkuu, tupe shule
 
Kiwand cha general Tyre ikisimama hyo Ni bonge la kiwanda siasa cmezababishwa had kiwanda kishindwe kuoperate
 
Tajiri Tanzanite,

Kwani huo usafiri huko Arusha uliondolewa na serikali ya chama gani na sasa umerudishwa na serikali ya chama gani hebu usijitoe fahamu tatizo limetengenezwa na wenyewe halafu mkilitatua mnataka kupewa credit ya nini kwanza mnadaiwa kwanini miaka 30 mliondoa huo usafiri wa train na kuongeza garama ya maisha ya watu wa chuga. Hiyo ni sabu tosha ya kuwapumzisha. Tulidhania mliondoa sababu mliona haina Faida kumbe ilikuwa bado na faida Kwahiyo mliondoa kwa makosa adhabu inawahusu.
 
Tajiri Tanzanite,

Kura haitolewi kama ahsante/ shukrani.
Hutolewa kwa sera nzuri na uwakilishi.
Mh Rais amefunga Beureau De change nyingi hapo arusha. Na bado kuna mahitaji mengi kuliko hiyo treni.
 
Tajiri Tanzanite,

Huyu unaemtaka yeye anawaza kwao Chato.

Hata Wanyama anahamisha kupeleka huko ili watalii waennde chato badala ya Arusha Na kilimanjaro.

Na uwanja wa kimataifa wa amejenga kwa lengo hilo.

Muwe mnafikiri na kuwaza kabla kupenda


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mbona watawala watangulizi hawakupenda kusifiwa hivi. Kwa nini utawala huu unataka na kung'ang'ania sana kusifiwa. Hivi hii ni nini sasa! Kuna nini? Yaani ushamba uliooneshwa juzi wa kuita wasanii na kutumia fedha zote hizo wakati mama zetu huku mavijijini hawana dawa na wanajifunika mashuka ambayo ni vitambaa walivyopewa na CCM ni ushamba kweli kweli.
 
Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi, watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei. Chadema kweli ina wanachama wenye akili ndogo kweli.
Hizi treni zilikuwepo na sasa ni kampeni ila kwa usafiri mzuri na comftable kutoka Dar to Arusha baada ya ndege ni Buses.
Na kwa usalama zaidi ni Buses.
Treni ya mwaka 47 na spidi ya kiberenge sio ya kudanganya watu wazima.
Hii reli ya Mjerumani imepitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna majimbo ambayo ccm imeyakalia kwa miaka mingi mfano Mtwara, lindi, Ruvuma, Mara, Tabora, Rukwa nk mbona yana hali mbaya sana?
 
Kodi zimekusanywa na ccm tangu uhuru hadi leo lkn hamna lolote walilofanya zaidi ya kugawana kodi zetu na kujaza matumbo yao,
hawa ndio vivuruge wa maisha ya watanzania huu ndio wakati wa kuiondoa CCM madarakani

#2020 NI YEYE YULE TUNDU LISU ✌️
CDM inakusanya kodi? Uwezo wako wa kufikiri upo chini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…