Uchaguzi 2020 Wana Arusha tumrudishieni Dkt. John Magufuli asante ya kufikisha usafiri wa treni Arusha, kwa kuifuta CHADEMA hapa mjini

Uchaguzi 2020 Wana Arusha tumrudishieni Dkt. John Magufuli asante ya kufikisha usafiri wa treni Arusha, kwa kuifuta CHADEMA hapa mjini

Swali je ameweka leli mpya? Kama jibu Hapana leli ilikuwa toka zamani unatakiwa kujiuliza kwnn hapo mwanzo ilikufa? Unatakiwa ujue hivi cc wanainch toka tupate Uhuru WA taifa hili hicho ndio chama tulixhokuwa nacho madarakani,ukiona unaposikia watu wanalipwa mishahara hewa ujue ni wao, mikataba mibovu ya madini ambapo tumepoteza mamilion ya Shilingi ujue kazi ya utawala huu WA chama hicho,ukisikia ufisadi jua utawala wa chama kilichokuwa madarakani ukisikia wafanyakazi wenye vyet feki ujue ni wao waliokuwa madarakani viwanda Vingi vimekufa wao , ndio waliviuwa baada ya kushindwa kuviendesha kutoka kwa wakoloni, unamkumbuka yule aliesema wanainchi wale majani lkn ndege za kutembelea raisi lazima inunuliwe ile ndege ipo wapi kwa sasa imesaidia nn kwa taifa lkn ilinunuliwa kwa pesa ya selikali

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Hamna kitu kinachoitwa leli..sijui unaongelea kitu gani..pia maandishi yako yapange vizuri.
 
Arusha ni jimbo la Lema na hayo maendeleo kayaleta yeye mbunge wetu sifa na pongezi ziende kwa Lema
 
Arusha ni jimbo la Lema na hayo maendeleo kayaleta yeye mbunge wetu sifa na pongezi ziende kwa Lema
Akili ya Lema ni ndogo kuliko unyeti wa mji anaungoza..ndio maana hakuweza kufanya kitu chochote Arusha mpaka sasa.
 
Tajiri Tanzanite,

Mmmmh! Kumbe hujui siasa wewe, bila kuwepo kwa Chadema nyingi Arusha hiyo reli isingefufuliwa Leo Wala kesho. Kuifufua reli Ni njia ya kukutongoza wewe. Vijana kuweni na akili, siasa sio Kama Simba na Yanga. Bila lema hiyo reli unayosema isingepelekwa, hata elimu ndogo Kama hiyo huna?
 
Arusha tunamchagua Lema sababu tunamtaka mchapa mdomo mzur kuhusu kero zetu nikukumbushe we jamaa maendeleo yanaletwa na kodi zetu na haijawai tokea chadema wakawa wakusanya kodi wa nchi hii,Lisu tunamchagua sababu ya uboya wenu huu mnakusanya kodi zetu alaf mnatakwa muabudiwe wakati sisi wananchi kiuhalisai ndo maboss wenu ila siku izi ata uhuru wetu wakuongea mnaubana mmelewa madaraka nyie
 
Tajiri Tanzanite,
Reli ilikuwepo Arusha tangu tunapata Uhuru, kwani ilikwenda wapi? Nani aliiharibu? Nani aliiachia ife? Sababu zipi ziliiua?
 
" Arusha imekuawa na historia mbaya ya machafuko ya kisiasa ".
Wewe na serikali yako ya ccm nani mkweli? Maana serikali kila siku inahubiri amani na kutaka watalii wa ndani nje watembelee vivutio vilivyomo ndani ya nchi. Lakini wewe unapingana na serikali yako unapodai kwamba kuna machafuko.

"Tunakumbuka Arusha kwa miaka ya nyumba ilikuwa ni mji ambao serikali ilipendekeza kufanyia mikutano yake ya kimataifa".
Kama kuna kikundi kidogo ambacho kinaweza kuizuia serikali kuendelea na mipango yake kama ilivyo jipangia, je serikali hiyo ina pata uhalali gani wa kuongoza hali yakuwa inashindwa hata kudhibiti kikundi kidogo chenye kuleta machafuko (kuvuruga amani) ndani ya nchi?

"Kitendo cha Rais Magufuli kufufua Reli na kufikisha Arusha".
Kufufua reli maana yake ni kwamba alikuwa imekufa. Swali la msingi, je ni nani aliua usafiri wa treni kuja Arusha? Kivyovyote vile jibu litakuwa ni serikali ya ccm. Je ccm inapataje uhalali wa kubaki madarakani kwa kuua mradi huu kwa miaka karibia 26?

"Hawa wapinzani hawajawahi kuleta maendeleo yeyote hapa Arusha".
Linapokuja suala la maendeleo ndani ya nchi huwa ni jukumu la serikali kutekeleza hayo. Mbunge ni muwakilishi kati ya serikali na wananchi walio mtuma kuwawakilisha bungeni. Na kwa kupitia bunge, mbunge anawasilisha kero za wananchi kwa serikali ili izifanyie kazi. Je serikali yako ya ccm inazifanyia kazi kero za wananchi zinazowasilishwa na mbunge wa upinzani? Je serikali yako ya ccm inashirikiana vipi na mbunge wa upinzani ambae ndiye muwakilishi wa wananchi kuleta maendeleo katika kila jimbo husika?

"Hizo barabara zilizojengwa ndani ya mji wa Arusha ambayo chadema inatumia kama ngao,ya kuwadanganyia hao wafuasi wake ni project ya World Bank iliyoanza kipindi cha Kikwete."

Hivi kuna mradi wowote ndani ya nchi hii unafanyika/uliofanyika bila msukumo wa wahisani kutoka nje? Unajua hata elimu yetu kuna mkono wa wahisani ndani yake? Unajua hata afya zetu kutengemaa kuna mkono wa wahisani ndani yake? Nk? Miaka zaidi ya 50 kuwa huru bado tumekuwa omba omba. Licha ya misaada bado kuna mikopo. Unajua serikali ya ccm mpaka sasa imekopa kiasi gani? Wewe kama mwananchi unajua unadaiwa kiasi katika deni lililo sababishwa na serikali yako ya ccm?

Yaani maswali ni mengi mno, acha tu niishie hapo.
Shuka Madini mkuu, tupe shule
 
Kiwand cha general Tyre ikisimama hyo Ni bonge la kiwanda siasa cmezababishwa had kiwanda kishindwe kuoperate
 
Tajiri Tanzanite,

Kwani huo usafiri huko Arusha uliondolewa na serikali ya chama gani na sasa umerudishwa na serikali ya chama gani hebu usijitoe fahamu tatizo limetengenezwa na wenyewe halafu mkilitatua mnataka kupewa credit ya nini kwanza mnadaiwa kwanini miaka 30 mliondoa huo usafiri wa train na kuongeza garama ya maisha ya watu wa chuga. Hiyo ni sabu tosha ya kuwapumzisha. Tulidhania mliondoa sababu mliona haina Faida kumbe ilikuwa bado na faida Kwahiyo mliondoa kwa makosa adhabu inawahusu.
 
Tajiri Tanzanite,

Kura haitolewi kama ahsante/ shukrani.
Hutolewa kwa sera nzuri na uwakilishi.
Mh Rais amefunga Beureau De change nyingi hapo arusha. Na bado kuna mahitaji mengi kuliko hiyo treni.
 
Tajiri Tanzanite,

Huyu unaemtaka yeye anawaza kwao Chato.

Hata Wanyama anahamisha kupeleka huko ili watalii waennde chato badala ya Arusha Na kilimanjaro.

Na uwanja wa kimataifa wa amejenga kwa lengo hilo.

Muwe mnafikiri na kuwaza kabla kupenda


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mbona watawala watangulizi hawakupenda kusifiwa hivi. Kwa nini utawala huu unataka na kung'ang'ania sana kusifiwa. Hivi hii ni nini sasa! Kuna nini? Yaani ushamba uliooneshwa juzi wa kuita wasanii na kutumia fedha zote hizo wakati mama zetu huku mavijijini hawana dawa na wanajifunika mashuka ambayo ni vitambaa walivyopewa na CCM ni ushamba kweli kweli.
 
Reli inakusaidia kupata hicho chakula kirahisi, watu watasafirisha mizigo kwa bei rahisi bidhaa na chakula zitashuka bei. Chadema kweli ina wanachama wenye akili ndogo kweli.
Hizi treni zilikuwepo na sasa ni kampeni ila kwa usafiri mzuri na comftable kutoka Dar to Arusha baada ya ndege ni Buses.
Na kwa usalama zaidi ni Buses.
Treni ya mwaka 47 na spidi ya kiberenge sio ya kudanganya watu wazima.
Hii reli ya Mjerumani imepitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mpinzani ila mpinzani mwenye akili timamu, kweli kabisa chadema na upinzani vifutwe arusha, arusha imekua kama vile jiji la wahuni sababu ya chadema, hata mambo ya msingi kabisa wanapinga furaha yao wakishangiliwa na bodaboda na vurugu basi ..sisikii maendeleo ya mkoa wa arusha hata huyo mbunge sijui amefanya nini miaka 10 ya kukaa kwake
Kuna majimbo ambayo ccm imeyakalia kwa miaka mingi mfano Mtwara, lindi, Ruvuma, Mara, Tabora, Rukwa nk mbona yana hali mbaya sana?
 
Kodi zimekusanywa na ccm tangu uhuru hadi leo lkn hamna lolote walilofanya zaidi ya kugawana kodi zetu na kujaza matumbo yao,
hawa ndio vivuruge wa maisha ya watanzania huu ndio wakati wa kuiondoa CCM madarakani

#2020 NI YEYE YULE TUNDU LISU ✌️
CDM inakusanya kodi? Uwezo wako wa kufikiri upo chini sana
 
Back
Top Bottom